Vito Corleone
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 2,418
- 5,257
Japo sikuoa (thanks God)bt mm nilimuomba sana tufunge boman japo wote wakristo yaani sipendi zile mbwbwe za harusi kabisa ila mwenzangu alilia kishenzi akisema Bomani ni sawa nakumdharau yeye na ukoo wake.
Ila nkapewa wazo nihamie upande wapili ni simpo kwani ni Shehe,jamvi na ubani,ila wakati najaribu tuhamie kwa Mtume ndio yakatokea yakutokea.
Asante kwa ushauri mkuu, nitalifanyia kaziFinished kwa mwanajumuia yeyote wa jumuia,iliyo mtaani kwako,utapewa utaratibu wa kufanikisha jambo hilo.
Imetokea tu, maisha hayapo straight forwardkwahio miaka sabayote mnazini?ukiristo niukichaa hauna mipaka na maonyo yoyote.
Naam mkuu, mimi ndo nataka ndoa isiyo na mambo mengi..Muoe bint wa watu kumridhisha.
Kama suala ni ndoa isiyo na mambo mengi mbona zipo sana na inawezekana.
Ni life tu, ishatokea wala mi sijapenda niwe mzinzitoa ujinga wako hapa mzinifu wewe.
Usichukulie maisha serious sana bosstoa ujinga wako hapa mzinifu wewe.
Thanks madamAll the Best
Asante sana mkuu, ngoja nitafanyia kazi hili suala liishe ndani ya hii miezi 12 inayokujaHiki ulichoandika kamuonyeshe padri yeyote atakufungisha ndoa mkiwa watu wanne tu (wewe na mkeo, wasimamizi wenu wawili) naye akiwa na watumishi tu.
Au kama atakuwa ametingwa atawafungisha ndoa kwenye zile misa za kila siku asubuhi, mnaingia saa 12:15 mnatoka saa 12:45 asubhi, mnaendelea na ratiba nyingine.
Asante mkuu ngoja nitafuatilia hiliSiku hizi kuna ndoa wanaziita za msamaha, hizi ni za chap chap, mwaka jana kuna parokia ilifungisha 26.
Powa mkuu, napokea ushauri wako ili niufanyie kaziZipo nenda kwa kiongozi wako wa jumuia,zinafanyikaga kila mwaka na ukitaka ile ya peke yako isio na mambo mengi katikati ya week, nenda kanisani jiandikishe hudhuria mafundisho ya ndoa ,andikisha ndoa yako ya misa zile za asubuhi, nusu saa tayari ushaoa na kuondoka na mkeo.
Sio sijaamua mkuu, ni maisha tu... kwanza kilichonipa setback, kikao cha mahari kilivunjikaga, ni story nyingine hiyo... ndo ikanipoteza munkari kabisa...[emoji28]kasheshe hutaki mambo mengi kabisa, We si mwanaume na ndoa huwa IPO upande WA mwanaume na sanasana mwanaume anasema anataka ndoa yake iwaje mbn unaweza kufunga ya kanisani na ikawa kama unavyotaka, ww hujaamua Tu.
Yaani kakaa na mkewe miaka 8 na wana watoto 2 bado anaitwa mke mtarajiwa?jitahidi kumpa mke wako mtarajiwa ndoa ya namna hiyo
Mkuu, hapa unabariki ndoa sio kufunga ndoa.Ninachokifikiria kichwani ni kufunga ndoa isiyokuwa na kelele
Basi ita watu wachache tu, nenda kanisani, timiza adhma ya binti, muheshimishe kama ambavyk anatamani, atleast mfamyie jambo ambalo kwake ni la thamaniNaam mkuu, mimi ndo nataka ndoa isiyo na mambo mengi..
Kabisa mkuu mwakani maliza kabisa.Asante sana mkuu, ngoja nitafanyia kazi hili suala liishe ndani ya hii miezi 12 inayokuja
Zipo mkuu. Nenda tu jumuiya then wambie wakufanyie mchakato. Unaweza funga hata wakati wa ibada ya usiku mwaka mpya au Christmass ukienda home kulala na asubuhi ikawa kama hamna kilichotokeaUkweli huyu ninayemuita mke wangu, hatuna ndoa kamili ya kanisani, pamoja na kuishi miaka 8 na kubahatika watoto wawili (Miaka 7 na miaka 3).
Sasa msukumo wa ndoa umekuwa mkubwa sana kutoka pande zote, na yeye mwenzangu naona hii kukosa ndoa inampa sononeko maana wazazi wake wanaogopa nisije nikamuacha (japo hii sababu sioni kama ina mashiko, kwasababu hata ukiwa na ndoa unaachika tu).
Ukweli mwingine ni kwamba, sababu haswa ya kutokufunga ndoa mpaka sasa, ambayo naijua mwenyewe ni kwamba, mi sio mtu wa shereha kabisaaaa.
Yaani kila nikikaa chini nikajifikiria kwamba nipo sijui navalisha pete ya uchumba, sijui nipo natoa mahari, sijui nipo mbele ya kadamnasi ya kanisa na padri pale mbele, sijui nipo kwenye ukumbi watu kibao. Yaani sijioni kama naweza lolote hapo na sipendi hayo mambo.
Ninachokifikiria kichwani ni kufunga ndoa isiyokuwa na kelele, nilitaka kufunga ya serikali, naona mwenzangu akagoma, anataka ya kanisani.
Sasa hapa wazo limenijia nakumbuka kuna zile ndoa zamani zilikuwa zinafanyika mkesha wa mwaka mpya au krismasi kama sijasahau, maana ni kipindi nipo mdogo, enzi hizo nahudhurua kanisani. Unakuta kuna ndoa kama sita hivi za haraka haraka. Hiyo ndo naona inanifaa kwa sasa.
Embu kwa wakatoliki wenzangu naombeni utaratibu wa ndoa hii ya fasta fasta isiyohitaji kelele. Ila ubaya mwingine ni kwamba mimi pia sio mtu wa kwenda jumuiya... yaaaaniiiii
Asanteni, naombeni ushauri ili nimalize hili jambo