Hivi wachezaji wetu wanagundu au wana tatizo na mfumo?

Leodgar chila Tenga, Kabendera, Ally Mayai, Kassim Majaliwa Majaliwa kuwataja wachache huenda muandishi ni generation Z
Kasim Majaliwa alikuwa anachezea timu gani? Na ni mwaka gani mkuu?
 
Inategemea na kiwango alichofikia cha Uchezaji mpira, kwa Ngazi ya Timu ya Taifa huyo Tenga na Ally Mayai, Lakini Hata Dr Ramadhan DAU aliwahi kucheza yanga kids kadhalika Prof Mshindo Msola
Asante sana kwa elimu mkuu. Duh mpaka Ramadhani Dau, kweli wewe unafahamu mengi!
 
Unafahamu kwamba Tunawachezaji ambao ni Graduates kwenye hii ligi kuu ya NBC? Unafahamu kwamba Zawadi Mauya Ana diploma? RELIANT LUSAJO alisoma MUCCobs pia katika nchi hii ya kidemokrasia Elimu si hoja sana unaweza kuipata ukiwa ndani ya uteuzi, katika Demokrasia mshindi ni yule anaekubalika zaidi regardless ni mvuta bangi, shoga, msagaji, muuza mada wa n. K nenda kafanye homework
 
Kwanini usifanye homework? Kabla ya kuandika ulipaswa kufanya kijiutafiti
Mkuu nafikiri unafahamu maana ya kuandika kitu ambacho mtu unakifahamu, na maana ya kuandika kitu ambacho haukifahamu kwahiyo unataka ukifahamu.

So kama umesoma vizuri nilichoandika, basi hauwezi kuwa na sababu ya kuniuliza swali.
 
Unafahamu kwamba Bob nyanga Makani (Rip) aliwahi kucheza mpira hadi chuo kikuu? Ismail Aden Rage yeye humfahamu?
Ya Rage nafahamu kuwa aliwahi kuwa mchezaji wa Simba na baadae akawa mbunge huko Tabora kama sikosei.
Marehemu Bob Makani yeye sikuwahi kuijua historia yake ya mpira, namfahamu zaidi kwa upande wa siasa tu.
 
Ya Rage nafahamu kuwa aliwahi kuwa mchezaji wa Simba na baadae akawa mbunge huko Tabora kama sikosei.
Marehemu Bob Makani yeye sikuwahi kuijua historia yake ya mpira, namfahamu zaidi kwa upande wa siasa tu.
Joel Bendera yeye Alipata kuwa Waziri pia, na Leodger Tenga yeye ana Ukwasi kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wenye Viwanda
 
Hapana nakupinga. Siku hizi elimu inaangaliwa tena sana. Hakuna mvuta bangi atachaguliwa kisa anajuana na mamlaka ya uteuzi. Kina msukuma, Lusinde na Kishimba wangeshaukwaa uwaziri kitambo sana. Hata kama ni mvuta bangi mwenye connection lazima awe na elimu kwa sasa vinginevyo ataishia kuwa chawa tu kama Steve Nyerere. Viongozi na matajiri wakubwa kwa sasa wameshashtuka wanahakikisha watoto wao wanapata elimu bora kabisa kwa gharama yoyote.
 
Kunipinga mimi sio tatizo, tatizo ni kupingana na ukweli wenyewe, kwa sababu unachanganya mambo, mwenzio kataja kuhusu teuzi, wewe ukasema wacheza mpira ni wavuta bangi, mimi nimekueleza kwamba katika demokrasia kigezo si merit ni namna gani jamii inakukubali nikiaamnisha katika Ubunge n. k wewe badala yake unasema unanipinga sijui kwa lipi? Wewe hukuona kuna waziri kabla ya mchengelwa alikuwepo wizara ya michezo ni mtu wa sigara bwege? Au hujui kwamba Taletale, msukuma n.k ni wa bunge na hawana shule
 
Hana elimu huyo Mchengerwa? Kina Taletale, msukuma na wengine wameingia bungeni kwasababu katiba inawalinda... ila kwenye uwaziri hutakaa uwasikie. Hoja yangu ipo kwenye elimu.
 
Hahaha πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Joel Bendera yeye Alipata kuwa Waziri pia, na Leodger Tenga yeye ana Ukwasi kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wenye Viwanda
Asante mkuu kwa darasa. Nimejifunza kile nilichokuwa sikifahamu.
 
Aisee nimecheka sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wasanii ni karatasi inayotumika kuchambia, hivyo muda mwingine huzawadiawa tuvyeo.
Wasikubabaishe hamna kitu, ni watu wanaotumiwa. Msanii huimba na nyimbo kuenea haraka masikioni hata kama hupendi kuwasikiliza, utalazimika hata ktk daladala, bar, mtaani nk hivyo hutumika kuwaimbia viongozi.
Watanzania wengi ni vilaza wasiotaka kufikiri hivyo ukitumia wasanii unawashswishi vilaza kiulaini.
 
Absul Mteketa alikuwa mbunge wa Kilombero
 
Hapa nimekupata vizuri mkurugenzi.
 
Katika ngazi ya ubunge na udiwani, wasanii wanatumia umaarufu wao hasa kwa vijana na wanawake kupata kura pia uwezo wao kifedha unawawezesha kufanya kampeni kubwa. Wachezaji wetu sio maarufu kama wasanii labda Mayele na Chama ambao sio watanzania. Kwa upande wa teuzi, Elimu inawaangusha wachezaji, mfano Nick wa pili, Jokate, Mwana FA wote ni wasomi wa level ya Masters na Nick anakaribia kumaliza PHD, wachezaji wetu wengi ni darasa la saba japo Kuna wachache walio fika Elimu ya Masters kama Tenga na Mtemi Ramadhani na walipata teuzi kwenye mashirika, Profesa Madundo Mtambo nadhani bado ni Mkurugenzi Mkuu TIRDO.
Vile vile ni vigumu kwa mchezaji kupata teuzi akiwa bado mchezaji, mpira ni too demanding, unamuhitaji mchezaji kufanya full time job na club yake angalau miezi 9 kwa mwaka ikiwemo kukaa kambini na kusafiri na timu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…