Hizi mboga na nafaka kiingereza chake ni kipi?

Hizi mboga na nafaka kiingereza chake ni kipi?

Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu Trubetzkoy

Mimi siyo MUHA.

Kule Kanda Ya Ziwa, Neno, "NYANYANTOLE" au "MATOLE" linatumika zaidi kuliko, "NYANYAMSHUMAA" au "NYANYACHUNGU".

Nimetumia neno hilo hili kuwakwepa wana comedian wa, "Mr Katelephone don't smoke my river".

Sijui kama dhamira yangu imeeleweka mpaka hapo.
 
mada tamu saaaana hii
mimi pia ua nataman saana kujua dengu inaitwaaje kwa kingereza
Shukrani sana mkuu,

Kuhusu "DENGU" jibu lake limetolewa katika kurasa ya 1 na ya pili.

Pitia page ya 1 na ya 2 utaliona jibu lake.
 
Mlenda= Jutemallow
Bamia= Okra
Nyanyamshumaa= African eggplant
Mchicha= Amaranth
Kunde= Cowpea
Mbaazi= Pegionpea
Dengu= Lentil
Majani ya kunde= Cowpea leaves
Matembele= Sweet potato leaves
Biringanya= Eggplant
Figiri= Ethiopian Mustard
Choroko= Greengram/Mungbean
Hoho= Sweet pepper


Wewe ni chef au???
 
SUA walipaswa watuwekee hayo mavitu kwenye goggle lakini wapiii?!

SUA bana!
Ni kweli mkuu Akilinjema

Vyuo vyetu vya kilimo, BAKITA, TUKI, na Taasisi nyingine za umma kama WIZARA YA KILIMO wana kitu cha kufanya ili kuzidi kuiboresha Lugha yetu Ya Taifa pale SWAHILI PEDIA (ENCYCLOPEDIA), GOOGLE SWAHILI, WIKI SWAHILI.

Yaani tuko nyuma sana katika ukuzaji na uhariri wa Lugha yetu ya Taifa kwa njia ya mtandao.

Hata hariri na rejea pale
https//sw.m.wikipedia.org/wiki/Kiswahili
haziwekwi wala kurejewa kwa wakati.
 
Mkuu pleo wakati nikivinjari vinjari mtandaoni nikaona "LETTUCE", Ikiwa katika tafsiri ya Kiswahili, kwa neno, "SALADI"

Mahali penyewe ni www.spokenswahili.com
Saladi nahisi kwa haraka ni jina lililotoholewa kujenga picha Ila kwa ninachojua "MCHUNGA" ni jina halisi la kiswahili ambalo pia baadhi ya makabila wanalitumia.

Mmea huu asili yake ni pwani ya Afrika mashariki.....
Mmea unaofanana na huu ambao unaweza kupatikana kwenye Kanda nyingine za kiikolojia unafahamika kama Wild lettuce Ila botanical name ni tofauti na Mchunga japo yote Ina sifa ya kutumika kama chakula na dawa kwa pamoja.
 
naomba kufahamishwa mboga inayoitwa MGAGANI inatumiika saaana mikoa ya kanda ya ziiwa ,na maeneo ya mikoa jirani na zambia kama vile RUKWA.
 
Back
Top Bottom