Hivi watu wanaonuka midomo huwa hawajijui?

Hivi watu wanaonuka midomo huwa hawajijui?

Yap! kujisikia vibaya lazima lkn kwa mtu mwelewa atakuona wewe wa maana sana, kiukweli mimi mwenyewe nampenda sana mtu anaeniambia ukweli wa madhaifu yangu haijalishi litaniuma kiasi Gani lkn nitachukua hatua za haraka kuhakikisha nalekebisha.

Nina ushuhuda wa madhaifu yangu mengi tu ambayo niliyajua kupitia watu wenye hawana unafiki na niliyafanyia kazi.
Safi sana mkuu, hongera kwa kuwa na watu walionyooka
 
Watu wasafishe sehemu zote zilizo wazi, kuna wengine wananuka vipapa jamani chaah!!
Sijui na wanaume zao wanaishije huko majumbani, unakuta mwanamke ananuka shombo la papa mpk wewe mwanamke mwenzie unaziba pua.!

Wanaume sasa midomo, miguu yani kavaa viatu bado anatoa halafu. Sasa akivua buti lake la jeje patakalika kweli?? Mapombou leo tuyaache huko ndo balaa..!! 😹😹😹
😁😁😁🙌una hoja usikilizwe
 
Heshima yenu wana jukwaa, mimi huwa najiuliza hawa watu wanaonukaga midomo huwa hawajijui kwani.

Kuna mbaba mmoja huwa anakujaga hapa ofisini kuna muda anaweza akawa anaongea karibu na mimi namsikia kabisa mdomo wake unatoa harufu, sasa najiuliza hata nyumbani mke wake ameshindwa kumwambia, yeye mwenyewe je hasikii hiyo harufu.

Kwa mnaofahamu hili tatizo dawa yake ni nini, tuwasaidie watu wanaopitia hii changamoto.
Kipindi hiki (mwezi huu) wako wengi sana.
Naomba niishie hapo
 
Ok. Sikuwahi kujua km kuna tongue cleaner
Ila me brush ninazotumia the other side huwa kuna km another brush lkn huwa ndogo na ngumu, niliskia kuwa ndio special kwa kusafishia ulimi
Unazotumia nazo nzuri pia mm nimeweka suggestions kwa wale Ata kimoja hawana some wanasukutua tu maji ila it's fine unachotumia maan inasafisha ulimi pia
 
Zipo kama chuma ivi or uh just Google ☺️
Nimeziona 🤣🥰🥰
For the first time in my life ndio nimejua km kuna hii kitu. Kweli JF ni shule
Screenshot_20250327_171354_Google.jpg
Screenshot_20250327_171344_Google.jpg
 
Usafi wa kinywa kwa kina unahitajika, Wengi wao huwa hawasugui Ulimi na mswaki.

Sipendi mtu anae toa harufu kinywani, huwa naboreka, nawaza mwenza wake anawezaje kuvumilia Denda? Au kupumuliana.
Hiyo harufu, Woiiiiiiih.
Pia kutokunywa MAJI mengi na pia kutotibu magonjwa ya kinywa!
 
Screenshot_20250328-115600~2.png

Atumie floss picks mara baada ya kula nyama na atumie chai yenye viungo vya mchai chai itasaidia kupunguza bacteria walio kwenye kinywa.
 
Back
Top Bottom