Hizi ndio nchi 10 pekee Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya Serikali.

Hizi ndio nchi 10 pekee Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya Serikali.

Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
  1. Botswana
  2. Cape Verde
  3. Eritrea
  4. Mauritius
  5. Mozambique
  6. Namibia
  7. Sao Tome and Principe
  8. Senegal
  9. South Africa
  10. Tanzania
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
hapo ni uchu wa madaraka tu, na hakuna demokrasia yeyote na woga kwa wananchi basi.
 
Nimekuambia katika mtazamo wa kisheria.
Huko kwingine unapokwenda sipatambui.
Nchi zote dunian zipo kisheria na siyo kihisia kama unavyomaanisha eti Tanzania ni Tanganyika wakati Tanganyika+Zanzibar=Tanzania.
Sheria ipi unaizungumzia maana hati ya muungano inasomeka "Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar'
 
Sheria ipi unaizungumzia maana hati ya muungano inasomeka "Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar'
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kwenye kesi ya Machano Hamis and Others vs SMZ.
Kwenye hiyo kesi Mahakama ilisema kwamba Zanzibar siyo dola, na kwamba dola la Zanzibar lilikufa rasmi April 26, 1964 pale Tanganyika na Zanzibar ilipoungana na kuzaa nchi mpya inaitwa Tanzania.
Hivyo hivyo, pia dola la Tanganyika lilikufa rasmi siku ambayo Zanzibar lilikufa.
Hizo hati unadai ni za Muungano haziwezi kuwa na authority kuishinda Katiba
 
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano was Tanzania.
Pia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kwenye kesi ya Machano Hamis and Others vs SMZ.
Kwenye hiyo kesi Mahakama ilisema kwamba Zanzibar siyo dola, na kwamba dola la Zanzibar lilikufa rasmi April 26, 1964 pale Tanganyika na Zanzibar ilipoungana na kuzaa nchi mpya inaitwa Tanzania.
Hivyo hivyo, pia dola la Tanganyika lilikufa rasmi siku ambayo Zanzibar lilikufa.
Hizo hati unadai ni za Muungano haziwezi kuwa na authority kuishinda Katiba
dah bush lawyer unasema constitution iko superior kwa Articles of Union umekula maharage ya wapi wewe!!??
 
dah bush lawyer unasema constitution iko superior kwa Articles of Union umekula maharage ya wapi wewe!!??

Maharage hayana uhusiano na taaluma yangu.

Hizo hati zenyewe zinazungumzia juu ya Muungano wa nchi mbili ambapo Tanzania imezaliwa.

Hata kama nchi ingeitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, still nchi ni moja tu!
 
Tanganyika ilikufaje wakati Zanzibar bado ipo,
Hapa ninazungumzia state, yaani dola; hakuna dola inaitwa Zanzibar, na hakuna dola inaitwa Tanganyika.
Sifa ya dola ni kuwa na:
1. Watu
2.Mipaka
3. Serikali
4. Uhuru ( wa kitaifa na kimataifa) yaani internal and external sovereignty.
Zanzibar ina watu, serikali, na mipaka ila haina UHURU wa kujiamulia mambo yake yenyewe kwa ukamilifu.
Kimataifa, Zanzibar haijulikani na haitambuliki kama dola huru, isipokuwa Tanzania ndiyo inatambulika na kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Zanzibar haina kiti UN. Haina uwezo kusaini baadhi ya mikataba ya kimataifa.
Uhuru wa ndani: Zanzibar haina Uhuru wa kulinda watu wake, isipokuwa, inategemea Tanzania.
Pia Zanzibar haina Uhuru wa kutunga na kusimamia sheria zake yenyewe.
Sharia zinatungwa na Bunge la Tanzania.
Kuhusu ulinzi, JWTZ ndiyo jeshi lenye dhamana ya ulinzi Zanzibar, na lipo chini ya Serikali ya Muungano.
Zanzibar is not a sovereign state, ONLY Tanzania is sovereign and Zanzibar is part of Tanzania.
Both Zanzibar and Tanganyika States died since 1964, April 26
 
Sababu kuu ziko Kama ifuatavyo Kuna nchi Zina utawala wa majimbo.Ambazo Zina nguvu kuliko serikali kuu kwenye Mambo mengi.Sasa upindue ili umpindue Nani uvamie Jimbo la mwingine au?
Mfano Ni south Afrika.

Pili Ni composition ya makabila mengi .Nchi zenye makabila makubwa machache makubwa kutwangana kwao kawaida.Nchi ikiwa na makabila mengi uasi unakuwa mgumu mno kuupanga .

Tatu uwepo wa utitiri wa dini nyingi zenye Imani tofauti tofauti.Kuna faida kubwa Sana nchi kuwa na dini nyingi na madhehebu mengi utitiri yenye Imani tofauti tofauti.Kupanga mapinduzi huwa Ni kugumu mno sababu ya tofauti kubwa za kiimani.Nchi mfano zenye dini moja au mbili tu mfano rahisi mno kupanga mapinduzi.nchi Kama somalia ,nchi Kama Rwanda iliwezekana sababu ya tatizo Hilo Hilo mauaji ya kimbari yalikuwa rahisi kupangwa ndani ya kanisa Katoliki sababu ndio wako majority ndio dini ya wanyarwanda wengi ukiunganisha na nch ihiyo kuwa na makabila makubwa mawili tu ya wahutu na watusi unaona kabisa ilivyo rahisi kufanya mapinduzi kwa kutumia muundo mbinu wa kanisa Katoliki au wa kikabila wa kitusi au kihutu.Ukiwa na dini nyingi zenye imani tofauti husaidia mfano waislamu wa siasa Kali wakilianzisha waislamu wenye msimamo wa wastani wanapinga,walokole wakilianzisha wakatoliki hawaungi mkono,wakatoliki wakilianzisha wasabato wanalikataa nk nk kwa hiyo amani inadhibitiwa kwa kuruhusu dini ziwe nyingi iwezekenavyo na zenye Imani tofauti tofauti.Hapa ndipo wanasiasa husema dini Zina mchango mkubwa katika amani ya nchi.Nchi zenye dini moja au mbili kubwa mapinduzi marahisi kuyapanga.Nchi za Latin America Ni moja ya mifano na nchi za kiarabu.Nchi Kama Iran nk .

Nne Tatizo la Ardhi huchangia Sana.Ajira kubwa kwa watu wengi Ni kwenye kilmo.Watu wanachohitaji kwanza Ni uhakika wa chakula.Sasa watu wengi Kama Ni vigumu kupata ardhi Vita yaweza fumuka na mapinduzi kirahisi.Mapinduzi ya Urusi yalitokea sababu ya ardhi kuhodhiwa na wachache na kuacha umati ukiwa hauna ardhi na haujui uishije.Tanzania watu walio wengi Wana uhakika wa chakula akishashiba karidhika hataki Shari.

Tano Ni sababu ya gharama za kuendesha mapinduzi.Wapinduaji huhitaji support kubwa ya fedha na vifaa vya kivita huo ni mtihani mkubwa.Hivyo unakuta Hakuna mwenye hamu ya mapinduzi.

Sita Ni aina ya watu walioko katika nchi.Kuna nchi unakuta watu wao Sio washari by nature mfano Tanzania majority Sio watu wa Shari na hawapendi Shari.Hivyo kupata uungwaji mkono ukianzisha Shari SI rahisi kupata support.Mfano mikoa ya Pwani ,mikoa ya katikati ya nchi makabila makubwa Kama wasukuma ,wanyamwezi,wanyakyusa ,wangoni,wamatengo,wafipa,waluguru,wapogoro,wazanzibari weusi. Hivyo mwanzisha mapinduzi lazima akwae kisiki kupata support Sio rahisi.

Saba Ni kiwango Cha mwamko wa kupenda madaraka na vyeo kwa raia na wanajeshi .Kuna wanajeshi na raia nchi unakuta kila Askari au raia mfano anaota kuwa genetali wa Jeshi.Sasa unakuta vikoplo aau raia vinapindua nchi kila kukicha vijipe vyeo vya generali au vishike nchi kwa mapinduzi .Tanzania mfano watu walio wengi hawako interested kabisa na vyeo vya kisiasa.Ni wachache ndio huvitolea macho

.Nane Ni kiwango cha kuridhika cha watu watu kuridhika na woichonacho.Wakishajiridhikia hawahitaji chochote.Kuna siku kiongozi mmoja wa Upinzani alipita mtaani alisema CCM kumejaa mafisadi CCM inabidi iondolewe madarakani.Kuna Wazee walikuwa wakicheza bao mmoja akamjibu hao mafisadi walichukua pesa ya mama yako? Yanakuhusu Nini? Wazee wengine wakaanza kuunga mkono kauli ya Mzee mwenzao na kusisitiza kumhoji hao mafisadi wamechukua pesa ya ya mama yako?.Wakamwambia Tuondokee hapa na porojo zako.Akaondoka mnyonge .Wazee wa watu wamejilia kipande Cha mhogo na fungu la dagaa la shilingi Mia mbili wameridhika zao!!! Kupindua nchi ya watu walioridhika na walichonacho Sio kazi rahisi.
Hiyo namba 8 ndio ujinga wa watanzania wengi ulipo! Ndo mana fisiem wanapenda ujinga huo coz wanautumia kama mtaji wao wa kisiasa
 
Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
  1. Botswana
  2. Cape Verde
  3. Eritrea
  4. Mauritius
  5. Mozambique
  6. Namibia
  7. Sao Tome and Principe
  8. Senegal
  9. South Africa
  10. Tanzania
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
Mara nyingi hutokana na watawala ambao wanaongoza bila kufuata sheria
 
Back
Top Bottom