Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Jana Rais Samia kutoa milioni 700 kwa Taifa Stars baada ya kufuzu AFCON 2025 kama pongezi kwa kuliheshimisha taifa kufuzi mara ya nne katika fainali hizo. Je, zawadi hii inawahusu wachezaji waliocheza mechi za mwisho dhidi ya Ethiopia na Guinea pekee, au inajumuisha wachezaji wote waliowahi kushiriki hatua ya makundi?
Pia, Soma:
+ Rais Samia aipa Taifa Stars Milioni 700 kufuzu AFCON
+ Full Time: Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024
Tunakumbuka mwaka 2019, Taifa Stars ilifanikisha kufuzu kwa AFCON baada ya kuifunga Uganda 3-0. Kama sehemu ya pongezi kwa mafanikio hayo, Rais wa wakati huo, hayati John Magufuli, aliwazawadia wachezaji viwanja huko Dodoma. Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Taifa Stars, Paul Makonda, pia aliahidi Tsh milioni 10 kwa kila mchezaji wakati huo.
Hata hivyo, Nahodha Mbwana Samatta alisimama kidete kuwakumbusha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu mchango wa wachezaji walioumia katika majukumu ya kitaifa. Alitoa mfano wa Shomari Kapombe, ambaye aliumia wakati akiitumikia Stars lakini alionekana kusahaulika wakati wa mgao huo wa zawadi.
Sasa, tunapozungumzia zawadi ya milioni 700 kutoka kwa Rais Samia, mgao wake ukoje. Je, wapate Wachezaji wa kikosi cha mwisho kuitwa na kupambana dhidi ya Ethiopia na Guinea nakuvuna alama 6 muhimu ambazo zimechangia kufuzu kwa AFCON 2025?. Lakini je, wachezaji waliokuwa sehemu ya hatua ya makundi, hata kama hawakuitwa kwenye mechi za mwisho, hawastahili kutambuliwa?.