Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

nakuuliza swali,unaniumiza swali,hivi unajielewa wewe
Sasa kati ya mimi na wewe nani anayemjibu mwenzie kwa maswali na siyo majibu maana kwanza maswali yaliyopo kwenye mada tu hadi sasa haujayajibu unazunguka tu halafu na wewe unaniuliza maswali

Mimi ndo nilitakiwa nikuulize kama wewe unajielewa au haujielewi jibu kwanza maswali yale pale juu halafu na wewe ndo uje uniulize ya kwako vinginevyo nimekwambia kabishane na wavulana wenzio hapa nabishana na wanaume tu wanaojua kujibu maswali na kuja na hoja zao
 
nasikia pia wanataka na 'special treatment.'
exactly what they need, they want to be equal to men while receiving special treatment from very same people whom they claim to be equal with.

ndio maana kwenye matangazo ya kazi tunaona maneno kama "women are highly encouraged"
 
Mapenzi ya kweli hayaishi, mali na material zingine ndio huisha.
Maamuzi ya kumuacha mtu hayaji from nowhere, mtu unaweza ishi nae kila akiamka asubuhi akakuona moyo unajaa majuto kwa miaka 40, mtu wa hivyo naweza sema maisha aliyoyachagua yamemfanya awe katili[emoji3][emoji3].
Sawa namaanisha kama mwanamke kaolewa na mwanaume ila hampendi huyo mwanaume lakini mwanaume anampenda halafu baadaye mwanamke akaamua kuvunja ndoa na kumuacha huyo mwanaume kwanini muanze kusema kwamba wanawake ni wakatili wakati hata wanaume wapo wanaofanya hivyo?
 
Hahahaha unajibu kirahisi sana unajua ni kwanini shetani alimuita mwanamke ndo ale tunda halafu akamwambia ampe mwanaume? Kwanini asingemuita mwanamume ndo ale kwanza halafu ampe mwanamke? Najua utakuja na jibu lako hilo hilo kuwa wanawake ni dhaifu kuliko wanaume kitu ambacho siyo jibu la hayo maswali niliyokuuliza anyway ngoja nikuache uamini unachoamini
hata ccm wameweza kumnunua Waitala lakini kamwe hawawezi hata kuwaza kumnunua Lisu. Maana wanajua hawatafanikiwa kabisa.
 
Mada yako inaongelea madai ya wanaume kusema kuwa wanawake mnataka usawa wa kijinsia na sio vinginevyo, hivyo basi hata comments zangu tangu awali zimejikita kwenye kiini cha mada yako(usawa) sasa unapouliza kuwa bado tunaongolea usawa.. nnashangaa sana maana hapo sasa tunakuwa tunaenda kwenye mada nyingine ndani ya mada.

Pili, huwezi ukasema mwanamke na mwanaume hawako sawa halafu hapo hapo unataka majukumu ambayo hata kitamaduni ni ya kwako na Mimi niyafanye. Unapoongelea mgawanyo wa majukumu based on gender huwezi ukaniambia Mimi nioshe vyombo na kupika huo sio mgawanyo wa majukumu my dear na ukitaka hivyo basi kubali na wewe niwe nakubebesha majukumu ya ulinzi na kuchimba shimo la choo siku moja moja.

hizo ndoa unazopenda kuzitolea mfano sijui unazioneaga wapi.
Sasa mkuu mbona umekazania kwenye ulinzi tu mimi naongelea kutafuta pesa na kuhudumia familia kama mwanamke anakusaidia kutafuta pesa na kuhudumia familia wewe unashindwa nini kumsaidia kufanya kazi za ndani na kulea familia?

Mwanamke ambaye hakusaidii kutafuta pesa wala kuhudumia familia basi hata wewe hautakiwi kumsaidia kufanya kazi za ndani wala kulea familia yaani point yangu hapa ni kwamba kama anaingilia majukumu yako basi na wewe ingilia majukumu yake ila kama haingilii majukumu yako baso na wewe usiingilie majukumu yake
 
Sasa kati ya mimi na wewe nani anayemjibu mwenzie kwa maswali na siyo majibu maana kwanza maswali yaliyopo kwenye mada tu hadi sasa haujayajibu unazunguka tu halafu na wewe unaniuliza maswali

Mimi ndo nilitakiwa nikuulize kama wewe unajielewa au haujielewi jibu kwanza maswali yale pale juu halafu na wewe ndo uje uniulize ya kwako vinginevyo nimekwambia kabishane na wavulana wenzio hapa nabishana na wanaume tu wanaojua kujibu maswali na kuja na hoja zao
umesema wanawake wana akili kuzidi wanaume,nikakuuliza akili gani kwa mfano ,unaniuliza tena maana ya akili? unajielewa kweli wewe
 
Siyo useme vyovyote mwanamke anayeona muelekeo wa ndoa hawezi kukuchuna ila mwanamke ambaye haoni mueleko wowote wa kuolewa lazima akuchune sababu kumbuka unapomchezea unampotezea muda wake wa kuolewa

Wakati wewe hauna cha kupoteza maana wewe hata ukifika miaka 40 utaoa tu ila kwake miaka 40 ni ngumu kuolewa sasa kama wewe unampotezea muda wake kwanini na yeye asikupotezee pesa zako?
then hapo hapo unasema mwanaume na mwanamke wapo sawa, inakuaje mwi ngi ne aingie kwenye ndoa at 40 na mwingine ashindwe
 
umesema wanawake wana akili kuzidi wanaume,nikakuuliza akili gani kwa mfano ,unaniuliza tena maana ya akili? unajielewa kweli wewe
Jibu swali langu la kwenye mada kwanza kama hauwezi basi ngoja nikupuuze maana naona hauna la maana unalotaka kusema unabwabwaja tu hapa
 
Sawa namaanisha kama mwanamke kaolewa na mwanaume ila hampendi huyo mwanaume lakini mwanaume anampenda halafu baadaye mwanamke akaamua kuvunja ndoa na kumuacha huyo mwanaume kwanini muanze kusema kwamba wanawake ni wakatili wakati hata wanaume wapo wanaofanya hivyo?
Ndio maana nasema watu me/ke huchagua maisha ambayo mwisho wa siku yanawafanya wafanye maamuzi ya kikatili, kwa lengo la kujikomboa kutoka kwenye hayo maisha.
 
then hapo hapo unasema mwanaume na mwanamke wapo sawa, inakuaje mwi ngi ne aingie kwenye ndoa at 40 na mwingine ashindwe
Wapi nimesema wanaume na wanawake wapo sawa kwenye kila kitu? Inukuu hiyo sehemu unionyeshe halafu kuhusu umri wa kuoa au kuolewa hiyo ni mitazamo ya kijamii tu ila kiuhalisia mwanaume anaweza kuoa na mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wowote ule ambao unamruhusu yeye kufanya tendo la ndoa

Hata kwenye maandiko inajulikana na hakuna sehemu maandiko yamespecify umri maalum wa mwaume kuoa au mwanamke kuolewa na mimi nitaenda kimaandiko zaidi na siyo kitamaduni na mitazamo yenu hii inahopingana na maandiko sasa kama haujui maandiko pole
 
Ndio maana nasema watu me/ke huchagua maisha ambayo mwisho wa siku yanawafanya wafanye maamuzi ya kikatili, kwa lengo la kujikomboa kutoka kwenye hayo maisha.
Sawa mkuu
 
Sasa mkuu mbona umekazania kwenye ulinzi tu mimi naongelea kutafuta pesa na kuhudumia familia kama mwanamke anakusaidia kutafuta pesa na kuhudumia familia wewe unashindwa nini kumsaidia kufanya kazi za ndani na kulea familia?

Mwanamke ambaye hakusaidii kutafuta pesa wala kuhudumia familia basi hata wewe hautakiwi kumsaidia kufanya kazi za ndani wala kulea familia yaani point yangu hapa ni kwamba kama anaingilia majukumu yako basi na wewe ingilia majukumu yake ila kama haingilii majukumu yako baso na wewe usiingilie majukumu yake

Bhana huwezi ukaliweka suala la ulinzi kando hata siku moja unapoongelea majukumu ndio maana nnalitaja kila mara.

Kama mwanamke anatafuta pesa na Mimi natafuta pesa kisha wote tunaleta mezani huko sio kuingiliana majukumu bali ni kusaidiana majukumu, maana Mimi sijaacha kutekeleza majukumu yangu isipokuwa yeye ndio kaamua kuunganisha nguvu kwenye kutekeleza majukumu yangu.

Kama mwanamke anatafuta pesa halafu mimi mwanaume nimekaa tu bila kujishughulisha kivyovyote, huko sasa ndio kumruhusu mwanamke aingilie majukumu yangu.Na mwanaume wa dizaini hii anastahili viboko kabisa.

Halafu kwanza hapa tunaongea vitu ambavyo ni unrealistic tu, ni wanawake wangapi wenye vipato ambao wanapeleka walau hata 50% ya vipato vyao kwenye family running expenses? wengi wenu hata mkiwa na mishaara mikubwa kuliko waume zenu bado waume zenu ndio watabeba sehemu kubwa ya majukumu yanayohusiana na fedha.
 
hata ccm wameweza kumnunua Waitala lakini kamwe hawawezi hata kuwaza kumnunua Lisu. Maana wanajua hawatafanikiwa kabisa.
Sijaelewa mantiki ya hoja yako inaingiaje hapo
 
Wapi nimesema wanaume na wanawake wapo sawa kwenye kila kitu? Inukuu hiyo sehemu unionyeshe halafu kuhusu umri wa kuoa au kuolewa hiyo ni mitazamo ya kijamii tu ila kiuhalisia mwanaume anaweza kuoa na mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wowote ule ambao unamruhusu yeye kufanya tendo la ndoa

Hata kwenye maandiko inajulikana na hakuna sehemu maandiko yamespecify umri maalum wa mwaume kuoa au mwanamke kuolewa na mimi nitaenda kimaandiko zaidi na siyo kitamaduni na mitazamo yenu hii inahopingana na maandiko sasa kama haujui maandiko pole
huwezi kutenganisha hayo maandiko na tamaduni,unajiona ulivyo kilaza,hayo maandiko ni tamaduni za kiyahudi
 
Back
Top Bottom