Habari chief,
Nikirejea uzi wako hapo juu inaonesha unahitaji misingi ya game na elimu ya biashara angalau kutoka kwa mfanyabiashara mzoefu awe mentor ili kukupa experiance ya game. Binafsi nitachangia kidogo kulingana na uelewa wangu naamini itasaidiapo haha.
Umeandika kuwa umewahi kufanya biashara kwakuajiriwa kwa mtu lakini kimsingi hapo ulikua muajiriwa si mfanya biashara.
Katika biashara zingatia yafuatayo:
1) Lijue soko lako (wateja) kwa kufanya utafiti kujua walaji wako ni watu wa namna/kipato gani hii itakusadia/kukuanda na aina ya mzigo wakuweka usije ukawa unaleta mchele grade 1 kumbe soko linataka mchele wa kitonga kwa bei yakutupa
2) Mahusiano,
Biashara ni watu tufuta watu wanaofanya biashara kama yako hususani walio karibu/maeneo ya jirani ongea nao itakusaidia kulielewa game la eneo husika na tabia za wateja wake pia zungumza na wateja wako utajifunza kitu na pia mahusiano mazuri yatakusaidia kupata dalali wa kuaminika angalau.
3) Biashara ni imani na inaitaji uwe na muscle kupigania ndoto yako hususani ikiwa kwenye hatua za awali na upepo ukayumba, kikubwa usikate tamaa kama umejiridhisha kwenye point 1, 2 hapo juu.
Imani inaenda mbali zaidi kushirikisha Mungu/Ushirikina utachagua wewe
4) Ubunifu na jitihada
Usisubiri mteja akufuate, weka jitihada kutafuta mteja mpe sababu ya kununua kwako zingatia mteja ni mfalme na ukimpata jitahidi kumtunza kwa kuzingatia matakwa yake na hapa ndio utaelewa kwanini makampuni yanayo jielewa yanatenga bajeti kubwa kwenye upande wa masoko (marketing) na upande wa tafiti (R&D)
Wadau wataongezea mengine,
Mwisho nikupongeze kwa uthubutu na kila lakheri kwenye safari yako ya mapambano.