Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Suala la nani awe nani katika suala la uzazi liliwekwa na Mungu na kila jinsia ikapewa quality maalumu kwa ajili ya kutekeleza jukumu lake; mwanamke amepewa role yake ambayo huwezi kuilinganisha na mwanaume katika hili ukilifikiria kwa kina lakiniMkuu kuwa realistic sawa anauwezo mkubwa sana na mm nakubali kama kubeba kiumbe mieezi tisa....... lakini jiulize hicho kiumbe anachobeba kajipa mwenyewe? Mind you Kuna aliesababisha kiingie na kukaa tumboni mwake.
Kikubwa nadhani tunapaswa kuelewa/kuelewani kuna suala muhimu sana la haki na wajibu kwa mke na mume. Hivi vitu ni nature ya muumba na hata ukipingana navyo ni kama kushindana na ukuta. Mume ana wajibu kwa mkewe na mke nae vivyohivyo. Sitaki kusema haki ya nani inamzidi yupi hilo linataegemeana na misingi mbalimbali ikiwemo ya imani za dini ambapo jamii husika ipo. Kuna jamii kabisa mke yupo juu ya mume mfano wao ndiyo walipa mahari na wanaolewa na wanaume zaidi ya mmoja. Mwanamke kwa maana rahisi anakuwa na mitala.... yaani anapanga lini nikalale na mume yupi.
Hivyo ndiyo maana tangu awali nilisema haya mambo kuyajadili na kuyapatia jibu la uhakika ni ngumu sana. nilitoa mfano wa ukristo ukifundisha kuwa wajibu wa mume ni kumpenda mkewe na mke ni kumtii....sasa tafuta kwa kina maana ya KUPEND na maana ya KUTII kuna baadhi ya watu wanaweza kuikana imani kabisa. Lakini pia nikasema baadhi ya jamii/makundi Ulaya na America wao wana ndoa za mikataba yenye makubaliano ya lini ndoa itaisha, itaishaje na hata namna ya kuishi ndani ya hiyo ndoa ikiwa ni pamija na mtu kuja na mchepuko wake nyumbani siku akijisikia bila kubughudhiwa na mwezake.
Kwa ujumla haya mabo yanahitaji mtizamo mpana sana ili kujua hiyo 50/50 inaweza apply kwa kundi gani na wakati gani.
Suala la balance ni la kinadharia sana haswa katika nchi zetu za kiafrika ambazo zinaishi kwa misingi ya kidesturi na kidini ambayo kwa kiasi fulani ipo kinyume na hiyo concept