Hivi wale Waislam wa kipindi kile walipotelea wapi?

Hivi wale Waislam wa kipindi kile walipotelea wapi?

Mkuu umenikumbusha mbali Sana!!nilikua naamka na jamaa zangu FULANI wa madrasa usiku kuamsha watu kula daku tukipiga madufu yale!!!ilikuwa raha Sana AISEH!!

Ati Waislam wa siku hizi ndio wenye Ilmu kuliko wa zamani.

Hapa ndio nashangaa
 
TAIKON, sunnah na Qur'an ndiyo mwisho wa yote, mengine ni ongezeko la Ubunifi wa viumbe wa leo. Karibu katika dini ya amani na ustaarabu.

Nashukuru Sana Kwa dini ya Amani na ustaarabu.

Lakini kwangu Dini nazichukulia Kama vyuo tuu vyakujifunzia elimu za kiroho.

Siwezi kuwa na dini moja.
Nasoma zote Kwa maana hakuna dini iliyokamilika mpaka sasa nilizozisoma.
 
Unaelewa kwanza dini ni nini? Ukristo siyo dini.
 
Hiyo mashindano ya kusoma Quran imeandikwa kwenye Quran?

Muziki sio haramu, Ila Inategemea na ain ya Muziki unaotumika.
Ndio maana kuna Kawaida, au hujui kaswida pia ni nyimbo/muziki?

Hakuna sherehe pasipo Nyimbo, muziki, vinywaji na chakula. Hakunaga sherehe ya hivyo.

Kuhusu chakula Hilo lipo wazi, Waislam sheria zinawaongoza vyakula vya kutumia.
Sikukuu si wanapika Pilau, wali, nyama, nqvyakula vingine vinavyoruhusiwa.

Hiyo kucheza michezo yenye Afya imeandikwa kwenye Quran, nani michezo gani hiyo?

Kumbuka kwenye dini yoyote Ile kuna mambo yaliyoagizwa na Mungu ambayo ndio yamsingi lakini pia kuna mambo ya kibinadamu.
Kaka unapoteza muda wako bure kubishana na hao "pingapinga"..

Hao wanaitwa ni Mawahabi..

Msingi mkuu na mafundisho ya Mawahabi ni Kujilipua, Kuchinja wasiokuwa waislamu, Chuki baina ya waumini na kuleta mifarakano kwenye dini ..

Yale makundi ya kigaidi yote duniani (mfano Boko Haram, Al Shabaab, Isil, Al Qaeda etc)ni imani ya kiwahabi..
 
😊😊😊
 
Tulia bwana Taikon uislamu hauendeshwi kibubusa na Rai za ajabu ajabu ...Muislam safi Ni Yule anaefuata Quran na Sunnah ,,,kataa wahuni na Wazushi ktk dini...
Wewe jamaa kama umemaind hivi
 
"¶¶ Twamshukuru salimu waziri wetu mkuu, kufungua mipaka wake zetu wananga'aa, aliekuwa jaluo amekua muarabu eeee, tiktiktuktuk ¶¶
 
Kaka unapoteza muda wako bure kubishana na hao "pingapinga"..

Hao wanaitwa ni Mawahabi..

Msingi mkuu na mafundisho ya Mawahabi ni Kujilipua, Kuchinja wasiokuwa waislamu, Chuki baina ya waumini na kuleta mifarakano kwenye dini ..

Yale makundi ya kigaidi yote duniani (mfano Boko Haram, Al Shabaab, Isil, Al Qaeda etc)ni imani ya kiwahabi..
Usiwe Muislamu mjinga ww
Ponda alopigisha watu ni wahabi?(nijibu hili swali)
hlf nitajie sheikh mmoja tu hao mnosema wa kiwahabi alojiripua

Watu wengi haki wanaichukia wanapenda kufata matamanio yao bali hawataki kufuata Qur'an na sunnah za mtume
 
Hiyo mashindano ya kusoma Quran imeandikwa kwenye Quran?

Muziki sio haramu, Ila Inategemea na ain ya Muziki unaotumika.
Ndio maana kuna Kawaida, au hujui kaswida pia ni nyimbo/muziki?

Hakuna sherehe pasipo Nyimbo, muziki, vinywaji na chakula. Hakunaga sherehe ya hivyo.

Kuhusu chakula Hilo lipo wazi, Waislam sheria zinawaongoza vyakula vya kutumia.
Sikukuu si wanapika Pilau, wali, nyama, nqvyakula vingine vinavyoruhusiwa.

Hiyo kucheza michezo yenye Afya imeandikwa kwenye Quran, nani michezo gani hiyo?

Kumbuka kwenye dini yoyote Ile kuna mambo yaliyoagizwa na Mungu ambayo ndio yamsingi lakini pia kuna mambo ya kibinadamu.
Mkuu Imani ya kiislamu ipo tofauti na kikristo kwetu sisi nyimbo ni haramu hata aimbe nani yule. kwnye Uislamu kilichoruhusiwa ni mashairi tu bila ya Ala za muziki

Mashindano ya Qur'an ni bidaa(uzushi) kawaulize hao wanofanya ivo watoto wao wangapi wamehusudiwa baada ya kushinda hyo mashindano? Na wao wameyapata.wapi mna hakuna Aya wala hadith inotufundisha tufanye mashindano ya Qur'an
 
Sipo hapa kubishana.

Kwa hiyo Elimu ya sasa iliyowafikia Waislam wengi na zamani, wapi waislam wenye unafuu?

Kwa muono wangu Waislam wa zamani wamewaacha mbali Sana Waislam wa sasa. Mbali sana
Kwel kabisa mkuu tena wamewaacha mbali sana,kwaiyo saiz wasanii wanavyo futulisha watu namacamera kwaiyo huo ndio uislam?
 
Na wapi wanakataza kusherekea sikukuu za kiislam Kwa ALA za Muziki na nyimbo??
Swali zuri kwanza inatakiwa ujue kuwa waislam wote duniani hakuna anaweza kupinga juu ya uharam wa muziki maana imekatazwa katika sehem nyingi sana

Mfano kwenye quran suratul Al anfaal aya ya 35

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ ٱلْبَيْتِ إِلَّا مُكَآءًۭ وَتَصْدِيَةًۭ ۚ فَذُوقُواْ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٥﴾

Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba ila ni kupiga mziki na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
 
Usiwe Muislamu mjinga ww
Ponda alopigisha watu ni wahabi?(nijibu hili swali)
hlf nitajie sheikh mmoja tu hao mnosema wa kiwahabi alojiripua

Watu wengi haki wanaichukia wanapenda kufata matamanio yao bali hawataki kufuata Qur'an na sunnah za mtume

Nitajie kundi moja la kigaidi hapa duniani ambalo halina imani ya Kiwahabi?
 
Abdullah ibn Masoud alikua ni Swahaba wa mtume kutoka kabila la Hudhayl alianza kuzisikia habari za mtume akiwa mtoto huko milimami akiwa anachunga mbuzi (watu walikua wanamuita mtoto wa kijakazi)
mtoto huyo ambae badae alikuja kuwa Swahaba wa mtume alikua ni mtaalam wa kusoma Quran

sasa Kama hata maswahaba wa mtume huwajui na unawapuuza ni kipi unacho kijua katika uislam? au kupinga kwa hisia?
Hadithi ni uthibitisho kwamba Qur'an haitoshi,hadithi ziliibuka miaka 150 baada ya mtume saw kufariki,hadithi zinawagawa waislam kwa misingi ya madh'hab,kila mtu akiwa na wapokezi wake,hadithi miundo wake tu unajua no hekaya
 
Kwema Wakuu!

Nimewakumbuka Sana! Hivi wako wapi? Mko wapi? Tafadhali naombeni mnijibu!

Taikon nitawarudisha na kuwapeleka mpaka kijiji cha Makanya huko nilikozaliwa, pengine labda Waislam hao ndipo walipokuwa wanapatikana lakini hapana, nilibahatika kuwaona wakati Fulani nilipoenda Morogoro miaka ya 2006 Kurudi nyuma.

Hii ni kusema Waislam hawa walikuwa wapo nchi nzima. Sasa iweje wapotee wote na tusijue waliko?

Miaka hiyo ni mtoto mdogo kabisa, nikiwa na watoto wenzangu, nilishuhudia misafara yenye kundi kubwa la watu waliovalia kanzu za namna na rangi tofautitofauti, kichwani wakiwa wamevalia Barakashia na malemba yenye kuvutia haswa. Mavazi hayo yaliwatambulisha Kama Waislam.

Mikononi mwao walikuwa wamebeba Ngoma Kwa Baadhi Yao, huku wengine wakiwa wamebeba Milingoti mifupi na mirefu yenye bendera za namna kadhaa; zilizoandikwa maandishi ya kiarabu. Kwa kipindi kile sikuweza kujua zinamaandishi yanayomaanisha nini.

Ngoma zilipigwa na nyimbo zikaimbwa huku msafara huo ukikatiza mtaa Kwa mtaa, barabara Kwa barabara. Huku waislam hao wakicheza Kwa furaha ungedhani wameishinda Dunia.

Hisia zilizokuwa zinakuja kichwani mwangu Taikon ambaye nilikuwa nikiufuata msafara huo aidha Kwa kuvutiwa au kushangaa, nilifikiri Dunia ndio ilikuwa inafika mwisho wake. Waliimba Kwa msisimko, walionyesha hamasa.

Ngoja nijaribu kuimba kadiri ya nilivyoyasikia maneno ya moja ya wimbo zile, ingawaje naweza nisipatie sana!; Hivyo mtanisamehe na wenye kujua mtaweka marekebisho;

"Allah maulana! Allah maulana Saidina Huayallah. Huayallah! Huayallah (mtume) Huayallah! (Karima) Huayallah!"

"Mtume Yallah! Yallah!. Karma Yallah! Yallah×2"

Basi wakawa wanapita huku na huko wakisherekea.

Ilikuwa ni ngumu sikukuu ya Maulidi au ya Idi kupita bila ya misafara hii mirefu yenye watu wengi mno wakizunguka majira ya Jioni kabisa baada ya Kula na kunywa na kufurahia chakula.

Hiyo ndio namna nilivyozitambua sikukuu za kiislam nyakati zile nikiwa ndio naanza kupata Uelewa wa Dunia.

Sasa Taikon najiuliza, mambo Yale mbona yalipotea?

Waislam wale walitoweka na kuyeyuka Kama Moshi?

Au je Baadhi ya Maeneo bado desturi hii inaendelea?

Kwa kweli napenda kuwashauri Waislam wote wa Zama hizi.

Ile Desturi ni nzuri mno. Ingawaje Mimi sio Muislam lakini desturi Ile ya kuzunguka mitaani na misafara yenye Ngoma, bendera mkicheza Kwa furaha kufurahia sikukuu zenu ni moja ya mambo yaliyowafanya Spesho katika usheherekeaji wa sikukuu tofauti na dini zingine.

Watoto waliovalishwa vizuri, Wamama waliojitanda, Wababa na Wazee waliovaa vizuri kanzu zao mpya na Kama sio mpya basi Safi walishiriki katika misafara hii. Iweje leo badala ya Waislam kufurahia Kwa namna hiyo wanaishia kwenda kwenye Matamasha ya muziki ya kidunia, Bora lingekuwa tamasha la Dini.

Wako wapi waislam wale? Uko wapi uislam ule?

Wao wapi waislam wale ambao Sisi Wakristo wa Enzi hizo tukiwa watoto tulikuwa tunashirikiana nao kuutafuta Mwezi! Hivi unakumbuka?

Makundi Kwa makundi ya watu Majira ya Jioni jua likiwa limezama yalisimama kutazama angani upande wa Magharibi kuutafuta mwezi.

Ilikuwa ni sifa na Jambo la kujivunia kuwa WA Kwanza kuuona mwezi mwandamo wa mfungo wa Ramadhan.

Sio watoto, sio wamama wala wazee, kila mmoja alihangaika kuutazama mwezi mchanga.

Na Kama kundi Lenu lingechelewa kuuona mwezi basi Kwa mbali ungesikia sauti kutoka mtaa wa pili au mbali kidogo zikiimba;
" Mwezi! Mwezi! Mwezi×"

Hali hiyo ingekufanya uzidishe kukaza macho kuuona mwezi.
Ilikuwa bahati mbaya Sana Kama macho yako yalishindwa kuuona mwezi mpaka ulipozama kwani haukaagi angani muda mrefu.

Wapo wapi wale Waislam?

Maana hawa wa sasa nahisi Kama sio. Hawa wanasubiri watangaziwe redio, luningani na mitandao ya kijamii.
Hawajishughulishi.

Wanataka wengine wawaonee huo mwezi. Loooh!

Sisemi kuwasema vibaya, Ila nazungumzia utamu na zile Raha za uislamu wa kipindi kile ambao ulileta shamrashamra na kutufanya mpaka Sisi tusiowaislam kuufurahi uislam.

Mimi sitaki kueleza mambo ya kuletewa Tende, Kualikwa Kula Futari msije sema Taikon anapenda Kula, lakini hata mkisema ni Sawa kwani Kupenda Kula ni kosa! ama Kwa hakika uislam wa kipindi kile ulikuwa ni Neema kubwa katika jamii zetu.

Labda maisha yamebadilika kutokana utandawazi lakini haiondoi ukweli kuwa uislam wa sasa umezidiwa na uislam wa Enzi ninakua.

Labda kilichobaki ni Adhana ya kukumbushana Sala!

Au je Waislam wasasa wanaona aibu kuwa Waislam?

Mungu awabariki waislam wote wa Zama hizo walioufurahisha moyo wangu, waliojitahidi kuutangaza uislam kwa namna njema.
Walioleta neema ndani ya jamii.

Pia awabariki wanaoendelea kufurukuta katika Zama hizi mbaya za utandawazi.
Kwa kweli Zama hizi ukiona Muislam anayejitahidi kufuata miiko na Mila za kiislam mpe hongera hata Kama sio dini yako.

Wako wapi wale Waislam wa Zama zile?

Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kibiti, Pwani.

tuliisha wape elimu tosha kutoka kwa waislamu wanaojielewa salafi. kuwa haitakiwi kubeba mabendera na maandamano katika uislamu hii hakuna naona wameelewa. bado sisi waislam salafi tunazidi kuwapa elimu waislamu bakwata waache kupiga madufu hiyo sio dini na kusoma maulidi hiyo sio dini waache. na nyinyi TV zote msifikiri kutuletea watoto wa madrasa wanaimba nakupiga dufu huku wakicheza kwenye ma tv mkafikiri kwa waislamu ni ibada hapana sio ibada ni kumkufuru mungu sisi hatuna hiyo hao ni waislamu wa madhehebu ya bakwata
 
Swali zuri kwanza inatakiwa ujue kuwa waislam wote duniani hakuna anaweza kupinga juu ya uharam wa muziki maana imekatazwa katika sehem nyingi sana

Mfano kwenye quran suratul Al anfaal aya ya 35

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ ٱلْبَيْتِ إِلَّا مُكَآءًۭ وَتَصْدِيَةًۭ ۚ فَذُوقُواْ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٥﴾

Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba ila ni kupiga mziki na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
Una uhakika hiyo Aya imetaja muziki!?...au unatafsiri kukidhi itikadi zako
 
Sunnah ni mambo ambayo ukifanya unalipwa thawabu na usipo fanya hupati dhambi

Quran siyo Sunnah mzee acha kabisa kuandika upuuzi
Sunnah ni mwenendo,kwa muktadha wa dini ni aliyotenda mtume ambayo hayamo kwenye Qur'an,wenyewe wahabi(answar Sunnah) ukiwaambia Sunnah ni ukifanya unapata thawabu ukiacha hipati dhambi mtagombana,sababu kuvaa dontach kwao ni Sunnah na kutovaa ni ukafiri
 
Mzee aliyestaarabika anaweza kuoa kabinti ka miaka 9?

ndio unaoa hata wa miaka 5 uliza watemi waliokuwa wanatawala tanzania zamani walikuwa wanaoa watoto wadogo sana. na ukumbuke zamani kulikuwa hakuna dawati la kijinsia hizi sheria za kufika miaka 18 zimetungwa majuzi juzi na wazungu ila kabla ya hapo watu walikuwa wanaoa watoto wadogo sana wanaishi nao
 
Back
Top Bottom