Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Mkuu labda aje raisi kichaa, ila serikali haihami Dar, sio leo wala kesho, itafungua makao makuu Dodoma, ila shughuli zile zile na huduma zile zile za makao makuu zitapatikana Dar, yan et siku serikali iseme pale magogoni raisi hatakaa tena pafungwe 😂 hapana aiseee

Kuhusu balozi za kimataifa, hizi wanaamua wao wakae wapi, na sidhani kuna balozi itaenda ikajitese kukaa Dodoma iache Dar,

Dar itapungua nguvu ya ushawishi sawa ila bado itakuwa kinara hapa Tz kwa miaka mingi sana ijayo,
Serikali kufanya mkoa wa pwani kuwa mkoa wa kiviwanda hio ndio ilipiga muhuri kuwa Dar haitafuta utawala wake kwa miaka mingi sana ijayo,
Huyo rais kichaa ndio magufuli sasa maana kayafanya ambayo watangulizi wake walisita kuyafanya .

Ukitaka kuamini ingia YouTube uuangalie mji wa kiserikali ulipofikia. Ni kichaa Tu ndio hataamini kuwa serikali inahamia dodoma

Halafu mnaongelea watu kuteseka dodoma kwa sababu ni pakame. Kuna miji mingapi duniani ni mikubwa na ya kijangwa Kabsaa na hizo balozi zing'ang'ane na dar wakati nchi inaendeshwa dodoma si utakuwa ni uwenda wazimu

By the way hakuna mkoa watu wanaishi kwa tabu kama dar, kuanzia joto, foleni na makazi yasiyopangiliwa. Shaghala bagala, kitu ambacho dom hakitokuja kutokea
 
Wanavyosema hizo bandari kavu (ICDs) sijui zitafanya bandari ya Dar idolole utafikiri hiyo mizigo itakuwa inashushwa kwenye hizo ICDs na ndege

ICDs zikiongezeka basi wajue na bandari ya Dar ina maana itakuwa busy zaidi
Kinachozungumziwa hapa ni sehem ya mapato ya bandar ya dar yatatozwa kwenye hizo bandari kavu incase isiwe hivyo.Ila mizigo ya kanda ya ziwa ikitozwa kodi ISAKA NA FELA basi ujue mamlaka za hayo maeneo zitaongeza mapato yao tufauti na sas kodi ya mizigo yote hutozwa bandarini hapo dar.

NOTE:Ukuaji wa dar upo kwenye jitihada za mikoa mingne,siku serikal ikiacha habari za mwaka 60 basi dar itapata ushindani mkubwa sana wa kiuchumi.

Sehem ya mapato ya utalii kanda ya ziwa na kaskazini yanaenda dar.
Sehem ya mapato ya sangara na sato kanda ya ziwa yanaenda dar
Sehem ya mapato ya migodi ya kanda ya ziwa,kaskazini na southern highlands yanaennda dar.
Mizigo yote nchi karibia 90% inapitia dar..hii mizigo ipo ya kanda ya ziwa,kaskazini,kusini,magaribi,kati n.k ila mapato yanatozwa dar pekee.

Dar ni kama baba mweny nyumba na mikoa mingne ni kama wapangaji.Linapokuja swala la nani anahela nyinyi na kodi basi baba mweny nyumba(DAR) atakuwa kinara na kupitia hio pesa ataboresha nyumba yake kisha ataonekana tajiri kumbe kuna wapangaji(MIKOA MINGINE)ni tajir kuliko yeye.

MWANZA inagdp ya zaid ya 11T huku dar inagdp 25T mara mbili ya GDP ya mwanza ila ukija kwenye mapato ya TRA Mwanza ni 200+B huku dar ni zaidi ya 15+T...yani zaidi ya mara 75 .HII NI HUMAN MADE ERROR

MBEYA yenyew GDP ni 9+T ila mapato ya TRA ni hata 100B hayafiki
 
Na hapa ndipo tunaongelea miaka mingi ijayo

Tuulize sisi tuliokulia mikoani enzi hizo, mtu ukiskia dar unatetemeka ila siku hizi vitu vilivyo dar, hata mikoani kwa kiasi chake vipo

Na hilo la watu kuivumilia Dar ni kwa sababu kulikuwa hakuna alternative.

chuo kikubwa kipo dar, huduma za kiafya za uhakika "Dar", embassies zote "dar", serikali "Dar", viwanja vya michezo "dar", huduma za mizigo "Dar", HQ za makampuni makubwa hata kama shughuli zake mikoani ila zipo "Dar"

Fikiria vinaanza kuondoka kimoja baada ya kingine, sasa fikiria ikifika siku almost 70% ya vyote viwe dom. Unadhani Dar itabakia kuwa "Dar" Kwenye nchi hii
Kweli mkuu lakin kuna vitu haviwez kuondoka, kama kariakoo, JNIA, bandari and the likes…
 
Watu wanavyosema Dar unadhani hakuna biashara mpya zinazaliwa Dar au wanadhani dar itasimama kuiacha hio mikoa ije,
Dar itaendelea kuwa commercial hub kwa miaka mingi ijayo hilo lipo wazi ..

Lakini pia hiyo ni Hollywood ya Tanzania maana shughuli kubwa za kimichezo na kiburudani zipo Dar kitu ambacho hakibadiliki leo ama kesho unless utokee mji mwingie wenye mamilioni ya watu.

Ila kwenye kupungua makali, tayari ishapunguzwa kutokana na urbanization ya mikoa mingine. Na itazidi kupungua siku hadi siku
 
Kweli mkuu lakin kuna vitu haviwez kuondoka, kama kariakoo, JNIA, bandari and the likes…
True, kariakoo haiondoki lakini kuna lile eneo la stand ya ubungo wa zamani kinashushwa commercial market ingine tena ya kisasa kuliko kariakoo. Kwa hivyo unaona tu kuwa bado serikali inapaendeleza dar kuendelea kuwa mkoa wa kibiashara.

Kuhusu uwanja wa ndege ni kwa sababu viwanja vingine vimefubazwa kiasi hazina international activities za maana. Fikiria Kiwanja cha Mwanza kimedumazwa miaka mingi, yani wakaona waendeleze songwe kuliko kumalizia mwanza. Sasa fikiria Mwanza na msalato vaanee kupokea international flights wakati serikali ipo dom, nani ataenda Dar mkuu

So, ni suala la muda tu japo hatujui ni lini, yawezekana ni 30 to 80 years to come 😁😁
 
Fact sheet ya Dar kubwa sana....98% mapato yoooote Tanzania yanatola Dar....labda 500 yrs to come sio saaaa
Hio 80+ ni pamoja na mapato ya mikoa mingne. Kampuni za migodi zinalipa kodi dar so ni swala mda kila kitu kitajifix.

Wew ujiulizi GDP ya dar ni 25+T inachangia 14%ya gdp ya nchi 77B $ huku mkoa inaofata ni 11+T
 
Wachambuzi wengine bwana, hivi aliyekuambia Dar kutokuwa tena mji mkuu kunaathiri uchumi wake au wa Tanzania ni nani? Dar ni jiji la biashara na litabaki kuwa hivyo hivyo hata iweje au hata Dodoma ifanane na Dar haiwezi kuipiku Dar.
 
Hata Washington na Beijing ni miji ya kiserikali, diplomats, international NGOs na mashirika makubwa duniani yako humo yanaoperate

Lakini GDP za majiji hayo haijaifikia California au Shanghai miji ya kibiashara
Exactly hazilingani kiuchumi lakini ni majiji yenye hadhi yake.

Mfano mwingine ni jo'burg, Durban and Pretoria

Kitu ambacho ni tofauti na huku ambapo dar ni kama lonely city maana serikali iliwekeza kila kitu katika mji mmoja.

Yaani chukua Dar na Dodoma ya 2010. Zilikuwa ni mbingu na ardhi ila kwa sasa kidogo Dom inaanza kupata ile hadhi inayostahili lakini wakati hili linafanyika. Lazma Dar ipungue influence

"Sijasema Dom itaipita Dar hivi karibuni kwa sababu bado imeipiga gap kubwa sana ila influence yake itapunguzwa kwa kiasi kikubwa"

"Zile zama za mtu akifikiria jambo lolote anaiona Dar, zinaisha ".hapa ndo point yangu kubwa ilipo mkuu
 
True, kariakoo haiondoki lakini kuna lile eneo la stand ya ubungo wa zamani kinashushwa commercial market ingine tena ya kisasa kuliko kariakoo. Kwa hivyo unaona tu kuwa bado serikali inapaendeleza dar kuendelea kuwa mkoa wa kibiashara.

Kuhusu uwanja wa ndege ni kwa sababu viwanja vingine vimefubazwa kiasi hazina international activities za maana. Fikiria Kiwanja cha Mwanza kimedumazwa miaka mingi, yani wakaona waendeleze songwe kuliko kumalizia mwanza. Sasa fikiria Mwanza na msalato vaanee kupokea international flights wakati serikali ipo dom, nani ataenda Dar mkuu

So, ni suala la muda tu japo hatujui ni lini, yawezekana ni 30 to 80 years to come 😁😁
80 years to come we will all be doomed hapo hakuna tatizo, ndio napita hapa ubungo stand ya zamani …KUDOS.
 
Kweli mkuu lakin kuna vitu haviwez kuondoka, kama kariakoo, JNIA, bandari and the likes…
We jamaa mbishi kinoma Kuna hayo maeneo mawili ujenzi wa bandari kavu makambako soko la kimataifa makambako na bandari ya mtwara reli ya mtwara mbambay na bandari ya mbambabay. Hapo ni Kwamba hakuna mfanyabiashara wa Zambia au wa congo au malawi ataenda karikoo. Na ninavyoongea hivi soko la mazao la kimataifa lipo tayari makambako.
 
Kinachozungumziwa hapa ni sehem ya mapato ya bandar ya dar yatatozwa kwenye hizo bandari kavu incase isiwe hivyo.Ila mizigo ya kanda ya ziwa ikitozwa kodi ISAKA NA FELA basi ujue mamlaka za hayo maeneo zitaongeza mapato yao tufauti na sas kodi ya mizigo yote hutozwa bandarini hapo dar.

NOTE:Ukuaji wa dar upo kwenye jitihada za mikoa mingne,siku serikal ikiacha habari za mwaka 60 basi dar itapata ushindani mkubwa sana wa kiuchumi.

Sehem ya mapato ya utalii kanda ya ziwa na kaskazini yanaenda dar.
Sehem ya mapato ya sangara na sato kanda ya ziwa yanaenda dar
Sehem ya mapato ya migodi ya kanda ya ziwa,kaskazini na southern highlands yanaennda dar.
Mizigo yote nchi karibia 90% inapitia dar..hii mizigo ipo ya kanda ya ziwa,kaskazini,kusini,magaribi,kati n.k ila mapato yanatozwa dar pekee.

Dar ni kama baba mweny nyumba na mikoa mingne ni kama wapangaji.Linapokuja swala la nani anahela nyinyi na kodi basi baba mweny nyumba(DAR) atakuwa kinara na kupitia hio pesa ataboresha nyumba yake kisha ataonekana tajiri kumbe kuna wapangaji(MIKOA MINGINE)ni tajir kuliko yeye.

MWANZA inagdp ya zaid ya 11T huku dar inagdp 25T mara mbili ya GDP ya mwanza ila ukija kwenye mapato ya TRA Mwanza ni 200+B huku dar ni zaidi ya 15+T...yani zaidi ya mara 75 .HII NI HUMAN MADE ERROR

MBEYA yenyew GDP ni 9+T ila mapato ya TRA ni hata 100B hayafiki

Watu hawalioni hili mkuu kwa sababu wana perception ya dar ndio Tanzania 😁😁

Kwa hiyo ukiwapa facts zingine ni lazma wapinge ila issue ipo wazi. Dar imekuzwa kwa serikali kufanya centralization ya shughuli zake zote lakini pia kudumaza maendeleo ya sehemu zingine. Imagine tuna bandari tatu lakini watu wote jicho lilikuwa dar

Hii situation utasema Dar ina strategic location au serikali ilitengeneza mazingira ya watu kuitumia Dar, zaidi
 
We jamaa mbishi kinoma Kuna hayo maeneo mawili ujenzi wa bandari kavu makambako soko la kimataifa makambako na bandari ya mtwara reli ya mtwara mbambay na bandari ya mbambabay. Hapo ni Kwamba hakuna mfanyabiashara wa Zambia au wa congo au malawi ataenda karikoo. Na ninavyoongea hivi soko la mazao la kimataifa lipo tayari makambako.
Mkuu ivi kweli unasikiliza story za wanaccm aisee kwamba hivyo vitu vitaota kama uyoga kama umeme tu nchi hii ni tatizo ? Bro kimaandish yapo very very good ila kiutekelezaji ni tatizo kubwa sana, they are trying to contain you guys until you get them back into the white house, ndio wanavyofanyaga mkuu. Usikubali kuwa brainwashed kirahis hivyo mzee, i dont trust these people at all…Haya unayoyasema ni stori tu za wanasiasa ila nnachokisema mimi ni kitu kina tangible evidence man. Jaribu hata kurelate kidogo mkuu
 
Back
Top Bottom