Hivi wanaume umeishawahi kuishi kwenye nyumba inayomilikiwa na mwanamke ambaye labda ni mke wako au mpenzi wako?

Simulia ilikuwaje
 
Hebu funguka na wadau nini kilitokea?


#nyumayapazia
Mkuu kama una mawe fanya hivyo.
Ila kama tia mchuzi tia mchuzi.
Mawe yanakupa nguvu ya kufanya lolote muda wowote ule.
Tena inaonekana unaenda kutembea😀😀
 
Kazi tunayo....mwanaume lazima uwe mwanaume.....Kuna mwamba alikaa kwa mama muuza wakati twasotea kazi mradi wa........kila asubuhi twaenda sabahi,shemeji za asubuhi.....twakaribishwa na glass ya gongo......maisha ni safari.....jamaa ni senior surveyor
 
Aisee.
 
mawazo ya kijinga kama haya wanayo vijana graduates na wazembe wapenda vitonga. Tafuta pesa broo uishi kwako wanawake hawafai kwenye chao
 
Kuishi kwenye nyumba ya mwaname sio dhambi ila dhambi kubwa ni siku mkizinguana akakufukuza uwe huna hela na pakuishi huna. Fedhea mbaya sanaa asee
Akili ni hii;Hata kama umemuoa na mna watoto kabisa ishi kwa tahadhari.
Hakikisha una nyumba yako binafsi ambayo yeye haijui. We jenga ama nunua kimyaa kimyaa kama wazazi wako hai wafahamishe.
Kama huna uwezo wa kujenga basi ukianza kuona chenga chenga tuu fanya utafte nyumba ya kupanga fastaa, weka mazaga muhimu kaa mkao wa kupeperuka.
Siku akiropoka tuu wewe yuleee,atashangaa tuu haurudi walaa hunuulizi. Huyo hata ukimrudia heshima itakuwepo kisha jenga mjengo wa kimyakimyaa
 
Hapa napokaa kuna jamaa kauzu, hasalimii na ukimsalia haitiki, nilisikia mkewe akisema jamaa hataki mazoea na anataka mkewe asiongee na mtu ila mke kagoma
Juzi usiku nikasikia vishindo nje mara mawe yana rushwa kutoka nimekuta show ya kimya kimya jamaa katimiliwa na kaondoka.
 
Haya maisha,ni kitu kingine.
1. Unaweza kuishi kwake,kama unapendwa,na uwezo huna. Sawa,kwa mda utakaa,ila kikubwa soma mazingira. Na kosa kubwa,mkaaji utakuta hajiongezi. Kama umepewa hifadhi ya mda,onyesha msimamo. Na ikiwezekana ukipata kodi,kapange,uwe kwake kukiwa na haja. Na pia ukiwepo,jishughurishe na chochote siyo ukae tu usubiri kuinamisha.

2. Kuna wengine yupo radhi kuachia kila kitu mikononi mwako. Kama kweli amekolea. Wa hivyo ni muelewa,ukimhamisha mtahama. Kwake apangishe,mkapange. Ila kuishi kwake,utahangaika.

3. Kuna wengine akili zimefyatuka. Hata wanaume wapo wa hivyo. Anaweza akakutafuta na akalia. Ila sasa,ukiwa kwake,sijui wazimu,nini. Hata kama mnapiga sarakasi,atakugeuka na akufukuze. Tena hata majirani watajua mshikaji kuzenguliwa hapa.
-Mwanamke anaweza kupata hifadhi kwa mwanaume.
-Mwanaume,anastahili hifadhi kwa mwanaume mwenzie. Lakini umario umekuwa mwingi
 
Shauri zenu, yakiwakuta mje kutusimulia.
 
Siyo ukame wala msoto, sisi kwetu hatuishi nyumba ya mume. Mwiko.

Mimi binafdu mume anaishi kwangu leo miaka zaidi ya 40 ya ndoa yetu na ana majumba yake.

Siwezi kuvunja mafundishobha wazee wetu, mama zetu tumewakuta wameolewa lakini wanaishi kwao si kwa waume zao.
Na mwanamme hamiliki kitu ndani ya nyumba zaidi ya nguo na pumbu zake tu.

Siku mwanamme ukikuta kufurushi cha nguo zako nje ya nyumba ndiyo usanzuke.
 
Kabila gani
 
Ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…