Hizi ndio bei za mbolea ambazo wakulima watanunulia kuanzia Agosti 15, 2022 baada ya bilioni 150

Hizi ndio bei za mbolea ambazo wakulima watanunulia kuanzia Agosti 15, 2022 baada ya bilioni 150

Utashangaa kiukweli hii inaonyesha ni Kwa namna gani serikali inawasikiliza watu wake hasa katika kuhakikisha inawapunguzia makali wakulima kutokana na hali ya kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia si Tanzania pekee bali ni ulimwenguni kote. Zipo sababu kadhaa zilizosababisha bei kupanda ikiwemo ugonjwa wa Covid-19 na mgogoro unaondelea kati ya Ukraine na Russia ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji na upatikanaji wa mbolea.

Kwa jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wakulima wa Tanzania sasa watanunua mbolea hizo kwa bei nafuu licha ya yote yanayoendelea ili tu isiathiri msimu wa kilimo na pia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

AINA ZA MBOLEA NA BEI ZAKE
1. DAP ingeuzwa sh 131,676 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 61676.

2. UREA ingeuzwa sh 124,734 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 54,734.

3. CAN ingeuzwa sh 108,256 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 60,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 48,156.

4. SA ingeuzwa sh 82,852 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 50,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 32,852.

5. NPK's ingeuzwa sh 122,695 bila ruzuku lakini sasa itauzwa sh 70,000 ambapo ruzuku ya serikali ni sh 52,695.​
Mbona sioni mbolea yA minjingu kwenye orodha ?
 
CCM imeshatufanya watanzania wote wajinga. Mbolea ilikuwa inauzwa elfu 50,000 wakapandisha mpaka 130,000. wanajifanya kushusha mpaka 70,000 na sisi kwa uzuzu tunashangilia
 
Aliyepandisha bei nani? Nipandishe mimi nishushe mwenyewe
Ndo kuupiga mwingi?
Ndugu zangu naomba mnitajie bolea inayofaa kwa kilimo Cha mpunga ktk hatua zote had mavuno nataka ninunue saiv niweke stoo kuepusha kukutana na wimbi la mbolea kupanda Tena! Pia naomba ushauri km mbolea za maji mfano super gro km inafaa kw kilimo Cha mpunga
 
Back
Top Bottom