Leo kama bahati tu, nimekutana na yule mzee ambae ameweka kuanzisha chanzo cha umeme kupitia sumaku. Nimeshangaa snaa kwamba video alitembelewa na waziri wa nishati na mkurugenzi wa shirika la tunaangaza maisha kwa mgao.
Unajua ile mashine yake alivounda, haipigi kelele wala kutoa hewa chafu. Unaeka tu pembeni hata seating room ukacheki tv, ukawasha friji, kuchaji simu na kila kitu yani. Alafu anaunda kwa size tofauti kutokana na mteja. Naona zingine anatuma mikoani kama geita na mbeya.
Unajua ajabu nikwambie sio hii mashine aliyounda huyu mzee. Ajabu ni kwamba anasema hajasoma yani vyeti hana kabisa vya ufundi. Anasema robo tatu ya maisha yake amespend kwenye mavyuma tu na hata Aka yake wanamuita hivyo hivyo 'machuma chuma'.
Kuna basi lipo mbuga moja kubwa kule kusini Afrika kwa maphorisa aaah sorry Ramaphosa. Ile mbuga inaitwa kruger, wadau wa utalii wanajua ukubwa na watalii wanaoenda kwny hii mbuga kutoka 'duniani'. Sasa huyu mzee alipewa kazi ya kuweka ufundi wake kwenye moja yw mabasi ambayo watalii hutumia kuzunguka kwenye mbuga.
Lile basi ni kubwa lina gorofa moja kama yale ya london pale katikati.
Yani imagine jamaa wamemtoa huku kupeleka ujuzi wake umbali wote huo. Nadhani pia ni invention ya kwanza kufanyika kutumia sumaku kama chanzo cha umeme.
Najaribu kuwaza hii kitu angevumbua mtu kama Elon au wale kina gates ingekua kitu kubwa kiasi gani??? Wanafunzi wa vyuo vikuu huenda pia kujifunza pale. Hii ni invention ambayo jamaa inampa maisha ingawa mwnyw anasema badooooo.....
Imagine maisha yake yote anaishi bila kelele za luku mana hii mashine wataalamu wa tanesko wanasema hizo sumaku ni zile 'permenent' ambazo haipungui nguvu miaka nenda rudi labda uichome kwenye motoo mkali sana ndio inaweza haribika.
Hii sio tafiti ya mastaz wala doctor of philosophy, ni uvumbuzi umegusa jamii moja kwa moja. Hizi tafiti zetu za mlimani na sua zinatoa majibu kama haya kweli? Najua hivi vipaji vipo vingi lakini binafsi hii kwangu ni kwanza naiona alafu haina support kabisa kutoka kwa wenye mamlaka mzee asaidie kutatua mgao wa umeme ujueee.....mie nshaeka oda yangu ndgo ntaitumia kwny kibanda changu...naweka linki hapa mchekini injinia anaestahili digrii ile ya heshima kabisa kutoka kwa watanzania
View: https://youtu.be/93NXHr3fxpo?si=VpLvNrsFl1aD-5J4