Hivi Waafrika hatuna akili?

Hivi Waafrika hatuna akili?

Niliwahi kuiuliza ChatGPT, kwakuwa ni mada sensitive ikawa inaleta majibu ya kiungwana. Ila ukweli ni kwamba Waafrika mbongo zetu hatuzitumii ipasavyo.

Mimi naamini: mazingira, mfumo wa maisha, elimu, na umasikini ndiyo vyanzo vikuu vya Waafrika kuwa nyuma katika mambo ya msingi.

1. Mazingira yanayomzunguka mtu yana nafasi kubwa sana kuchangia fikra, maamuzi na matendo ya mtu. Huwezi kuwa influenced kubuni Teknolojia kubwa kupiku nyingine ikiwa the biggest achievement kwenye taifa ni kumiliki gari, nyumba n.k.

2. Mfumo wa maisha ya Waafrika ni kuamka, kunywa chai, kazi, kula mchana, kazi, kula usiku, kulala, kesho mzunguko unaanzia palepale kwa muda wa mwaka mzima: hapa tunazungumzia waganga njaa ambao bila kutoka kitandani basi siku hiyo ni hohehahe tu na hii ndiyo namba kubwa ya Waafrika wanaishi hivi. Hapa ndiyo unapata taifa la watu ambao mwaka mzima anafanya kazi non-stop, akipata muda wa kupumzika kichwani anawaza atalipaje bills za mwezi ujao akiwa tayari ana madeni na mshahara umeisha.

3. Elimu, hii wala haina haja kuelezea. Teknolojia imekuja ku-expose elimu yetu vibaya mno, wachache wenye nacho wanapeleka watoto wao International Schools, wengine wanakimbilia nje kupata angalau vyeti vya kimataifa kwa ngazi za juu.

4. Umasikini. Hapa ndiyo tatizo lilipo, Waafrika bado tunasumbuliwa na mambo mengi madogomadogo kutokana na umasikini. Huwezi kuwaza mambo makubwa ikiwa mlo wa siku tu ni shida, huo mlo kamili wa kufanya mwili wa binadamu ufanye kazi ipasavyo ndiyo haupatikani kabisa.

Haya matatizo siyo kwamba nchi zilizoendelea hayapo ila wenzetu wamefika sehemu namba kubwa ya raia wao wanapata mahitaji yote muhimu: mlo kamili, elimu bora, makazi bora na huduma zote za kijamii, afya bora; wenzetu wanafanya mpaka therapy kwaajili ya afya ya akili huku afya inayozingatiwa ni ya mwili tu na hapo ni hadi mtu azidiwe ndiyo anatafuta hospitali ilipo.

Akili ya binadamu inahitaji focus ya hali ya juu sana kufanya kazi ipasavyo, Mwafrika ni rahisi sana kuwa distracted kulingana na mazingira aliyopo.
 
Niliwahi kuiuliza ChatGPT, kwakuwa ni mada sensitive ikawa inaleta majibu ya kiungwana. Ila ukweli ni kwamba Waafrika mbongo zetu hatuzitumii ipasavyo.

Mimi naamini: mazingira, mfumo wa maisha, elimu, na umasikini ndiyo vyanzo vikuu vya Waafrika kuwa nyuma katika mambo ya msingi.

1. Mazingira yanayomzunguka mtu yana nafasi kubwa sana kuchangia fikra, maamuzi na matendo ya mtu.

2. Mfumo wa maisha ya Waafrika ni kuamka, kunywa chai, kazi, kula mchana, kazi, kula usiku, kulala, kesho mzunguko unaanzia palepale kwa muda wa mwaka mzima: hapa tunazungumzia waganga njaa ambao bila kutoka kitandani basi siku hiyo ni hohehahe tu na hii ndiyo namba kubwa ya Waafrika wanaishi hivi. Hapa ndiyo unapata taifa la watu ambao mwaka mzima anafanya kazi non-stop, akipata muda wa kupumzika kichwani anawaza atalipaje bills za mwezi ujao akiwa tayari ana madeni na mshahara umeisha.

3. Elimu, hii wala haina haja kuelezea. Teknolojia imekuja ku-expose elimu yetu vibaya mno, wachache wenye nacho wanapeleka watoto wao International Schools, wengine wanakimbilia nje kupata angalau vyeti vya kimataifa kwa ngazi za juu.

4. Umasikini. Hapa ndiyo tatizo lilipo, Waafrika bado tunasumbuliwa na mambo mengi madogomadogo kutokana na umasikini. Huwezi kuwaza mambo makubwa ikiwa mlo wa siku tu ni shida, huo mlo kamili wa kufanya mwili wa binadamu ufanye kazi sawasawa ndiyo haupatikani kabisa.

Haya matatizo siyo kwamba nchi zilizoendelea hayapo ila wenzetu wamefika sehemu namba kubwa ya raia wao wanapata mahitaji yote muhimu: mlo kamili, elimu bora, afya bora; wenzetu wanafanya mpaka therapy kwaajili ya afya ya akili huku afya ni mwili tu na hapo ni hadi mtu azidiwe ndiyo anatafuta hospitali ilipo.

Akili ya binadamu inahitaji focus ya hali ya juu sana kufanya kazi ipasavyo, Mwafrika ni rahisi sana kuwa distracted kulingana na mazingira aliyopo.
nimeanza-kuamini-ulegelege-wetu-waafrika-kama-bara-katika-maendeleo-unatokana-na-wastani-wa-iq-ya-umma-kuwa-chini-sana-sehemu-ya-ii.2281226

eads/hitimisho-la-uchunguzi-jiografia-kama-sababu-kuu-ya-kudumaa-kwa-maendeleo-ya-afrika-tumtue-kidogo-mkoloni-mzigo-wa-lawama.2281764
 
Habari za ijumaa wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka ni kwanini hatuna akili?

Siongelei akili ya darasani, Bali naongelea akili yenye impact katika maisha ya binadamu.

Hakuna teknolojia yoyote ambayo mwafrika amefanikiwa kuanzisha, Yani inshort ni kuwa sisi Waafrika huenda tupo hivi kiasili.

Mwafrika mtu asiyekuwa na akili zaidi katika uso wa dunia.
Hujajua mambo mengi. Waafrika tuna akili na tunagundua vingi. Lakini mzungu hayuko tayari mwafrika atangeze kugundua mbele yake. Ama uyahongwa unyamaze qatangaze wao, ukileta ubishi utazikwa. Labda uwe ugunduzi ambao hauna madhara sana kiuchumi.

Mpemba formular, sijui kama inaijua. Jamaa wa Tanga, katika kuhangaika na majukumu ya kigamilia , alikuja kugundua kuwa maziwa ya moto yakiwekwa kwenye friza huganda haraka kuliko maziwa ya baridi. Aliwaumiza wazungu kichwa kutafuta ni kwa nini. Mwishowe walimchukua na yeye na sidhani kama amerudi. Walimpa ajira hukohuko.
Mwalimu Nyerere na baadhi ya marais wa Afrika baada ya nchi zao kupata uhuru, waliweka mikakati ya kwenda mbio kimaendeleo. Kilichowakuta ni kupinduliwa na kuuawa ama vikwazo vya upatikanaji wa vipuli vya miyambo ya viwanda vyao ili vife.

Elimu yetu inatawaliwa na wao bila sisi kujijua. Wanatoa misaada na masharti ya namna ya kuifanya hiyo elimu. Elimu yao ni siri yao na hata hawa waafrika wanaoenda kusoma nje, husoma mtaala wa jumla na kurudi huku wenyeji wakibaki na workshop, shortcourses na seminas zinazowapa ujuzi wa ziada zaidi ya ule mtaalaal ambao tunajifanya tunasoma scholarship.

Bwawa la mwl Nyerere lingekwishajengwa miaka hiyo. Wazungu waliweka ngumu wakidai ni uharibifu wa mazingira. Ukibisha kuna mahali utakula kibano hadi unyooshe maelezo. Utanyimwa msaada au mkopo ambao ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.

Misaada ya maendeleo kwa nchi zetu ni midogo sana na imejaa masharti magumu. Kwa mfano, unapewa msaada wa kujenga barabara, na sharti mojawapo ni kununua baadhi ya mahitaji kutoka nchi au kampuni ya ulikotoka msaada. Au unapewa msaada kwa sharti la kutoa rasilimali za nchi na kwa vyovyote zitakuwa na thamani kubwa kuliko msaada. Ndivyo tunavyopigwa na kubaki maskuni.

Ni vitu ambavyo haviko wazi na baadhi huvipuuza ila ndivyo vyanzo vya sisi kuonekana hatuna akili na hatuna ubunifu.

Shida inakuja kuwa kubwa kutokana na viongozi wetu kuwa walafi wa mali na fedha za nchi na kujilimbikizia pasipo kujali hali za wananchi wao.

Povu ruksa.
 
Unaanza ongea mambo ya kale baada ya Uhuru watanzania mmeshindwa panga Mitaa au kusambaza Maji wakati vyanzo mnavyo.. mmeshindwa tengeneza vyuma wakati chuma na makaa ya mawe mnayo. Mmeshindwa kuendesha uchimbaji WA madini Kwa manufaa ya taifa mmeachia wahindi na wachina. Bandari mmegawa Kwa waarabu na wanyama mnauza Kwa promotion. Ukitaka kujua Jamii imejaa wapumbavu Angalia maamuzi yao
Kwani hoja imesema waAfrika wa mwaka upi? 2025? Basi ngoja huu mwaka uishe tuone. Otherwise nachukulia ni waAfrika wa miaka yote, iwe kale au jana, ni waAfrika.

Hayo mengine yote ni masuala ya ubinafsi na rushwa tu, na sio kukosa akili., maana hata kuiba pesa za miradi ya maji na barabara inahitaji akili pia. Mfano lile jizi Andrew Chenge, kasoma hadi Havard, hana akili yule?

Usichanganye Uadilifu na Akili!
 
Habari za ijumaa wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka ni kwanini hatuna akili?

Siongelei akili ya darasani, Bali naongelea akili yenye impact katika maisha ya binadamu.

Hakuna teknolojia yoyote ambayo mwafrika amefanikiwa kuanzisha, Yani inshort ni kuwa sisi Waafrika huenda tupo hivi kiasili.

Mwafrika mtu asiyekuwa na akili zaidi katika uso wa dunia.
Sasa na wewe hilo la kuuliza?
Akili tuzitoe wapi?
 
Wapo watu weusi walikulia nchi za ughaibuni na wamefanya gunduzi tunazozitumia leo. Mfano Lewis Latimer alibuni bulb zinazotumia filament na hata three light traffic light imegunduliwa na mtu mweusi bila kumsahau Ben Carson neurologist aliyeishangaza dunia.
Ben Carson nadhan hakuwa wa kwanza kutenganisha watoto vichwa. Ila alikuwa mweusi wa kwanza.
 
Ben Carson nadhan hakuwa wa kwanza kutenganisha watoto vichwa. Ila alikuwa mweusi wa kwanza.
Alitenganisha mapacha ambao madaktari bingwa duniani walisema hawawezi kutenganishwa ila yeye akafanya hayo maajabu soma kitabu chake cha GIFTED HANDS.
 
Wazungu wenyewe hawapendi sisi tuwe wagunduzi na hii yote nikutokana na kutokuwa na imani na mtu mweusi

Hivi unadhani tukiwa wagunduzi wazungu watatusapoti ikiwa sisi kwa sisi hatusapotiani.
Acha tuwe hivihivi kama manyumbu, uchawi kwa sana

Yaani mtu nweusi hususani Tz akiona mtoto wajilani anafanya vizuri darasani anamroga, sasa huo ugunduzi utatoka wapi
Kwani mzungu alisapotiwa na nani mpaka akafika hapo alipo? Jibebe mwenyewe aacha kumsingizia mtu.
 
Ili tuendelee tunahitaji kuondoa vitu vitatu tu akilini mwetu
1.Roho mbaya
2.Uongo.
3.Wizi
Hapa serikali inatakiwa kuwa ya kikatiri kupita kiasi bila hivyo tutabaki tulivyo milele.
 
Kwani hoja imesema waAfrika wa mwaka upi? 2025? Basi ngoja huu mwaka uishe tuone. Otherwise nachukulia ni waAfrika wa miaka yote, iwe kale au jana, ni waAfrika.

Hayo mengine yote ni masuala ya ubinafsi na rushwa tu, na sio kukosa akili., maana hata kuiba pesa za miradi ya maji na barabara inahitaji akili pia. Mfano lile jizi Andrew Chenge, kasoma hadi Havard, hana akili yule?

Usichanganye Uadilifu na Akili!

Changamoto ya mwafrika ni kwenye taasisi, tunahitaji waafrika wengi wenye IQ nyingi kwenye nyadhifa mbalimbali kuanzia viongozi wa juu mpaka watendaji , changamoto yetu nafasi hizi hazitolewi kutokana na ubora wa vile vilivyopo vichwani kwa watu bali zinatolewa kwa misingi ya "anayepata nafasi anajuana na nani"
 
Habari za ijumaa wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka ni kwanini hatuna akili?

Siongelei akili ya darasani, Bali naongelea akili yenye impact katika maisha ya binadamu.

Hakuna teknolojia yoyote ambayo mwafrika amefanikiwa kuanzisha, Yani inshort ni kuwa sisi Waafrika huenda tupo hivi kiasili.

Mwafrika mtu asiyekuwa na akili zaidi katika uso wa dunia.
Wewe Tu Ndo Akili Huna Mara Nyingi Machizi Hivyo Ndivyo Wanawazaga.
 
Habari za ijumaa wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka ni kwanini hatuna akili?

Siongelei akili ya darasani, Bali naongelea akili yenye impact katika maisha ya binadamu.

Hakuna teknolojia yoyote ambayo mwafrika amefanikiwa kuanzisha, Yani inshort ni kuwa sisi Waafrika huenda tupo hivi kiasili.

Mwafrika mtu asiyekuwa na akili zaidi katika uso wa dunia.
Sio wote wengine tuna akili kuzidi wazungu na wachina.
 
Kuna jambo kubwa linalozidi ujenzi wa Mapyramid? Hadi leo hakuna mtu mwenye uelewa wa jinsi walivyopandisha mablock ya tani kadhaa hadi juu…,Na usidanganyike ukafikiri hawa wamisri waarabu ndio walikuwa mafarao, Mafarao walikuwa ni waAfrika weusi wenye asili ya kama watu wa Sudan hivi..
Acheni kujidanganya, kwamba Mafarao walikuwa weusi then wakakimbia nchi au waliuliwa!? Mbona leo hawapo wala vizazi vyao havipo? Historia huwa haifutiki.
 
Kama ukisoma biblia kwa utulivu, utabaini kuwa waafrika tumelaaniwa. Waafrika tumetokana na ukoo wa yule mtoto wa Nuhu aliyelaaniwa na baba yake baada ya kumkuta akiwa uchi....yeye badala ya kumfunika, akaanza kumcheka...na kuishiwa kulaaniwa milele.
Tunajadili uhalisia hapa, hizo story za kusadikika baki nazo
 
Habari za ijumaa wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka ni kwanini hatuna akili?

Siongelei akili ya darasani, Bali naongelea akili yenye impact katika maisha ya binadamu.

Hakuna teknolojia yoyote ambayo mwafrika amefanikiwa kuanzisha, Yani inshort ni kuwa sisi Waafrika huenda tupo hivi kiasili.

Mwafrika mtu asiyekuwa na akili zaidi katika uso wa dunia.
waafrika tuna akili sana,angalia pyramids za misri,kulikuwa na biashara kubwa sana mangaribi ya afria wakati huokukiwa na tajiri mkubwa mansa musa,unaambiwa ata mayahudi asili yao ni afrika,ata malikia wa sheba alizaa na mfalme daudi,,,unaambiwa ata YESU mwenyewe jamaa wanasema ni mzungu lakini ni mweusi vladmir putin alwaumbua wazungu,lakini ata Q'RAN TUKUFU inasema 'na tuchukue udongo mweusi ambao ukiganda ukionganga unalialia na tumfanye binadamu,,,,,ata pale kibibosho moshi wazungu walipofika na magobore yao walikuta wenyeji wanamilikiadvance bunduki,wazungu waliwakata mikono hao jamaa,,,ata pale upareni kuna ukoo walikuwa maarufu kwa ufuaji chuma lakini nao walikatwa mikono wengine waliuwawa,at chifu mkwawa,alikuwa na akili nyingi sana lakini walimkata kichwa na kukipeleka ujerumani,pia kuna malikia mmoja likuwa akitawa singinda alipambana na wajerumani balaa!! so kimsingi waafriaka tumefanyiwa brain wash!!!ata leo hii wakufunzi wengi wanaofundisha vyuo ulaya ni waafrika!! so usiwe mnyonge 2po vizuri!!,,,na kwa taarifa yako waafrika ndo wanaopooza hasira ya MUNGU asiangamize dunia
 
Acheni kujidanganya, kwamba Mafarao walikuwa weusi then wakakimbia nchi au waliuliwa!? Mbona leo hawapo wala vizazi vyao havipo? Historia huwa haifutiki.
Kule uarabuni watumwa wengi weusi walikuwepo, leo wako wapi? Mbona Marekani wapo? Historia haifutiki ndio, na ndio maana mabaki ya mapharaoh yaliyokuwa mummified yamefanyiwa vipimo vya DNA na kuonyesha wakikiwa waAfrika, unataka uthibitisho gani zaidi ya DNA?
 
Back
Top Bottom