Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nimewakumbuka Sana! Hivi wako wapi? Mko wapi? Tafadhali naombeni mnijibu!
Taikon nitawarudisha na kuwapeleka mpaka kijiji cha Makanya huko nilikozaliwa, pengine labda Waislam hao ndipo walipokuwa wanapatikana lakini hapana, nilibahatika kuwaona wakati Fulani nilipoenda Morogoro miaka ya 2006 Kurudi nyuma.
Hii ni kusema Waislam hawa walikuwa wapo nchi nzima. Sasa iweje wapotee wote na tusijue waliko?
Miaka hiyo ni mtoto mdogo kabisa, nikiwa na watoto wenzangu, nilishuhudia misafara yenye kundi kubwa la watu waliovalia kanzu za namna na rangi tofautitofauti, kichwani wakiwa wamevalia Barakashia na malemba yenye kuvutia haswa. Mavazi hayo yaliwatambulisha Kama Waislam.
Mikononi mwao walikuwa wamebeba Ngoma Kwa Baadhi Yao, huku wengine wakiwa wamebeba Milingoti mifupi na mirefu yenye bendera za namna kadhaa; zilizoandikwa maandishi ya kiarabu. Kwa kipindi kile sikuweza kujua zinamaandishi yanayomaanisha nini.
Ngoma zilipigwa na nyimbo zikaimbwa huku msafara huo ukikatiza mtaa Kwa mtaa, barabara Kwa barabara. Huku waislam hao wakicheza Kwa furaha ungedhani wameishinda Dunia.
Hisia zilizokuwa zinakuja kichwani mwangu Taikon ambaye nilikuwa nikiufuata msafara huo aidha Kwa kuvutiwa au kushangaa, nilifikiri Dunia ndio ilikuwa inafika mwisho wake. Waliimba Kwa msisimko, walionyesha hamasa.
Ngoja nijaribu kuimba kadiri ya nilivyoyasikia maneno ya moja ya wimbo zile, ingawaje naweza nisipatie sana!; Hivyo mtanisamehe na wenye kujua mtaweka marekebisho;
"Allah maulana! Allah maulana Saidina Huayallah. Huayallah! Huayallah (mtume) Huayallah! (Karima) Huayallah!"
"Mtume Yallah! Yallah!. Karma Yallah! Yallah×2"
Basi wakawa wanapita huku na huko wakisherekea.
Ilikuwa ni ngumu sikukuu ya Maulidi au ya Idi kupita bila ya misafara hii mirefu yenye watu wengi mno wakizunguka majira ya Jioni kabisa baada ya Kula na kunywa na kufurahia chakula.
Hiyo ndio namna nilivyozitambua sikukuu za kiislam nyakati zile nikiwa ndio naanza kupata Uelewa wa Dunia.
Sasa Taikon najiuliza, mambo Yale mbona yalipotea?
Waislam wale walitoweka na kuyeyuka Kama Moshi?
Au je Baadhi ya Maeneo bado desturi hii inaendelea?
Kwa kweli napenda kuwashauri Waislam wote wa Zama hizi.
Ile Desturi ni nzuri mno. Ingawaje Mimi sio Muislam lakini desturi Ile ya kuzunguka mitaani na misafara yenye Ngoma, bendera mkicheza Kwa furaha kufurahia sikukuu zenu ni moja ya mambo yaliyowafanya Spesho katika usheherekeaji wa sikukuu tofauti na dini zingine.
Watoto waliovalishwa vizuri, Wamama waliojitanda, Wababa na Wazee waliovaa vizuri kanzu zao mpya na Kama sio mpya basi Safi walishiriki katika misafara hii. Iweje leo badala ya Waislam kufurahia Kwa namna hiyo wanaishia kwenda kwenye Matamasha ya muziki ya kidunia, Bora lingekuwa tamasha la Dini.
Wako wapi waislam wale? Uko wapi uislam ule?
Wao wapi waislam wale ambao Sisi Wakristo wa Enzi hizo tukiwa watoto tulikuwa tunashirikiana nao kuutafuta Mwezi! Hivi unakumbuka?
Makundi Kwa makundi ya watu Majira ya Jioni jua likiwa limezama yalisimama kutazama angani upande wa Magharibi kuutafuta mwezi.
Ilikuwa ni sifa na Jambo la kujivunia kuwa WA Kwanza kuuona mwezi mwandamo wa mfungo wa Ramadhan.
Sio watoto, sio wamama wala wazee, kila mmoja alihangaika kuutazama mwezi mchanga.
Na Kama kundi Lenu lingechelewa kuuona mwezi basi Kwa mbali ungesikia sauti kutoka mtaa wa pili au mbali kidogo zikiimba;
" Mwezi! Mwezi! Mwezi×"
Hali hiyo ingekufanya uzidishe kukaza macho kuuona mwezi.
Ilikuwa bahati mbaya Sana Kama macho yako yalishindwa kuuona mwezi mpaka ulipozama kwani haukaagi angani muda mrefu.
Wapo wapi wale Waislam?
Maana hawa wa sasa nahisi Kama sio. Hawa wanasubiri watangaziwe redio, luningani na mitandao ya kijamii.
Hawajishughulishi.
Wanataka wengine wawaonee huo mwezi. Loooh!
Sisemi kuwasema vibaya, Ila nazungumzia utamu na zile Raha za uislamu wa kipindi kile ambao ulileta shamrashamra na kutufanya mpaka Sisi tusiowaislam kuufurahi uislam.
Mimi sitaki kueleza mambo ya kuletewa Tende, Kualikwa Kula Futari msije sema Taikon anapenda Kula, lakini hata mkisema ni Sawa kwani Kupenda Kula ni kosa! ama Kwa hakika uislam wa kipindi kile ulikuwa ni Neema kubwa katika jamii zetu.
Labda maisha yamebadilika kutokana utandawazi lakini haiondoi ukweli kuwa uislam wa sasa umezidiwa na uislam wa Enzi ninakua.
Labda kilichobaki ni Adhana ya kukumbushana Sala!
Au je Waislam wasasa wanaona aibu kuwa Waislam?
Mungu awabariki waislam wote wa Zama hizo walioufurahisha moyo wangu, waliojitahidi kuutangaza uislam kwa namna njema.
Walioleta neema ndani ya jamii.
Pia awabariki wanaoendelea kufurukuta katika Zama hizi mbaya za utandawazi.
Kwa kweli Zama hizi ukiona Muislam anayejitahidi kufuata miiko na Mila za kiislam mpe hongera hata Kama sio dini yako.
Wako wapi wale Waislam wa Zama zile?
Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kibiti, Pwani.