Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Huyo rais kichaa ndio magufuli sasa maana kayafanya ambayo watangulizi wake walisita kuyafanya .Mkuu labda aje raisi kichaa, ila serikali haihami Dar, sio leo wala kesho, itafungua makao makuu Dodoma, ila shughuli zile zile na huduma zile zile za makao makuu zitapatikana Dar, yan et siku serikali iseme pale magogoni raisi hatakaa tena pafungwe 😂 hapana aiseee
Kuhusu balozi za kimataifa, hizi wanaamua wao wakae wapi, na sidhani kuna balozi itaenda ikajitese kukaa Dodoma iache Dar,
Dar itapungua nguvu ya ushawishi sawa ila bado itakuwa kinara hapa Tz kwa miaka mingi sana ijayo,
Serikali kufanya mkoa wa pwani kuwa mkoa wa kiviwanda hio ndio ilipiga muhuri kuwa Dar haitafuta utawala wake kwa miaka mingi sana ijayo,
Ukitaka kuamini ingia YouTube uuangalie mji wa kiserikali ulipofikia. Ni kichaa Tu ndio hataamini kuwa serikali inahamia dodoma
Halafu mnaongelea watu kuteseka dodoma kwa sababu ni pakame. Kuna miji mingapi duniani ni mikubwa na ya kijangwa Kabsaa na hizo balozi zing'ang'ane na dar wakati nchi inaendeshwa dodoma si utakuwa ni uwenda wazimu
By the way hakuna mkoa watu wanaishi kwa tabu kama dar, kuanzia joto, foleni na makazi yasiyopangiliwa. Shaghala bagala, kitu ambacho dom hakitokuja kutokea