Hivi Walimu wa nchi hii tumemkosea nini Magufuli hata atutende hivi?

Hivi Walimu wa nchi hii tumemkosea nini Magufuli hata atutende hivi?

Walimu wengi mshukuru kuwa katika ajira,mfumo wa ovyo wa miaka mingi kuwaajiri waliofanya vibaya olevel na STD 7 yaani walimu wa upe.kazi yenu kubwa ni kuwapa majibu ya mitihani watoto.mishahara yenu kulingana na jitihada zenu mlipokuwa shuleni mnasoma na hata kwa elimu mnayotoa kwa watoto kwenye shule za serikali ni zaidi mlichostahili.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hoja yako ni ipi?Tulia uandike vizuri,hoja ieleweke.
Walimu wengi mshukuru kuwa katika ajira,mfumo wa ovyo wa miaka mingi kuwaajiri waliofanya vibaya olevel na STD 7 yaani walimu wa upe.kazi yenu kubwa ni kuwapa majibu ya mitihani watoto.mishahara yenu kulingana na jitihada zenu mlipokuwa shuleni mnasoma na hata kwa elimu mnayotoa kwa watoto kwenye shule za serikali ni zaidi mlichostahili.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mishahara yetu duni... Tumekubali

Posho ya mazingira magumu hamna.. Tumekubali

Madaraja hatupandi.. Tumekubali

Annual increment hamna.. Tumekubali.

Pay leave..likizo ya malipo hamna... Tumekubali.

LAKINI

Hata hili la kazi maalumu, kweli kabisa hutulipi. Yani mitihani imesahishwa,tumerudi nyumbani.. Mpaka leo? Kweli!?

Hivi Ualimu ni laana?
Hivi mkuu huwa mnapelekaga malalamiko yenu wizara ya elimu, na kama mnawapelekea majibu huwa yanakuaje, maana sasa imekua ni mzizi wa matatizo ulio komaaa
 
Mitihani kuibiwa haimaanishi kuwa NECTA siyo chombo Cha heshima.Kwani kwako ukiibiwa na majambazi,Basi unakuwa huna heshima?
An OATH ought not to be INFRINGED... and if that happens.. Of the two sides.. The lamenter of whom she/he feels not well treated as per the OATH...
HAS THE RIGHT TO QUESTION OF THAT INFRINGEMENT WHEREVER POSSIBLE.

It what this thread is all about...
 
An OATH ought not to be INFRINGED... and if that happens.. Of the two sides.. The lamenter of whom she/he feels not well treated as per the OATH...
HAS THE TO QUESTION OF THAT INFRINGEMENT WHEREVER POSSIBLE.

It what this thread is all about...
Unclear,Re-write.
 
Hivi mkuu huwa mnapelekaga malalamiko yenu wizara ya elimu, na kama mnawapelekea majibu huwa yanakuaje, maana sasa imekua ni mzizi wa matatizo ulio komaaa
Mkuu ukipeleka unakuwa noted...
Ukifika kituoni inafuata barua.. Ka ulikuwa kijijini panapofikiaka...sasa unatupwa chakaa ambako hata network hamna...
This field!!!!!??
 
Baba yetu ni msikivu.Naimani kabisa yeye hili halijui.Kama kweli halijui naamini kupitia hapa atajua.Naakijua naamini siku ya Leo haitapita kilio chenu atajibu.

Naamini kabisa kazi hii ni ya siri na heshima yake.Malalamiko kama haya hakika hayapaswi yaonekane hapa kutokana na unyeti wa Jambo lenyewe.Baraza la Mitihani ni chombo cha Heshima sana,naamini watashughulikia kilio cha watu wao hawa mapema.

Baba naomba wasikilize vijana wako.
Asante
Sema baba yako wewe.....huyu kwangu ni Rais....
Ila mengine umeandika point....hili suala ni sensitive sana
 
Baba yetu ni msikivu.Naimani kabisa yeye hili halijui.Kama kweli halijui naamini kupitia hapa atajua.Naakijua naamini siku ya Leo haitapita kilio chenu atajibu.

Naamini kabisa kazi hii ni ya siri na heshima yake.Malalamiko kama haya hakika hayapaswi yaonekane hapa kutokana na unyeti wa Jambo lenyewe.Baraza la Mitihani ni chombo cha Heshima sana,naamini watashughulikia kilio cha watu wao hawa mapema.

Baba naomba wasikilize vijana wako.
Asante
Umesema kweli mkuu.
Mimi pia Nina imani na Baraza. Nadhani Kuna Jambo wanalishughulikia na likiwa sawa watawalipa tu.

Sent from my X90 using JamiiForums mobile app
 
ualimu ni wito alafu mbona alikua anawalipa mishahara kipindi cha corona so inabidi mchapike kisawasawa au nasema uongo ndugu zanguuuu
 
Mishahara yetu duni... Tumekubali

Posho ya mazingira magumu hamna.. Tumekubali

Madaraja hatupandi.. Tumekubali

Annual increment hamna.. Tumekubali.

Pay leave..likizo ya malipo hamna... Tumekubali.

LAKINI

Hata hili la kazi maalumu, kweli kabisa hutulipi. Yani mitihani imesahishwa,tumerudi nyumbani.. Mpaka leo? Kweli!?

Hivi Ualimu ni laana?

Bora hata wewe wamekuajiri unapata mshahara....wengine bado tupo na vyeti vyetu mtaani kitakachofata ngoja tuka apply hata freemason kama watatukubalia maana njaa imekuwa kali mno
 
Mishahara yetu duni... Tumekubali

Posho ya mazingira magumu hamna.. Tumekubali

Madaraja hatupandi.. Tumekubali

Annual increment hamna.. Tumekubali.

Pay leave..likizo ya malipo hamna... Tumekubali.

LAKINI

Hata hili la kazi maalumu, kweli kabisa hutulipi. Yani mitihani imesahishwa,tumerudi nyumbani.. Mpaka leo? Kweli!?

Hivi Ualimu ni laana?
Acheni kulialia ninyi walimu mnakera sana basi kajifungieni makwenu mlieeee msituletee unyonge wenu humu kilasiku!! Hivi hamna chama? Simuandamane mpaka ofisi za CWT(chama cha wadekao tz) kaposho kenu mtapewa,kwanza kusahihisha niwajibu wenu hata msipolipwa!! pesa ya serikali hutolewa kiutaratibu njaa inawapigaa na uchaguzi mlisimamia why??
 
Mishahara yetu duni... Tumekubali

Posho ya mazingira magumu hamna.. Tumekubali

Madaraja hatupandi.. Tumekubali

Annual increment hamna.. Tumekubali.

Pay leave..likizo ya malipo hamna... Tumekubali.

LAKINI

Hata hili la kazi maalumu, kweli kabisa hutulipi. Yani mitihani imesahishwa,tumerudi nyumbani.. Mpaka leo? Kweli!?

Hivi Ualimu ni laana?
Uimbaji wa mapambio umepitwa na muda badilini staili ya uimbaji mtasikika tuu.
 
Respect kwa wapumbavu my foot walimu ni wapumbavu we huoni walikuwa wanachapwa fimbo? Narudia Tena walimu ni wapumbavu.ushaona manesi au madaktari wakichapwa fimbo?
Jamani, nafikiri lengo la mleta mada hii kwa wana jamii ni kupata mawazo na hata faraja kama mwana jamii. Nimesoma komenti nyingi zinakosa japo neno la faraja. Tukumbuke kuwa ualimu ni kazi ya heshima. Popote ukimtaja mtaalamu wa aina yeyote ni sharti awe amefundishwa na mwalimu. Ni vema ikiwa tutawaheshimu waalimu na kusikitika nao pale haki zao zinapokosekana. Niwape pole waalimu kwa kukosa stahiki zao kwa wakati. Niwatie moyo kwamba msikate tamaa. Fuatilieni madai yenu kwa utaratibu uliopo kwani serikali ni sikivu wakati wote. Ukiona usiku umeendelea jua mchana nao pia waja.
 
Magufuli anawapenda sana jamani, yeye mwenyewe alikuwa mwalimu, Mke wake ni mwalimu anawathamini sana mchango wenu. Kwa sasa tuwe wavumilivu wakati anaweka miradi ya maendeleo sawa. Hii miradi ni muhimu kuliko kulipana pesa tu kwa kuongezeana mishahara, huko mbeleni mtamkumbuka sana Magufuli kwa mema anayoyafanya sasa hivi.
 
Back
Top Bottom