Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Niliwahi kuiuliza ChatGPT, kwakuwa ni mada sensitive ikawa inaleta majibu ya kiungwana. Ila ukweli ni kwamba Waafrika mbongo zetu hatuzitumii ipasavyo.
Mimi naamini: mazingira, mfumo wa maisha, elimu, na umasikini ndiyo vyanzo vikuu vya Waafrika kuwa nyuma katika mambo ya msingi.
1. Mazingira yanayomzunguka mtu yana nafasi kubwa sana kuchangia fikra, maamuzi na matendo ya mtu. Huwezi kuwa influenced kubuni Teknolojia kubwa kupiku nyingine ikiwa the biggest achievement kwenye taifa ni kumiliki gari, nyumba n.k.
2. Mfumo wa maisha ya Waafrika ni kuamka, kunywa chai, kazi, kula mchana, kazi, kula usiku, kulala, kesho mzunguko unaanzia palepale kwa muda wa mwaka mzima: hapa tunazungumzia waganga njaa ambao bila kutoka kitandani basi siku hiyo ni hohehahe tu na hii ndiyo namba kubwa ya Waafrika wanaishi hivi. Hapa ndiyo unapata taifa la watu ambao mwaka mzima anafanya kazi non-stop, akipata muda wa kupumzika kichwani anawaza atalipaje bills za mwezi ujao akiwa tayari ana madeni na mshahara umeisha.
3. Elimu, hii wala haina haja kuelezea. Teknolojia imekuja ku-expose elimu yetu vibaya mno, wachache wenye nacho wanapeleka watoto wao International Schools, wengine wanakimbilia nje kupata angalau vyeti vya kimataifa kwa ngazi za juu.
4. Umasikini. Hapa ndiyo tatizo lilipo, Waafrika bado tunasumbuliwa na mambo mengi madogomadogo kutokana na umasikini. Huwezi kuwaza mambo makubwa ikiwa mlo wa siku tu ni shida, huo mlo kamili wa kufanya mwili wa binadamu ufanye kazi ipasavyo ndiyo haupatikani kabisa.
Haya matatizo siyo kwamba nchi zilizoendelea hayapo ila wenzetu wamefika sehemu namba kubwa ya raia wao wanapata mahitaji yote muhimu: mlo kamili, elimu bora, makazi bora na huduma zote za kijamii, afya bora; wenzetu wanafanya mpaka therapy kwaajili ya afya ya akili huku afya inayozingatiwa ni ya mwili tu na hapo ni hadi mtu azidiwe ndiyo anatafuta hospitali ilipo.
Akili ya binadamu inahitaji focus ya hali ya juu sana kufanya kazi ipasavyo, Mwafrika ni rahisi sana kuwa distracted kulingana na mazingira aliyopo.