Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Naomba msiwaamini watu kama @dos.2020 na wenzake wanaotaka kuleta Historia za mapokezano ya waarabu wa Oman waliogawana zanzibar kutokea Muscat Oman.
Nilimsoma kwa makini sana mkuu dos.2020 kuhusu maelezo yakealiyotoa kuhusu Wazanzibari na Wazanzibara.

Nilikubaliana naye kwa ufafanuzi aliotoa kuhusu uingiaji wa watu toka bara kwenda visiwani kwenye miaka hiyo aliyochagua kuiongelea.

Hakunishawishi kuamini kwamba matatizo yalyopo visiwani humo msingi wake ni mvutano wa watu kutoka bara na wale ambao ni wa palepale, ambao hakuwaeleza kinagaubaga ni nani hasa.
 
wazanzbar ubaguz upo kwny damu kama wahindi vile. mtu kutoka bara ukienda zanzbar hupat kaz kirahisi kama wao wakija bara
 
Hasan Moyo?

huyo mzee ametokea Songea, Na Zanzibar kashika nyadhifa kubwa za uwaziri kwa miaka mingi sana, Japo yeye mwenyewe likua anakanusha kwa kusema kuwa baba yake ndie aliehamia Unguja, lakini kwa taarifa za kuaminika ni kua hata yeye Hakuzaliwa. Na amekua akikiri wazi tu kuwa yeye ni mbara. Lakini yote hayo yamekuja baada yeye kujiunga na harakati za Maalim Seif, wakati akiwa CCM alikua akitamba na kuropokwa ropokwa kuwa wao ndio wamiliki wa Zanzibar.
 
Nadhani nimeanza kupata mwanga wa kutosha kuhusu 'KERO.'
 
wazanzbar ubaguz upo kwny damu kama wahindi vile. mtu kutoka bara ukienda zanzbar hupat kaz kirahisi kama wao wakija bara
Kule kwenye hoteli za kitalii katibia 100% ya wafanyakazi ni watanganyika
 
kama umewahi kusikia watu wabinafsi basi ni huyu mtoa mada, kwa hiyo watu wengine wasiende kuishi zanj ili unufaike na nini????
 
wazanzbar ubaguz upo kwny damu kama wahindi vile. mtu kutoka bara ukienda zanzbar hupat kaz kirahisi kama wao wakija bara

Mkuu ulienda ukakosa kazi? Karibu 30% ya adult wakaazi wa Unguja ni wabara
 
Naona kama kuna tofauti ya maelezo kati yenu. Maelezo yako yanaeleweka, hata kama bado nina maswali kadhaa juu yake.

Labda nikuulize tu kwa haraka haraka, kuna sehemu unaposema:

"Hawa wazanzibari wa wakati huo ni nani hasa, waarabu?
Walikua ni watu wa jamii mchanganyiko wakiwemo waarabu, waafrica na wahindi

Kulikuwepo na waafrika waliotambulika kama wazanzibari; kwa maana hata wale wahamiaji wa awamu ya kwanza (watumwa) nao inaonekana uraia wao pia ulikuwa bado ni wa shaka!

Hapana Uraia wao haukuwa na shaka.


Huyu ndie aliyekua Waziri Mkuu wa Zanzibar Baada ya uhuru, Alikua Muafrica. Na ndie serekali yake iliyopindule kwenye yale mapinduzi ya 1964. (Mohammed Shamte)

 
Tukimaliza hili sasa, tunaweza pia kuuliza maswali juu ya watu ambao asili zao zilikuwa uarabuni. Wote au wengi wao ni wale waliokuja na Sultan na kuweka makazi Zanzibar, na hakuna waarabu wengine waliokuja baadae kweka makazi yao hapo?

Sultan hakuja na watu, ila alikuja yeye na watendaji wake.
Waarabu walikuepo Zanzibar kabla ya hata ya ujio wa Sultan, na wao ndio waliomuomba aje. Kabla ya kuja yeye Zanzibar ilikua ikiongozwa na Machotara wa kiarabu.
Nahuyu Sultan alikuja kupambana na Mreno, na akamuondoa maeneo yote ya Zanzibar na Bara wakabakia msumibji huko ambako Sultan hakufika. Na eneo lote likawa chini ya himaya yake mpaka wazungu walipokuja kugawa mipaka ya kutawala bara la Africa hapo ndipo akabakishiwa visiwa vya pwani na eneo la mwambao tu.
Barua za mawasiliano baina ya Sultan na watawala wa Zanzibar zimehifadhiwa kwenye makumbusho nchini Oman mpaka hivi sasa.

Na kuhusu waarabu waliokuja Baadae kuweka makaazi, Walikuepo mkuu Ila hawakuwa wengi.
 
Na kuhusu waarabu waliokuja Baadae kuweka makaazi, Walikuepo mkuu Ila hawakuwa wengi.
Asante mkuu kwa kujibu swali langu ambalo nililiuliza vibaya.

Nilikuwa na maana ya hawa waliokuja baadae.

Je, pamoja na kwamba walikuwa ni wachache, wao walitambuliwa kuwa ni 'wazanzibari'; ingawa na wao kama wale weusi waliotoka bara walikuwa ni wageni vilevile!
Niseme tu kabla ya yote, hulazimiki kujibu hili swali. Siyo la muhimu sana kunipa ufahamu juu ya Zanzibar, kama niliopata kutoka kwako..
 
Jamaa wabaguzi hawa balaah, wenyewe kwa wenyewe tu wanabaguana , muunguja na mpemba wanabaguana , Sasa naona mnazidi kuextend ubaguzi wenu
 
Ukisema Zanzibar ni ya Wazanzibar na huku mmejazana Bara kuanzia kariakoo, chanika hadi Kigoma nawaona vituko kweli...acheni dawa iwaingie... hako ka wilaya ambako unaweza kuzurura siku moja na ukakamaliza kote kasiwatie kiburi...
 
Huku Bulwa kuna Wapemba wengi ndiyo wenye maduka na wanalima iliki, wala sisi hatuoni shida yeyote.
Ile ki uhakika kabisa kuwajibu watu wa hoja hizo ni kupoteza nguvu kabisaaa manake vile wamejaa huku na vile wako huru unaweza shangaa kabisa mtu wa hivi na hoja za hovyo kabisa, waje wawachukue ndugu zao uku wakae huko tuone

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Waarabu walikuepo Zanzibar kabla ya hata ya ujio wa Sultan, na wao ndio waliomuomba aje. Kabla ya kuja yeye Zanzibar ilikua ikiongozwa na Machotara wa kiarabu.
Asante mkuu dos.2020, kwa elimu hii maridhawa.

Niliahidi kwamba nitakuja na maswali mengine muhimu, pengine haya yatakapojibiwa, elimu yangu juu ya siasa za Zanzibar itakuwa imepanuka vya kutosha.

Katika mstari huo mmoja niliou'quote hapo juu, nilikuwa tayari na swali juu yake kabla ya wewe kuuandika humu. Hawa machotara wa kiarabu (bila shaka na weusi); yaani baba waarabu na mama weusi (waafrika).
Hawa nao unasema walikuwepo wengi kabla ya ujio wa Sultan, na kwamba ndio hasa waliomkaribisha sultan aje atawale. Kwamba wao ndio walikuwa ni watawala, ingawaje baba zao waarabu walikuwepo hapo Zanzibar.

Swali la kwanza ni hili: Weusi (waafrika) asili wa Zanzibar hawakuwepo? Acha hawa waliotokana na utumwa; na kama walikuwepo, wao siasa za utawala juu yao hazikuwahusu kabisa?
Machotara, ambao walikuwa ndio watawala wao kabla ya ujio wa Sultan, hawa weusi hawakuwa na kauli yoyote juu ya kumkaribisha sultan aje awatawale- Swali nimelifanya kuwa refu maksudi ili nilikamilishe.

Pili, na pengine hili ndilo muhimu sana katika siasa za sasa za Zanzibar - Uwingi wa hawa Machotara Zanzibar sasa ukoje? Ni wengi zaidi ya Wazanzibara, wakiunganishwa pamoja na wazanzibari (weusi) wale wanaotokana na utumwa; kiasi kwamba ndiyo sababu kwa mfano Hamad Seif kuwa anaporwa ushindi waliokuwa wakimpa?

Hili la weusi asili (waafrika weusi) wa Zanzibar kutokuwa na mchango wowote, au kutokuwepo kabisa linanitatiza na bado sijapata jibu lake sahihi.

Natanguliza shukrani, mkuu wangu dos.2020.
 
Samahani mkuu kwa kuwa nachelewa kukujibu, mambo ni mengi sana hua nakosa utulivu wakutulia JF.

Zanzibar hakuna muafrica asili, Kwa sababu jamii ya Zanzibar ilichanganyika sana asilimia kubwa ya watu wa zanzibar ni machotara. Asilimia kubwa ya watu wa Zanzibar wananasibishwa na Ushirazi ambao asili yao ni Iran. nahawa waliokua wakijiita washirazi ni uzao wa (Wapersia / Waarabu / Waafrica) Kumtafuta muafrica asili Zanzibar ni sawa na kumtafuta samaki asili bahari yetu, yawezekana waliokuepo mwanzoni lakini wakapotea kwa kuchanganyika na jamii nyengine. Na ndio mana hata wakati wa biashara ya utumwa iliposhamiri watumwa walifuatwa Kanda ya ziwa na congo, lakini hakuna mtu aliyefanywa mtumzwa Zanzibar, kwa sababu jamii yote ilikua inafanana kitabia pamoja na kitamaduni kiujumla.
Hakuna kabila la kiafrica asili Zanzibar, na fanya tafiti ndogo hebu hao wanaosema Zanzibar ni ya waafrica waulize ni waafrica wa makabila gani? hapo ndipo wanapokwama, Mbona Waafrica wa Tanganyika wote makabila yao yanajulikana? Lakini wa Zanzibar kwanini hawajulikani?
 

Population ya machotara Zanzibar imepungua sana since 1964, watu Zaidi ya 50,000 walikimbia Zanzibar 64 na 71 na kuwa wakimbizi, (Oman, UAE, Kuwait, Kenya, U.K, Canada) wengi wali settle kwenye hizi nchi. na baaadae 1995. Kwahio population ya machotara imedecrease kwa kiwango kikubwa sana.
ILa ushindi wa hamad haukuwa ukitokana na machotara, ushindi wa hamad ulikua unatokana na Wazanzibari wote. Population ya machotara iliopo Zanzibar kwa sasa haiwezi kushinda hata jimbo moja achilia kura zote. Hapa ndipo pale ninaporudia kuwa wazanzibari wote Waafrica na waarabu wote wanaongea lugha moja na wana malengo na misimamo mimoja. Hizi lugha za uarabu na ufrica zinaongelewa na serekali ya bara ili kupata sapoti kwa wananchi wake kwa wanayoyafanya Zanzibar kuwatawala kwa nguvu.
Zanzibar huwezi kukuta mtu ana care masuala ya miaka 200 nyuma ishu za masuala ya utumwa, ni mambo ambayo yameshapitwa na wakati na hayana mahusiano yoyote na mazingira ya kijamii ya sasa, Ukipititakwenye vibaraza vya kahawa utakuta waafrica na waarabu wapo pamoja wakipiga story, ila ni viongozi wa CCM bara pamoja na wale vibaraka wao wachache ambao hawawezi kupata hata 15% pakiwa na tume huru kule zanzibar wanaondelea kuhubiri hayo mambo.

Swala kuu la kujiuliza, ni muafrica yupi au mzawa yupi ambae serekali ya Tanganyika anamlinda na kumkinga kule Zanzibar? mbona hao anaosema anawalinda hawana uwezo hata wa kupata 20% ya kura?
 
Ahsante.

Niseme tu kwa kifupi kwa sasa hivi kwa kukosa muda.

Historia au maelezo haya hayajitoshelezi hata kwa kutumia mantiki tu?

Hawa machotara walitokana na waarabu au Persians na weusi wa wapi?

Inawezekana weusi wa Zanzibar, hasa wanaume walisombwa na kupelekwa utumwani hadi wakaisha wote visiwani?

Nitarudi tena kuliangalia vingine swala hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…