Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Mwanaume kumsaidia mkeo kazi za ndani siyo kosa wala siyo dhambi kama tu yeye anavyokusaidia wewe kutafuta pesa
Kwa hiyo mume akirudi apige deki, aoshe vyombo, apike na aandae chakula mezani sio
 
Na mwanaume akikosea naye anaadhibiwa na nani?? Au mwanaume hakosei kwa sababu tu 'yeye ndie mwenye ndoa"??
Mungu - Kristo - Mwanamume - Mwanamke. Nje ya hapo ni dhambi ya uasi. Umeona nani anayemwadhibu mwanamume?
 
Nimesoma mawazo ya watu, mie ninapenda nichangie kwa kunukuu kauli ya mpenzi wangu siku moja wakati tunapiga piga story alidokeza ila mimi dawa iliniingia, "Kama mwanamke ameumbwa kuwa msaidizi kwa mwanaume, hivyo basi ikitokea huyu msaidizi akapata nguvu zaidi au akapewa mamlaka au majukumu ya mwanaume mambo yatabadilika kidogo na hali yake ya usaidizi haitakuwepo tena na atakuwa sawa na huyu aliyekuwa anasaidiwa na pengine kuchukua nafasi yake mwanaume hivyo hii inaweza kupelekea mwanaume kujihisi anatawaliwa au kudharauliwa". Kwa nukuu hii, nasema hivi mimi kama Mwanaume, kitu tunachokuwa tunalalamika wakati mwingine ni kwa sababu ya uzembe wetu mahala fulani katika kuwajibika kama kichwa cha familia, tuki wajibika kama Baba wa familia na wao wakafanya sehemu yao kama akina mama nahisi hizi lawama hatutaziona. Naomba kuwasilisha hoja
 
Hakuna anayetaka mwanaume na mwanamke wawe sawa au mwanamke awe juu ya mwanaume ila wanachotaka ni kwamba wanaume mtumie mamlaka yenu mliyopewa juu ya wanawake vizuri mnatakiwa muwalinde na siyo kuwakandamiza
Vitabu vya Mungu vinakataa mwanamke na mwaume kuwa sawa maana mwanaume ni kichwa cha nyumba kama sio family kama Yesu alivo kichwa kanisa... Mwanamke atakuwa chini ya mwanaume mpaka dunia itapita na hao wanaojihangaisha kupinga maelekezo ya Mungu mwenyewe na kupiga debe haki sawa kwa kila kitu washindwe na wako kinyume na Mungu yaani wanapinga Mungu.. Wanajidanganya.

Uwe sawa na Mwanaume yaani nawe uwe na dudu linalosimama na kuwezesha kutia mimba na kuzalisha au!!??

Uwe sawa na Mwanaume yaani nawe uwe kichwa cha nyumba au familia au!!??
 
Kwahiyo je akikusaidia majukumu yako na wewe utamsaidia majukumu yake??
Asante mkuu. Nadhani hapa umejibu kila kitu.
Chanzo kikuu cha ndoa nyingi balaa linaanza mwanamke akishazaa tu. Sijui dharau na kiburi vinatokeaga wapi aisee.

Okay wanasemaga jukumu la kulea familia ni la baba. Its okay na ni sawa kabisa. Sasa kama mimi jukumu langu ni kulea familia hasa hasa financialy ni kwa nini mwananke wangu akafanye kazi sasa. Yaani nimlipe house girl wakati mke wangu yupo. No thank you. Kama tumeamua,sote tifanye kazi then vitu vingine lazima uingie gharama tu aisee
 
Shida siyo mwanamke kuwa na cheo ila shida ni mwanamke kukusaidia majukumu yako yaani unataka mkeo akusaidie majukumu yako ila wewe hautaki kumsaidia majukumu yake kwahiyo unataka yeye ndiyo afanye majukumu mengi kuliko wewe kichwa cha familia?? Uliona wapi makamo wa rais akawa ana majukumu mengi kuliko rais??
Mwanamke mwerevu hata kama ana cheo kikubwa kiazi gani lakini anajua majukumu yake ndani ya ndoa ni yapi. Hawezi kuruhusu upuuzi huu unaoutetea. Kuna kazi ambazo baba anaweza kusaidia home kama usafi wa mazingira nje ya nyumba au mifugo. Lakini eti mumeo aingie jikoni kupika au kufua nguo au kudeki. Hapana aisee. Tutawakimbia tu muolewe na hizo degree zenu
 
Nina miaka 20 sasa kwenye ndoa yangu na ninajua ninachokiongea sasa sijui unataka uniambie nini kuhusu ndoa tatizo wanaume wengi hamtaki kuambiwa ukweli
Unawaponza wenzio na kama umeolewa sidhani kama hiyo ndoa yako itafika mbali ukiendelea na hizi akili zako aiser
 
Kama mkeo anakusaidia kulipa gharama za mahitaji ya nyumbani na wewe unashindwa nini kumsaidia kazi za nyumbani?? Halafu kwani umeambiwa wewe ndiyo utafanya huku yeye akiwa amekaa tu si mnafanya wote

Hivi mfano wewe na mkeo wote mnatoka nyumbani alfajiri mnarudi usiku unataka mkirudi mkeo ndiyo afanye kazi zote za ndani peke yake wewe ukiwa umenyanyua miguu juu kwamba unashindwa kujiongeza kumsaidia japo kazi mbili tatu au unadhani yeye ndiyo hachoki huko kazini??
Kwa hiyo mume akirudi apige deki, aoshe vyombo, apike na aandae chakula mezani sio
 
Mungu - Kristo - Mwanamume - Mwanamke. Nje ya hapo ni dhambi ya uasi. Umeona nani anayemwadhibu mwanamume?
Ndiyo maana nikakwambia nipe andiko lilalomtaka mwanaume kumuadhibu mwanamke eti kwa sababu tu yupo chini yake!!

Na kumbe umeshajua kuwa hata Mungu naye tunamkosea ila hatuadhibu kadiri ya makosa yetu sasa wewe ni nani unayetaka kumuadhibu mwanamke popote anapokosea??
 
Mbona tunaafanya yote haya mamy jmn kama kuna mmoja au wawili hawawajibiki kwenye majukumu au wajibu wao ni hao hao sisi wengine tuko. Vizuri sana
Hakuna anayetaka mwanaume na mwanamke wawe sawa au mwanamke awe juu ya mwanaume ila wanachotaka ni kwamba wanaume mtumie mamlaka yenu mliyopewa juu ya wanawake vizuri mnatakiwa muwalinde na siyo kuwakandamiza
 
Siyo ubwege bali anajua nini maana ya ndoa yaani ndoa ni wanandoa wote kuvumiliana na kusameheana sasa wanaume wengi wanataka wavumiliwe na wasamehewe wao tu ila wao kuwavumilia na kuwasamehe wanawake zao hawataki
Lazima mwanaume awe na ubwege fulani mamabo ndo yataenda
 
Shukrani mkuu umenena vyema na huo ndiyo ukweli
Nimesoma mawazo ya watu, mie ninapenda nichangie kwa kunukuu kauli ya mpenzi wangu siku moja wakati tunapiga piga story alidokeza ila mimi dawa iliniingia, "Kama mwanamke ameumbwa kuwa msaidizi kwa mwanaume, hivyo basi ikitokea huyu msaidizi akapata nguvu zaidi au akapewa mamlaka au majukumu ya mwanaume mambo yatabadilika kidogo na hali yake ya usaidizi haitakuwepo tena na atakuwa sawa na huyu aliyekuwa anasaidiwa na pengine kuchukua nafasi yake mwanaume hivyo hii inaweza kupelekea mwanaume kujihisi anatawaliwa au kudharauliwa". Kwa nukuu hii, nasema hivi mimi kama Mwanaume, kitu tunachokuwa tunalalamika wakati mwingine ni kwa sababu ya uzembe wetu mahala fulani katika kuwajibika kama kichwa cha familia, tuki wajibika kama Baba wa familia na wao wakafanya sehemu yao kama akina mama nahisi hizi lawama hatutaziona. Naomba kuwasilisha hoja
 
Yepi mkuu?? Jamii nyingi za kiafrika zinamkandamiza mwanamke na tamaduni hizo kandamizi zilianzishwa na wanaume sasa mnawalinda vipi??
Mbona tunaafanya yote haya mamy jmn kama kuna mmoja au wawili hawawajibiki kwenye majukumu au wajibu wao ni hao hao sisi wengine tuko. Vizuri sana
 
Punguza hizo negativity. Simba dume hawindi but wakwanza kula
Kwahiyo kumbe wanadamu tumeumbwa kwa mfano wa wanyama na tunatakiwa tufuate maisha ya wanyama??

Sasa pale mwanaume alipoambiwa na Mungu kuwa atakula kwa jasho lake sijui pafutwe tu maana tumeshakuwa wanyama sasa!!
 
Back
Top Bottom