FATHER OF HISTORY
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 915
- 638
Umeongea hoja nzuri mkuu,lengo la mtoa mada ni kudai kile anachostahili.Katumia jukwaa hili pengine angepata faraja.Lakini kumekuwa na shambulio badala yake.Maswala ya uchaguzi sidhani vinauhusiano sana na hoja ya mtoa mada.Labda ninachoweza kusema sijajua mbinu au taratibu zao za kudai madai ya Jambo la aina hii.Lakini anahaki yake kudai malipo ya kile alichokifanyia kazi.Jamani, nafikiri lengo la mleta mada hii kwa wana jamii ni kupata mawazo na hata faraja kama mwana jamii. Nimesoma komenti nyingi zinakosa japo neno la faraja. Tukumbuke kuwa ualimu ni kazi ya heshima. Popote ukimtaja mtaalamu wa aina yeyote ni sharti awe amefundishwa na mwalimu. Ni vema ikiwa tutawaheshimu waalimu na kusikitika nao pale haki zao zinapokosekana. Niwape pole waalimu kwa kukosa stahiki zao kwa wakati. Niwatie moyo kwamba msikate tamaa. Fuatilieni madai yenu kwa utaratibu uliopo kwani serikali ni sikivu wakati wote. Ukiona usiku umeendelea jua mchana nao pia waja.
Maswala ya uchaguzi hakuna mwenyewe ushahidi wa moja kwa moja na hayo yanayosemwa. Nashauri mpeni tu utaratibu jinsi gani atapata haki yake siyo kumshambulia na kumkejeli.
Ila kama walivyosema baadhi ya wajumbe kwamba NECTA ni chombo chenye heshima na chenye weledi wa Hali ya juu.Hakiwezi wadhurumu walimu wake,itakuwa kuna taratibu tu walikuwa wanazikamilisha na hatimae watalipa.
Naamini kabisa haitapita kesho watu hawa watakuwa wamesharejeshewa furaha yao iliyopotea.
Ukweli kutoka moyoni ninawaheshimu sana pia ninawependa walimu.Naombeni walimu vuteni subiri Dkt.Msonde atawalipa pesa yenu