Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Suala la nani awe nani katika suala la uzazi liliwekwa na Mungu na kila jinsia ikapewa quality maalumu kwa ajili ya kutekeleza jukumu lake; mwanamke amepewa role yake ambayo huwezi kuilinganisha na mwanaume katika hili ukilifikiria kwa kina lakini

Suala la balance ni la kinadharia sana haswa katika nchi zetu za kiafrika ambazo zinaishi kwa misingi ya kidesturi na kidini ambayo kwa kiasi fulani ipo kinyume na hiyo concept
 
Sawa ila kama yeye anakusaidia kutafuta pesa basi na wewe ni wajibu wako kumsaidia kufanya kazi za ndani
Tatizo mke akishakuwa provider tu shida inaanzia hapo

mimi laziama nitoe zaidi yake
 
Mkuu huyo kwenye avatar ni wewe? [emoji470][emoji470][emoji470][emoji470][emoji470][emoji470]
Siyo yeye. Labda ni shangazi au mama wa ubatizo. Yeye ni chuma hatari. Trust me. Kuna avatar yake ya kweli bado naitafuta nitakupa nikiipata [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Na wewe za kwako huwa unampa??

Yes madam ninampa na hata akiniambia bana sikiliza this time hela yangu nafanyia hiki naomba uniongezee pesa kadhaa kiroho safi anachuku

Anajua exactly role zake na anajua ana deal na mtu mwenye mind set ya kibabu anafuata mule mule
 
Sawa ila kama yeye anakusaidia kutafuta pesa basi na wewe ni wajibu wako kumsaidia kufanya kazi za ndani

Mama narudia tena kazi za ndani sina wajibu nazo na ndo maana siwezi kuhangaika na nyinyi wanaharakati

Ninyi wa haki sawa ni wa kuweka tu na kusepa
 
Unajua mkuu kuna watu wengi sana hata bible hawaielewi vyema. Ni kweli kwa upande mmoja inasema Mume ni kichwa cha nyumba. Na tafsri ya wengi hapa inaangukia kwenye supremacy...kwa maana ya mwenye nguvu na mabavu juu ya mke....kitu ambacho kiuhalisia si kweli. Kuna jukumu ambalo mwanaume amepewa la upendo kwa mke... kama watu wakilielewa hili vizuri lenyewe tayari linaweka usawa katika mahusiano ya ndoa na wala si kumuweka mwanaume kama mtawala wa mwanamke. Wakorintho wa kwanza 13:4-8 inasisitiza kabisa kuwa upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauna wivu au majivuno. Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi, haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya, upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote. hivyo basi wanaume kujiinua kuwa juu ya wanawake kinyume na haya maandiko wanataka utukufu wao tu si wa kimungu.

Hivyo basi kwa wana ndoa mume anapokuwa na upendo wa dhati kama andiko linavyosema ukachanganya na andiko la utii analotakiwa kuwa nalo mke kwa mume....ndugu yangu raha inayopatikana kwenye couple hiyo ni kama paradiso. Maana kila mmoja anawajibu kwa mwenzake....mume akigawiwa pipi na rafiki zake huko njiani ni lazima ifike nayo kwa mkewe ili wakamege kwa pamoja. Mke hawezi fikia maamuzi ya jambo lolote lile lazima akamshirikishe mume na mume kwa sababu ya upendo lazima amshauri kwa busara na hata kama hakubaliani nalo sana kwa ajili ya upendo atamkubalia mkewe ili tu kutoikwaza nafsi na furaha yake. kosa hutokea pale tu mmoja anapotaka ku abuse nafasi na jukumu lake alilopewa.

Ku declare interest tu mm ni muumini wa usawa wa jinsia. lakini kuna baadhi ya mambo nayaunga mkono na mengine nayapinga. kwa mfano mila potofu dhidi ya wanawake ziwanyimazo fulsa ya elimu, ukeketaji, kuwapora wajane mirathi, kurithi wajane, kuwapa wanawake kazi kwa rushwa ya ngono n.k haya mimi sikubaliani nayo kabisa. Lakini pia sikubaliani na propaganda za wanaharakati wa jinsia wasio na maelezo ya kina wao wameshikilia tu kwa mfano mwanamke ana haki ya kuamua mambo yake ikiwa pamoja na lini ampe mumewe unyumba. Au kulazimisha tu nafasi zote ktk jamii zigawanywe kwa 50/50 bila kuzingatia uwezo na taaluma.

Lakini narudia tena hili masuala ya usawa wa jinsia ni yana mjadala mpana sana kulingana na imani tofauti za dini, mila na utamaduni wa jamii husika hali kadharika maeneo ya kijographia katika ulimwengu huu.
 
Ni kweli sio kweli pia. Kwa kifupi tu, hata mtazamo wa kale wa jamii nyingi ulifanana na mtazamo wa kiimani. Mfano mjane kurithiwa, mwanamke kutorithi mali wala kuajiriwa, majukumu ya mtoto wa kike vs wa kiume n.k. Tatizo lililopenyezwa ni mfumo wa kimagharibi. Tunatumikia matakwa ya wageni ndio maana tumepotea kama taifa. Tumeukana utamaduni wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…