Hivi waandaaji wa show za wasanii huwa wanapata vipi faida?

Hivi waandaaji wa show za wasanii huwa wanapata vipi faida?

mwekwa ntandu

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2019
Posts
1,526
Reaction score
3,756
Nikiwa naangalia hapa mechi ya USA na Belgium nikakukumbuka Kuhusu matangazo niliyoyaona yamezagaa huko mtaani kuhusu show ya Nandy akiwa na wasanii kibao maarufu tu itakayofanyika katika ukumbi wa the climax uliopo mwanza siku ya jumamosi trh 11/7/2026.

Kwa tathmini ya haraka ukumbi ule ukizidi sana unabeba watu 500 maana ni sehemu ndogo na kiingilio ni tsh 10,000 Kwa kichwa( elfu kumi) hivyo ukipiga hesabu ya haraka pesa ya kiingilio mlangoni ni milioni 5.

Sasa najiuliza msanii mkubwa kama Nandy unamlipa shilingi ngapi Kwa kiingilio hicho? Kumbuka pia Kuna wasanii wengine kibao tu tena maarufu na hapo bado hujaweka gharama za usafiri,hotel,steji,ushuru wa serikali n.k

Sasa wajuzi wa mambo tufahamishane huyu muandaa show anapata vipi faida maana najaribu kuwaza sipati majibu, au Kuna kitu huwa kinafichwa nyuma ya pazia (utakatishaji pesa) au wasanii wana njaa kiasi hicho kiasi kwamba wanapiga show za hela ndogo pamoja na umaarufu wao!! Tufahamishane maana najaribu kutafakari ila naona manyoka nyoka tu.
 
Na Mimi nasubiri waje watueleze vizuri. Mimi nachoshangaa ni kitu kimoja tu na nahitaji ufafanuzi mzuri kutoka kwa wataalamu wa maswala ya burdani.

Ukiangalia wasanii kwenye nchi kama South Africa, Nigeria na mbele huko kama USA ni matajiri sana na wana vipato vizuri na ni ngumu kujua nani msanii njaa na nani matawi.

Kwa bongo gap ni kubwa sana yani wasanii wenye kipato cha kueleweka wanaonekana kabsa wengine njaa kali inaonekana kuanzia usoni ukiachana na majina yao makubwa plus maigizo yao ya mitandaoni.

Swali ni langu ni issues za management ama wanadhulumiwa sana? Msanii kama Nandy anaonekana tajiri sana wakati kuna wasanii kibao wana vipaji kumzidi ila kiuchumi hawako vizuri sana. Au idea za uwekezaji wasanii wetu wengi hawana ama mziki haulipi?
 
Hao wadhamini wako 9,wanacover gharama zote kuazia logistics na Kila kitu.
Kiingilio ni very minor thing na Wala sio target ya owner wa hiyo nandy festival, target ni sponsors
Screenshot_20260707_040700_Instagram.jpg
 
Na Mimi nasubiri waje watueleze vizuri. Mimi nachoshangaa ni kitu kimoja tu na nahitaji ufafanuzi mzuri kutoka kwa wataalamu wa maswala ya burdani. Ukiangalia wasanii kwenye nchi kama South Africa, Nigeria na mbele huko kama USA ni matajiri sana na wana vipato vizuri na ni ngumu kujua nani msanii njaa na nani matawi. Kwa bongo gap ni kubwa sana yani wasanii wenye kipato cha kueleweka wanaonekana kabsa wengine njaa kali inaonekana kuanzia usoni ukiachana na majina yao makubwa plus maigizo yao ya mitandaoni. Swali ni langu ni issues za management ama wanadhulumiwa sana? Msanii kama Nandy anaonekana tajiri sana wakati kuna wasanii kibao wana vipaji kumzidi ila kiuchumi hawako vizuri sana. Au idea za uwekezaji wasanii wetu wengi hawana ama mziki haulipi?
Wenzetu mbele wamewekeza kwenye branding, matangazo vdo yanawalipa sana
 
Nikiwa naangalia hapa mechi ya USA na Belgium nikakukumbuka Kuhusu matangazo niliyoyaona yamezagaa huko mtaani kuhusu show ya Nandy akiwa na wasanii kibao maarufu tu itakayofanyika katika ukumbi wa the climax uliopo mwanza siku ya jumamosi trh 11/7/2026. Kwa tathmini ya haraka ukumbi ule ukizidi sana unabeba watu 500 maana ni sehemu ndogo na kiingilio ni tsh 10,000 Kwa kichwa( elfu kumi) hivyo ukipiga hesabu ya haraka pesa ya kiingilio mlangoni ni milioni 5.Sasa najiuliza msanii mkubwa kama Nandy unamlipa shilingi ngapi Kwa kiingilio hicho!!?? Kumbuka pia Kuna wasanii wengine kibao tu tena maarufu na hapo bado hujaweka gharama za usafiri,hotel,steji,ushuru wa serikali n.k Sasa wajuzi wa mambo tufahamishane huyu muandaa show anapata vipi faida maana najaribu kuwaza sipati majibu,au Kuna kitu huwa kinafichwa nyuma ya pazia (utakatishaji pesa) au wasanii wana njaa kiasi hicho kiasi kwamba wanapiga show za hela ndogo pamoja na umaarufu wao!! Tufahamishane maana najaribu kutafakari ila naona manyoka nyoka tu
Sponsors wameweka Hela yakutosha
Hao 500pax na hicho kiingilio cha 10k kimewekwa tu kuchuja wetu na kukwepa fujo, au kutoshusha brand ya msanii,kama vile band zilivyo shushwa thamani
 
Na Mimi nasubiri waje watueleze vizuri. Mimi nachoshangaa ni kitu kimoja tu na nahitaji ufafanuzi mzuri kutoka kwa wataalamu wa maswala ya burdani. Ukiangalia wasanii kwenye nchi kama South Africa, Nigeria na mbele huko kama USA ni matajiri sana na wana vipato vizuri na ni ngumu kujua nani msanii njaa na nani matawi. Kwa bongo gap ni kubwa sana yani wasanii wenye kipato cha kueleweka wanaonekana kabsa wengine njaa kali inaonekana kuanzia usoni ukiachana na majina yao makubwa plus maigizo yao ya mitandaoni. Swali ni langu ni issues za management ama wanadhulumiwa sana? Msanii kama Nandy anaonekana tajiri sana wakati kuna wasanii kibao wana vipaji kumzidi ila kiuchumi hawako vizuri sana. Au idea za uwekezaji wasanii wetu wengi hawana ama mziki haulipi?
Na hata hao unaowaona wametoboa kimsingi bado sana,sana sana ni kumiliki kigari na nyumba mbili tatu ambazo hata mtu wa kawaida asiye msanii anazo,Sanaa yetu bado sana Kwa wasanii kupata faida
 
Ukumbi unauza vinywaji
Unajitangaza
mmiliki anaweza kutoa hela mfukoni
Inawezekana lakini bado napata shaka,kwamba ugharamie let say mil 50 ya show afu kwenye vinywaji uambulie faida ya mil 4-6.Faida Iko wapi hapo!!??
 
Hao wadhamini wako 9,wanacover gharama zote kuazia logistics na Kila kitu.
Kiingilio ni very minor thing na Wala sio target ya owner wa hiyo nandy festival, target ni sponsors
View attachment 3624042
Wao wadhamini wanapata nini,kutangaza kwa audience ya watu wasiozidi elfu 1 Tena wengi wao pangu pakavu kiingilio chenyewe Cha elfu 10 anadunduliza ndio aje apande precision air🤔🤔,serious au mimi mambo ya biashara yananipiga chenga
 
Yanakupiga chenga kwelikweli.
Publicity anayoipata ni kubwa kuazia social medias,tv, radios nk kwa kuwa embedded kwenye hilo tamasha
 
Wenzetu mbele wamewekeza kwenye branding, matangazo vdo yanawalipa sana
Kwa nchi za wenzetu nakubaliana na wewe Kwa sababu uchumi wa mtu mmoja mmoja ni mkubwa na wanaweza kununua huduma ya sponsor wa show bila shida,ila Kwa huku kwetu mmmmmmmm hiyo ni ngumu kumeza maana wanaoenda kwenye shoo asilimia kubwa ni teenagers na wana vyuo wanaotegemea boom watu wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi wanaoenda kwenye hizo show ni wa kuhesabu ambao ndio hao wanaweza kununua huduma za ma sponsors.Sasa unamtangazia nani pombe ya TZEE NI SISI wakati asilimia kubwa ya audience wanaingia ndani wameshalewa pombe za bei chee za nje ya ukumbi😅🤔
 
Yanakupiga chenga kwelikweli.
Publicity anayoipata ni kubwa kuazia social medias,tv, radios nk kwa kuwa embedded kwenye hilo tamasha
Ok ni sawa anatangaza biashara yake kupitia social media,je, haiwezekani kupata publicity kwenye hizo social medias direct bila show za wasanii maana hapo unakuwa umeongeza gharama kubwa ya kudhamini show wakati ungetumia gharama kidogo kwenye socila medias na Bado ukawafikia watu wengi zaidi
 
Kwa nchi za wenzetu nakubaliana na wewe Kwa sababu uchumi wa mtu mmoja mmoja ni mkubwa na wanaweza kununua huduma ya sponsor wa show bila shida,ila Kwa huku kwetu mmmmmmmm hiyo ni ngumu kumeza maana wanaoenda kwenye shoo asilimia kubwa ni teenagers na wana vyuo wanaotegemea boom watu wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi wanaoenda kwenye hizo show ni wa kuhesabu ambao ndio hao wanaweza kununua huduma za ma sponsors.Sasa unamtangazia nani pombe ya TZEE NI SISI wakati asilimia kubwa ya audience wanaingia ndani wameshalewa pombe za bei chee za nje ya ukumbi😅🤔
Kitendo cha kusikia tu kinatosha
 
Tatizo n ww kutishika na huo usanii wao, gigi money aliwah Kusema alipewa 20k na nay wa mitego ili awe video queen, tena Huyo gigi akiwa na umaarufu wake wa kutosha.

Kuna wasanii hapo hata kuwapa laki wapige show n umewaonea huruma sana

Ndo mana wasanii wengi wakike wameamua kufanya umalaya mana ndo unawalipa vzr kuliko usanii wao, usanii wanautumia kuendelea kujiweka brand ili wapige pesa kwenye umalaya.
 
Back
Top Bottom