Hizi ndio Jamii tajiri zaidi Tanzania?

Hizi ndio Jamii tajiri zaidi Tanzania?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,850
Reaction score
6,030
Tanzania ni nchi kubwa , na yenye Jamii nyingi za asili mbalimbali, Lakini kiuhalisia kutokana na mambo ya historia na maeneo zilizopo jamii hizo imesababisha baadhi ya jamii kuwa na uwezo mkubwa kifedha kuliko jamii Nyingine.

Kwa miaka Mingi tokea uhuru jamii za Wahindi na waarabu zimeendelea kushikilia uchumi wa Tanzania kwakuwa ndio Jamii tajiri kabisa Tanzania, Hii ni kutokana na asili ya nchi wanazotoka na upendeleo wa serikali umekuwa ukiwanufaisha sana, japo wengi walihamia wakiwa na kiasi fulani cha utajiri , hivyo wamekiongeza,

Kwa Jamii za Kibantu, Ni muda mrefu jamii ya Wakinga na Wachaga imekuwa ikitengeneza jina na utajiri mkubwa, huku sababu kubwa zikiwa ni za kihistoria mfano kilimanjaro Wakoloni walisomesha sana wachaga, na waliweka biashara ya utalii kanda ya kaskazini kitovu cha utajiri, kwa wakinga wa Njombe/Iringa pia sababu za kihistoria zinawabeba.

Lakini pia kuna Jamii ya wachapakazi , ambayo ni jamii ya Kisukuma, hawa sasa wamekuwa moja kati ya makabila tajiri kabisa Tanzania, huku wengi wakiwa wamewekeza katika mikoa mbalimbali hadi Kariakoo, Sukuma ndio kabila lenye idadi kubwa ya watu Tanzania takribani Robo 1/4 ya watanzania wote ni Wasukuma, Kwa sasa nadiriki kusema Kabila la wasukuma limeshapiku Tayari wachaga na wakinga, huku biashara zao kubwa ni Madini, biashara na kilimo.

Hivyo kwa Sasa hizi ndo Jamii Tano tajiri kabisa Tanzania:

1. Waarabu
2. Wahindi
3. Wakinga
4.Wasukuma
5. Wachaga

Katika orodha hii hakuna Wagogo , wahaya , wala Wazaramo,
 
Wewe fact yako ikowapi kuonyesha hakuna anaewakaribia wachaga?

Mtoa mada hajatoa facts, katoa maoni yake. Nami nimetoa maoni. Sasa akija upande wa facts ndipo nami nitakuletea facts tena za kutosha kuhusu nchi hii kabila la wachaga ni kivipi linaongoza kiuchumi hapa Tanzania.

Kuanzia matajiri wakubwa mpakq level ya mtu mmoja mmoja.
 
Tanzania ni nchi kubwa , na yenye Jamii nyingi za asili mbalimbali, Lakini kiuhalisia kutokana na mambo ya historia na maeneo zilizopo jamii hizo imesababisha baadhi ya jamii kuwa na uwezo mkubwa kifedha kuliko jamii Nyingine, Kwa miaka Mingi tokea uhuru jamii za Wahindi na waarabu zimeendelea kushikilia uchumi wa Tanzania kwakuwa ndio Jamii tajiri kabisa Tanzania, Hii ni kutokana na asili ya nchi wanazotoka na upendeleo wa serikali umekuwa ukiwanufaisha sana, japo wengi walihamia wakiwa na kiasi fulani cha utajiri , hivyo wamekiongeza,

Kwa Jamii za Kibantu, Ni muda mrefu jamii ya Wakinga na Wachaga imekuwa ikitengeneza jina na utajiri mkubwa, huku sababu kubwa zikiwa ni za kihistoria mfano kilimanjaro Wakoloni walisomesha sana wachaga, na waliweka biashara ya utalii kanda ya kaskazini kitovu cha utajiri, kwa wakinga wa Njombe/Iringa pia sababu za kihistoria zinawabeba.
Lakini pia kuna Jamii ya wachapakazi , ambayo ni jamii ya Kisukuma, hawa sasa wamekuwa moja kati ya makabila tajiri kabisa Tanzania, huku wengi wakiwa wamewekeza katika mikoa mbalimbali hadi Kariakoo, Sukuma ndio kabila lenye idadi kubwa ya watu Tanzania takribani Robo 1/4 ya watanzania wote ni Wasukuma, Kwa sasa nadiriki kusema Kabila la wasukuma limeshapiku Tayari wachaga na wakinga, huku biashara zao kubwa ni Madini, biashara na kilimo.

Hivyo kwa Sasa hizi ndo Jamii Tano tajiri kabisa Tanzania ,
1. Waarabu
2. Wahindi
3. Wakinga
4.Wasukuma
5. Wachaga

Katika orodha hii hakuna Wagogo , wahaya , wala Wazaramo,
"Ukiwaondoa wahindi na waarabu ,waswahili wenye pesa ni wa kuwahesabu halafu weekend angalia nyendo zao kuchukua wake za watu na kufanya mambo nje ya uwezo wao" - Wagosi wa kaya.
 
Kwa jamii za kibantu sioni jamii yoyote ikisogelea hata theluthi kwa wachaga,😂 Mabasi ya mikoani mengi ukiachana na waarabu wao ndo wamejaa, Usafiri wa ndege wapo, 5 star hotels, Biashara ya usafiri kwa Dar hizi Daladala wengi ni wachaga mtu moja anamiliki hadi daladala 50, real estate, Kampuni nyingi za utalii mmiliki mtalii moja tu akija analipia hadi milioni 30, na hata hapo Kariakoo utawakuta walioanza game kitambo wana majengo kibao tu. Ukimalizana na hapo kafuatilie pale soko la Hisa DSE utawakuta,

Halafu hebu twende maendeleo ya vijijini kwao sasa, kuna maendeleo vijijini huwezi kufananisha hata kidogo na Kasulu, Makete, Gamoshi, Tukuyu, Tarime, Muleba, Simanjiro, n.k.

Ukimalizana na hapo wachaga Elimu imewajaza kwenye taasisi ambazo ni moyo wa fedha zat taifa, wamejaa mno TRA, BOT, n.k.

Daraja la kwanza Wanaoshikilia uchumi wa hii nchi ni Wahindi kama kina Mo, Waarabu kama kina Bakhresa, Waajemi kama kina Rostam, hao ni levels nyingine kabisa waliotawala top 30 ya matajiri nchini, Sioni wa kuwasogelea hata chembe. Daraja la pili ni Wachaga hawa ndio wawakilishi wa makabila ya asili wapo sekta mbalimbali, Daraja la tatu ni Waha, Wakinga, Wasukuma wengi wao hufanya biashara za uchuuzi, kilimo na madini. Daraja la nne ni Wahaya, Wanyakyusa, Wakurya, Wapare, n.k. hawa wengi wamefanikiwa kupitia ajira
 
Back
Top Bottom