PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Habari za Leo tena, karibu katika jamvi la story of change, jukwaa linaloibua mawazo mapya. Leo katika Uzi wangu huu, nataka wadau wote kutoka katika sector zote, tusaidie wadau na wanazuoni wanaotafuta titles za kufanyia research ambazo bado hazijawahi kufanyiwa kazi kabisa, naomba tuwe watulivu kabla ya kupost hizo titles ili unapoweka title iwe productive kwa ajili ya jamii zetu na taifa kwa ujumla. Pia niwaombe moderators wa Jforum, kuipin hii thread ili iwe accessable muda wote na wadau wote wanaotafuta titles kwa ajili ya kufanyia utafiti/research. Karibuni sana . Mimi nitaanza na hizi
Hizi ni ideas zangu, zipo titles nyingi sana, naomba tuandike kwa faida ya wadau mbalimbali wa tafiti
Karibuni sana 🙏🙏
- Vyakula vyenye athali kwenye mwili wa binadamu hususani afya ya akili
- koo zenye mafanikio makubwa Tanzania na Siri za mafanikio Yao
- Idadi ya watoto na watu wazima wenye akili kubwa zaidi Tanzania
- Ufugaji wa wadudu, faida na changamoto zake.
- Biashara ya vitu chakavu, faida na changamoto zake katika jamii
- Ufanisi wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania
- Mitandao ya simu inavyoathili shughuli za maendeleo katika jamii
- Kukati kwa umeme na athali zake katika ukuaji wa maendeleo katika jamii
- Alama za taifa zinavyochochea maendeleo katika uchumi wa taifa
- Historia ya Tanzania inavyochagiza maendeleo ya taifa
- Athali ya mabadiliko ya Khali ya hewa kwenye maeneo yaliyosifika zaidi kiuzalishaji wa mazao nchini Tanzania
- Idadi ya nchi rafiki zinazofaa kwa watanzania kwenda kuishi kwa ajili ya kufanya biashara na shughuli zingine za kimaendeleo
- Vazi linalopendwa zaidi na watanzania kama alama ya vazi la taifa
- Michezo isiyopewa kipaumbele, faida na hasala zake kuzishiriki
- Orodha ya biashara nzuri na ngumu kwenye kuchochea maendeleo ya jamii
- Faida na athali za Vijana katika taifa kujishughulisha na michezo ya kubahatisha na kamali
- Orodha ya ndoa zilizodumu zaidi Tanzania, Siri na changamoto walizopitia wanandoa hao
- Orodha ya milima yenye urefu mkubwa kwa Kila mkoa na wilaya
Hizi ni ideas zangu, zipo titles nyingi sana, naomba tuandike kwa faida ya wadau mbalimbali wa tafiti
Karibuni sana 🙏🙏
Upvote
2