Hivi wanaoishi maeneo haya na wenyewe wanajiona kabisa wanaishi Dar?

We unayeishi Kibondo unapata wapi nguvu ya kuwasema wakazi wa Dar?
 
Njoo kinondoni yetu uishi mzee

Ova
Tena kinondoni ndo na mpango wa kuhamia Kodi ikiisha hapa.....

Watu humu anaandika anashangaa mtu kuishi uswahilini wakati mwenyewe yupo huko huko,

Huko ushuani wanakula vyakula vya mwezi uliopita huku sisi uswahilini tukila fresh kuanzia morning to night.....

Next stop kinondoni mwanamboka mpaka Biafra, morroco hapo kidgo nasogea makumbusho
 
Sasa Dar ni ipi ukiiondoa hayo maeneo uliyotaja? Kwa akili Yako Dar ni kariakoo?!
 
Pale Kariakoo kati hivi watu wanaweza kupumua kweli kwa msongamano ule?

Kuna dereva wetu mmoja ilikuwa ukitaka kugombana naye mwambie tu "nipeleke Kariakoo" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚ Dar ina wenyewe asee
 
Dar ukitoa elfu 10 kwenye daladala kila mtu anakuangalia.
 
πŸ˜‚ Dar ina wenyewe asee
Mkuu,

Ina wenyewe na wengine wenyewe ndio sisi. Hapo Kariakoo kwetu, familia zimekaa hapo Misheni Kota tangu kabla ya enzi za Paul Rupia anamfadhili Baba Kabwela kwena UNO. Baba yake bibi yangu kajenga Azania Front wamemaliza 1903.

Ila Dar imebadilika mpaka wenyewe tukirudi tunakuwa wageni tunakuta kuna wenyewe wapya. Wengi wanatuona sisi ndio wageni.
 
Wanaita Goms wengine Gms ili kuficha madhaifu


 
Ukiishi mitaa hiyo(Uswazi) ndo umeishi Dar yenyewe sasa!
Wengine hizo mishe mishe na heka heka ndo zinamchangamsha mtu na kumfanya awe sharp na pia unajifunza mbinu nyingi za maisha tofauti na huko ushuani wanaishi kwenye mageti kama jelaπŸ˜‚
 
Mkuu kweli hayo maeneo ni zaidi ya Kijijini,wahi ukanunue shamba manzese,magomeni na mwananyamala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…