Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Ni sawa na mfano wa Nyuki wachache waliojiundia jumba lao hatimae wakatokea Kundi kubwa la Mchwa na kuamua kulivamia hilo Kundi dogo la Nyuki...... Je hilo Kundi dogo la Nyuki litakua salama pamoja na hayo makaazi yao!!!!
Thought experiment fikirishi - jibu maakazi ya nyuki/mzinga utabadilika asili na kuchukua umbile la kichuguu cha mchwa . Je hawa nyuki wachache wakivamia kichuguu cha mchwa milioni 50 ,nini matokeo? Kichuguu hakiterereki kabisa kitabakia salama salmini na umbile lake asili. Utawala wa wengi lazima kutambua na kuheshimu haki za wachache ilikuepusha udikteta wa wengi kwa wachache.
 

Hakuna mtu wa Zanzibar ambae alifanywa mtumwa, Hili unaweza kutafuta vitabu vyote vya historia hata hutalikuta hilo.
 
"Thought experiment fikirishi"?

Hili limezaa wazo kichwani mwangu: Inawezekana "weusi asilia" wa Zanzibar walitoweka, kama hao nyuki ilivyowalazimu kuhama mizinga yao baada ya kuvamiwa na mchwa?

Hao watu walikwenda wapi, maana siamini kamwe dhana ya kwamba visiwa vya Zanzibar havikuwa na watu (weusi), kabla ya ujio wa wageni visiwani humo. Hili siliamini kamwe!
 
Hakuna mtu wa Zanzibar ambae alifanywa mtumwa, Hili unaweza kutafuta vitabu vyote vya historia hata hutalikuta hilo.
Sasa walikwenda wapi? Walitoweka vipi na wakabaki Machotara na wageni wengine waliokuja visiwani humo!

Hili ni swali linalohitaji jibu, na bado jibu sijaliona popote.
 
Kalamu kimsimgi Uko vizuri sana wengi wanAkusikiliza hata kama kawakubiliani n.a.

na wewe
 
Sasa walikwenda wapi? Walitoweka vipi na wakabaki Machotara na wageni wengine waliokuja visiwani humo!

Hili ni swali linalohitaji jibu, na bado jibu sijaliona popote.
Na hutoliona mkuu, mana hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wa muafrica asili Zanzibar kabla ya mtu mwenigne, ni hoja ya kinadharia tu lakini facts zinakosekana.
Na ndio mana kauli mbiu ya wa Zanzibar ni kuwa, Zanzibar ni ya Wazanzibari.
 
Na hutoliona mkuu, mana hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wa muafrica asili Zanzibar kabla ya mtu mwenigne, ni hoja ya kinadharia tu lakini facts zinakosekana.
Na ndio mana kauli mbiu ya wa Zanzibar ni kuwa, Zanzibar ni ya Wazanzibari.
Hapa ndipo penye udhaifu wa hoja za upande wa waarabu na wageni wengine waliokuja visiwani humo na kuyafanya makazi yao.

Watu hawawezi tu kupotea wasiwepo, halafu wengine waibuke tu na kudai wao ndio wa hapo!

Hata kwa kutumia akili ya kawaida tu, hapawezi kuwepo nadharia dhaifu kama hiyo popote duniani.
 
Mleta mada unatakiwa ujue kuwa siku zote visiwa huwa havina mwenyewe. Vyote duniani raia wake ni wahamiaji waliotoka nchi kavu na kuvifuata.

Hayupo mwenye jeuri ya kujiita mtu wa kisiwa fulani akijidanganya kuwa na haki ya umiliki. Karume asili yake ni huku bara, Mwinyi asili yake ni kisarawe na wengi tu asili yao sio Unguja wala Pemba.

Ubaguzi wa kusema eti visiwa vinapoteza ule uasili wake ni kujidanganya tu, hakuna mwenye hati miliki ya visiwa vyote duniani.
 
Hussein Mwinyi anawanyoosha kwelikweli lazima wapagawe.
 
Huku Bulwa kuna Wapemba wengi ndiyo wenye maduka na wanalima iliki, wala sisi hatuoni shida yeyote.
Roho ya ubaguzi inatesa watu. Pale Namanga walikuja enzi za uongozi wa Mwinyi na wakatengeneza pesa ya maana ukizingatia enzi zile maduka yalikuwa machache hapa Dar.
 
Yani hili suala nilikuwa nazungmza na mzee leo asubuhi mimi ni mpemba tena wa chake chake kabisa lakini kuna baadhi ya wazanzibar wenzetu mna roho mbaya sana za kibaguzi hamfai sjui mngekuwa waarabu ingekuwaje
 
Kwani kinachoufanyeni muung'ang'anie huu Muungano ni kitu gani kama hamnufaiki nao? Maana naona wazanzibari wakihoji muungano mnaleta majeshi kukandamiza wanaohoji 😀
 
Wanaonufaika ni wazanzibari lkn majority ndio wanaopiga kelele kutoutaka muungano.

Katia ya Hayati Nyerere na Hayati Karume ni nani alimfuata/alimshauri mwenziwe waungane!!!?

Wazanzibari hata wakifukuzwa bara mbona sehemu nyingine nyingi tu wanaweza kukaa. Wao zaidi wanaangalia fursa za kipato. Na ndio maana wameenea sehemu nyingi duniani Sio huko bara tu.

Halafu, kuhusu makaazi mbona watu wa tanganyika pia ni wengi sana zanzibar.

Yaani ni wengi haswa.
 
Yani hili suala nilikuwa nazungmza na mzee leo asubuhi mimi ni mpemba tena wa chake chake kabisa lakini kuna baadhi ya wazanzibar wenzetu mna roho mbaya sana za kibaguzi hamfai sjui mngekuwa waarabu ingekuwaje
Wewe mpemba wa chake chake ya wapi?

Tibirizi au macho mane!!? [emoji23]
 

Ili hoja iwe dhaifu inatakiwa kupingwa kwa hoja yenye mashiko, Haiwezekani kung'ang'ania kuwa lazima Zanzibar kulikua na waafrica eti tu kwa sababu Zanzibar ipo Eneo la Africa bila ya ushahidi wowote.
Sasa mbona hawatafutwi waafirica asili wa Libya? napo si Africa ?

Na Kivovote vile, haya hayana mahusiono na chochote kinachoendelea sasa Zanzibar.
 
Mkuu, kutokuwepo na ushahidi wa maandishi sio sababu ya kuhitimisha kwamba yaliyopo ndiyo sahihi.

Na ushahidi hauonyeshwi kwa kuwaonyesha hao watu moja kwa moja, siyo lazima. Imekwishawekwa humu, tena kwenye mada hihii nadhani, kwamba uchunguzi umeonyesha uwepo wa watu Zanzibar kabla ya ujio wa Waarabu.
Na waarabu inajulikana wazi kwamba sio wao watu wa mwanzo kufika hapa; kwa hiyo hayo ya kung'ang'ania kuwa Zanzibar hawakuwepo watu hilo sio kweli, ila ni historia tu iliyowekwa kuhalalisha uvamizi wa eneo hilo.

Libya hawakuwepo watu wa asili pale? Sijui?
Na Egypt, hayo magofu yanayofukuliwa kila mwaka, haionyeshi kwamba watu walikuwepo pale?
 
Sasa mbona hawatafutwi waafirica asili wa Libya? napo si Africa ?
Mkuu, eneo la Libya kamwe huwezi kulilinganisha na eneo ilipo Zanzibar ili kuhalalisha uwepo wa waarabu Zanzibar, na kutokuwepo kwa waafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…