Ukitaka kuondoa ujinga kitu cha kwanza
1. Futa kazi wote wanaosimamia elimu nchi hii.
2. Andaa kamati ya kubaini watu wenye akili ( sio wenye vyeti) bali watu waliojaribu kuleta tofauti kwenye ubunifu mfano Kipanya na wengine wengi,kisha wape jukumu la kufikiri na kutoa mapendekezo yatakayofaa kwenye elimu.
Kamati inaapishwa,ikichakachua ikatuletea maprofesa wa hovyo waliopo,wanakula shaba wote.
3. Unafuta kabisa mfumo wa elimu uliopo.Mtu anaanza kujifunza kutengeneza simu,magari na vitu mbali mbali akiwa darasa la tatu.Anaanza kujifunza udaktari tangu darasa la tatu.Sio unampotezea muda mtoto anajifunza sungura mjanja au vishazi na ngeli!Upuuzi mtupu!
4. Mtu akitamba ana hela atuoneshe kitu alichokibuni cha uzalishaji chenye faida kwa jamii.Kama hakuna anafilisiwa na kufungwa jela ya kilimo na kazi ngumu.Hakuna pesa ya ujanja ujanja.Ama
5. Watu wote wanaodanga watulie kama hawapo wakionekana wanatamba mtandaoni sijui wanataka kuwa na wanaume wenye gari namba E tena gari ya maana,wakabidhiwe ekari kumi kila mmoja walime na kuzitunza ama wale shaba wote hatutaki watu wanafanya wanaume wanafanya lolote kupata pesa ikiwepo kutoa kafara.
6. Machawa wote peleka jela ya kilimo.Lazima kazi iheshimiwe sio mtu anapata pesa kirahisi rahisi tu.