Hivi wabunge wa CCM mnajisikiaje, wananchi hawafuatilii Bunge wanafuatilia kesi ya Mbowe?

Hivi wabunge wa CCM mnajisikiaje, wananchi hawafuatilii Bunge wanafuatilia kesi ya Mbowe?

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,325
Reaction score
2,491
Tuelekee moja kwa moja kwenye swali la msingi. Miaka ile bunge lilipokuwa limechangamka ndipo yakaibuliwa maovu ya serikali watu walikuwa wanaahirisha shughuli zao wanafuatilia bunge.

Leo hii sijui bunge halina mvuto, wananchi wanaahirisha shughuli zao wanafuatilia kesi ya akina Mbowe kama tamthiliya.

Hivi wabunge wa CCM mnajisikiaje wananchi hawafuatilii bunge wanafuatilia kesi ya akina Mbowe? Tuseme serikali IPO clear kabisa hakuna madudu ya kuibua wananchi tuyajue?

Zile ahadi za mafiga matatu yaani rais CCM, mbunge CCM, diwani CCM, watendaji wa mitaa CCM, je mbona hatuyaoni Yale mliyoahidi? Majibu tafadhali wabunge wa CCM.
 
Kusema ukweli hapa kitaa watu wanafatilia kesi ya Mbowe Sana, Mambo ya Bunge wafatilie kina Mahela
emoji1.png
 
Leo nikiwa kwenye bar moja hapa Kimara wakati nasubiri kitimoto (roast na ndizi 2) mhudumu mmoja alibadilisha channel na kuweka TBCCM. Nilimuona mzee Halima akiweweseka bungeni hata alichoongea hatukusikia maana members walimuamrisha meneja au azime tiivii kabisa au aondoe tbc haraka sana vinginevyo atabaki peke yake.
 
Back
Top Bottom