Tanzania ni nchi kubwa , na yenye Jamii nyingi za asili mbalimbali, Lakini kiuhalisia kutokana na mambo ya historia na maeneo zilizopo jamii hizo imesababisha baadhi ya jamii kuwa na uwezo mkubwa kifedha kuliko jamii Nyingine.
Kwa miaka Mingi tokea uhuru jamii za Wahindi na waarabu zimeendelea kushikilia uchumi wa Tanzania kwakuwa ndio Jamii tajiri kabisa Tanzania, Hii ni kutokana na asili ya nchi wanazotoka na upendeleo wa serikali umekuwa ukiwanufaisha sana, japo wengi walihamia wakiwa na kiasi fulani cha utajiri , hivyo wamekiongeza,
Kwa Jamii za Kibantu, Ni muda mrefu jamii ya Wakinga na Wachaga imekuwa ikitengeneza jina na utajiri mkubwa, huku sababu kubwa zikiwa ni za kihistoria mfano kilimanjaro Wakoloni walisomesha sana wachaga, na waliweka biashara ya utalii kanda ya kaskazini kitovu cha utajiri, kwa wakinga wa Njombe/Iringa pia sababu za kihistoria zinawabeba.
Lakini pia kuna Jamii ya wachapakazi , ambayo ni jamii ya Kisukuma, hawa sasa wamekuwa moja kati ya makabila tajiri kabisa Tanzania, huku wengi wakiwa wamewekeza katika mikoa mbalimbali hadi Kariakoo, Sukuma ndio kabila lenye idadi kubwa ya watu Tanzania takribani Robo 1/4 ya watanzania wote ni Wasukuma, Kwa sasa nadiriki kusema Kabila la wasukuma limeshapiku Tayari wachaga na wakinga, huku biashara zao kubwa ni Madini, biashara na kilimo.
Hivyo kwa Sasa hizi ndo Jamii Tano tajiri kabisa Tanzania:
1. Waarabu
2. Wahindi
3. Wakinga
4.Wasukuma
5. Wachaga
Katika orodha hii hakuna Wagogo , wahaya , wala Wazaramo,