ZANU PF chama kongwe cha siasa nchini Zimbabwe chini ya Robert Gabriel Mugabe, kwa makusudi kiliamua kufuata nafasi za makamu mwenyekiti na katibu mkuu wa chama cha ZANU PF ili mwenyekiti avae kofia hizo mbili za wasaidizi wake waliokuwa na nguvu kisiasa kama colonel mstaafu Abdulrahaman Kinana na sasa pengine secretary general Dr. Emmanuel Nchimbi.
Imechukua muda kupata mrithi wa Abdulrahman Omar Kinana hivyo chama kongwe dola CCM kina ogopa nini kufanya uteuzi wa makamu mwenyekiti wa CCM bara au ndiyo wanafuata njia ya ZANU PF kama mchambuzi nguli wa siasa za vyama kongwe dola mzimbabwe anayo dadavua kete za kisiasa zinavyosogezwa ktk ubao wa mchezo wa bao la kisiasa ...
View: https://m.youtube.com/watch?v=taHHsbP_RXATusikilize mchambuzi wa siasa za Zimbabwe akielezea jinsi mwenyekiti wa chama dola kongwe ZANU PF alipoamua kufuta vyeo vya makamu mwenyekiti wa chama na pia kufuta nafasi ya katibu mkuu wa chama ili rais wa nchi na mwenyekiti wa chama kujivisha vyeo hivyo vyote kujiongezea nguvu maradufu za kimaamuzi ... kuwaondoa aina ya wanasiasa wa CCM unaoweza kuwaita kina "
John Rambo" wa kisiasa aina ya Abdulrahman Kinana January Makamba, Nape Nnauye ...
Mchambuzi huyu mzimbabwe mahiri wa kumulika tamaduni za vyama dola kongwe anasema huko Russia ya Stalin na Russia ya Vladimir Putin, China n.k kulipo na vyama kama vya ZANU PF na CCM mtindo huu wa ku consolidate power yaani kujirudikia vyeo vingi mtawala mkuu ni njia ya kupeleka ujumbe nani ni bosi mkuu .
Na panga pangua kupitia mikeka ya teuzi kila usiku mara kwa mara ni njia mojawapo ya kupunguza fukuto la ndani kwa ndani ya chama na serikali yake ambapo asipopitisha chekeche lake linaloweza kumpunguzia muonekano ya kukosa nguvu na ushawishi wa kuendelea kuwa kiongozi mkuu ... nguli mchambuzi anaongeza ....