Hivi wafanyabiashara wenzangu, mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidi kila kitu!

Wewe mpuuzi acha kumwona jirani yako kama mpinzani wako wakati yeye yuko bize kupambania biashara yake. Pia jifunze Marketing. Kama hutajifunza hutafika popote.

Ila kikubwa zaidi punguza tamaa, wivu na roho mbaya. Kwa ulivyojielezea huna muda mrefu kabla hujaenda kwa mganga kuloga.
 
Pamoja na ushauri wote uliopewa usisahau kuwa na chumvi ya mawe katika biashara yako.

Quality
Price
Good customer care .
 
Nondo za humu ni zaidi ya shule najihisi nanufaika kuliko hata mleta mada

Kwenye biashara uvumilivu ndio kila kitu, lakini pia kwa kukushauri mleta uzi usipuuzie wanachokuambia wateja hata kama ni cha kijinga ujue hicho ndio wanakosa kwa huyo jirani yako na wengine wanaokuzunguuka na hichohicho ndio kitafanya umchomoe huyo mteja kwa jirani yako na kuwa wakwako

Mfano unauza mchele halafu mteja akahitaji na mafuta au unga wa pilau na akakwambia "uwe unatuekea na unga wa pilau"(wengi huwa wanasema) basi fanya hima kuuleta na ukishauleta upromote yaani waambie wateja kuwa umeshaleta hata kama hawajakuuliza

Ukiwa na subira ndani ya mwaka au miaka miwili nawewe utakuwa na wateja wako
 
Ni mchele ndiyo. Sasa kwanini unalalamika jirani boda wanajaa kwake na kwako hamna kitu?
Mim nahisi alifungua akiamini atakuwanae level sawa katka hiyo biashara pengine uko nyuma alianzia eneo tofauti akaona vinamchanganya akabadili..........ndo kufikia apo ambapo mwenzetu panamuwanzisha
 
Mambo matatu ktk biashara ni muhimu nanlazima kuyajua na kufanya kwa usahihi

1. Namna ya kununua mzigo
Ubora sokoni,bei rafiki,chaneli ya kupata mzigo kwa usahihi,wadau wa kudili nao nk

2. Namna ya kuuza
Bei yako sokoni,customer care,sera za ofisi na usimamizi wake nk

3. Namna ya kudhibiti pesa

Kila senti ya biashara lazima itumike kwa hesabu sahihi za kihasibu. Sera na usimamizi wa pesa ya biashara ni kitu muhimu sana sbb ndio uhai na ukuaji wa biashara ulipo

Kwa hiyo mkuu hayo mambo tajwa hapo juu huenda ndipo mafanikio ya jirani yako yalipo na ndipo anguko lako lilipo. Kutoka hapo ni ucheki maendeo hayo uboreshe
 
Aiseee umenipa somo kubwa sana shukrani bro🙏🙏
 
Afazari umenijibia huyu
 
Shukrani sana mkubwa
 
Ni sahihi round hii ndo nataka niend mwenyewe moja kwa moja mashineni sabab mwanzon nilikuwa natumia tu madalali
 
Hapo mwanzon nilikuwa siwajui wateja wang ila kwa sas nimejua wateja wang ni watu wa halii ya chini kwaiyo wanapenda mchele kitonga lakini pia uwe mzuriii ko nazanii asaiv nitaenda moja kwa moja mashineni na kuwachukulia mchele wanaohitajii
 
Ushasema mwenzio ana muda mwingi, maana yake ana wateja wengi, iwe hawa wakuja wenyewe, wa kuagizia, wa simu tu..
Jiongeze usihangaike na wateja wake tafuta wa kwako, ingia mitandaoni tangaza biashara yako, mwanzo mgumu mzee.

Halafu fanya utafiti uweze kupata mali nzuri na kwa bei nzuri ili uuze kwa bei poa.
 
Utulivu wa nafasi ni muhimu sana katika biashara, acha kuwa na kijicho au wivu kwa mwenzako uliyemkuta. Miezi mitatu ni michache sana kujitathmini , bado una muda wa kujifunza. Acha kutegemea madalali kwa asilimia 100 jiongeze mwenyewe
Una mawazo ya kibeki tatu, yawezekana hujawahi uza hata nyanya za gengeni.
Hakuna biashara ambayo washindani hawajifanyii evaluation na kujipima kulingana na market na industry. Na hiyo haiitwi wivu wala kijicho.
 
Una mawazo ya kibeki tatu, yawezekana hujawahi uza hata nyanya za gengeni.
Hakuna biashara ambayo washindani hawajifanyii evaluation na kujipima kulingana na market na industry. Na hiyo haiitwi wivu wala kijicho.
Tatizo weng waliomo humu wanaongea vitu wakiwa kwao kwa mama zao ko inshu za biashara wanaona rahisii sana na mtu akiuliza swalii wanaona kama ndo mshamb au ana wivu hiviii. Ila siku akija kuanza biashara yake ndo atajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…