Hizi ndio nchi 10 pekee Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya Serikali.

hapo ni uchu wa madaraka tu, na hakuna demokrasia yeyote na woga kwa wananchi basi.
 
Nimekuambia katika mtazamo wa kisheria.
Huko kwingine unapokwenda sipatambui.
Nchi zote dunian zipo kisheria na siyo kihisia kama unavyomaanisha eti Tanzania ni Tanganyika wakati Tanganyika+Zanzibar=Tanzania.
Sheria ipi unaizungumzia maana hati ya muungano inasomeka "Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar'
 
Sheria ipi unaizungumzia maana hati ya muungano inasomeka "Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar'
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kwenye kesi ya Machano Hamis and Others vs SMZ.
Kwenye hiyo kesi Mahakama ilisema kwamba Zanzibar siyo dola, na kwamba dola la Zanzibar lilikufa rasmi April 26, 1964 pale Tanganyika na Zanzibar ilipoungana na kuzaa nchi mpya inaitwa Tanzania.
Hivyo hivyo, pia dola la Tanganyika lilikufa rasmi siku ambayo Zanzibar lilikufa.
Hizo hati unadai ni za Muungano haziwezi kuwa na authority kuishinda Katiba
 
dah bush lawyer unasema constitution iko superior kwa Articles of Union umekula maharage ya wapi wewe!!??
 
dah bush lawyer unasema constitution iko superior kwa Articles of Union umekula maharage ya wapi wewe!!??

Maharage hayana uhusiano na taaluma yangu.

Hizo hati zenyewe zinazungumzia juu ya Muungano wa nchi mbili ambapo Tanzania imezaliwa.

Hata kama nchi ingeitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, still nchi ni moja tu!
 
Tanganyika ilikufaje wakati Zanzibar bado ipo,
Hapa ninazungumzia state, yaani dola; hakuna dola inaitwa Zanzibar, na hakuna dola inaitwa Tanganyika.
Sifa ya dola ni kuwa na:
1. Watu
2.Mipaka
3. Serikali
4. Uhuru ( wa kitaifa na kimataifa) yaani internal and external sovereignty.
Zanzibar ina watu, serikali, na mipaka ila haina UHURU wa kujiamulia mambo yake yenyewe kwa ukamilifu.
Kimataifa, Zanzibar haijulikani na haitambuliki kama dola huru, isipokuwa Tanzania ndiyo inatambulika na kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Zanzibar haina kiti UN. Haina uwezo kusaini baadhi ya mikataba ya kimataifa.
Uhuru wa ndani: Zanzibar haina Uhuru wa kulinda watu wake, isipokuwa, inategemea Tanzania.
Pia Zanzibar haina Uhuru wa kutunga na kusimamia sheria zake yenyewe.
Sharia zinatungwa na Bunge la Tanzania.
Kuhusu ulinzi, JWTZ ndiyo jeshi lenye dhamana ya ulinzi Zanzibar, na lipo chini ya Serikali ya Muungano.
Zanzibar is not a sovereign state, ONLY Tanzania is sovereign and Zanzibar is part of Tanzania.
Both Zanzibar and Tanganyika States died since 1964, April 26
 
Hiyo namba 8 ndio ujinga wa watanzania wengi ulipo! Ndo mana fisiem wanapenda ujinga huo coz wanautumia kama mtaji wao wa kisiasa
 
Mara nyingi hutokana na watawala ambao wanaongoza bila kufuata sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…