VINICIOUS JR
JF-Expert Member
- Dec 29, 2022
- 208
- 518
Bila shaka mko poa wana jukwaa na wale mabingwa wanaendaelea kusherekea ubingwa wao.HALAA MADRID. Moja kwa moya kwenye mada, wakuu nina rafiki angu kaoa mwana mke kahitimu chuo huko daslam miaka mitatu iliopita nadhani ni diploma ya uwalimu ila bado hajeajiriwa sasa huyu mwanamke nifull jeuri yani jamaa akiacha laki, 20 au 30 anaipiga yote na hataki kuulizwa kuhusu matumizi akiulizwa anakua mbogo, ndani ni full kununa anaweza ambiwa mke naomba remote lakini hasilete, wakipishana kauli kidogo anadai wagawane vitu aende kwao Daslam wakati vitu kavikuta na ni mama tu wa nyumbani, kadukua mawasiliano ya mume wake yani huyo mke akinasa mawasiliano ya mchepuko wa mumewe ni full mafumbo. Mfano naona sahizi upo kwenye penzi jipya. Sasa jamaa kagundua juzi kuwa mke wake kamdukua yani jamaa kamind sanaaa yani calls na texs zote ziwe za siri(binafsi) ,za kipuuzi, za wana,ndugu na hata boss mke anaziona. Yani boss akimpgia jamaa kumpa hela mke anajua, akipishana kauli na boss anajua. ukijumlisha na vitabia vingne vya mke wake mwana anabaki kujilaumu tu kwanini alioa, yani aliyoyatarajia kwenye ndoa ni tofauti anayoyakuta mke ni full kuonesha makucha, kuna mda wakigombana dem anachukua kisu na kutishia kumchoma jamaa , anadai akiachana na huyu haji tena kuoa. Kwahyo mliopo kwenye ndoa haya yote wanaume inabidi uyavumilie yani unafanya kazi ngumu unalipa kodi unamlisha, unamvisha akitaka kutembelea kwao unampa nauli mwisho wa siku anakuzarau!!! Namuonea hadi huruma yule mwamba. Wanaume wote mungu awape maisha marefu.