Hizi ndio nyayo vikanyagio vya Nabii Ibrahim, Jiwe dogo la mraba (Maqam Ibrahim) lililohusishwa na Ibrahim katika ujenzi wa Al-Kaaba

Hizi ndio nyayo vikanyagio vya Nabii Ibrahim, Jiwe dogo la mraba (Maqam Ibrahim) lililohusishwa na Ibrahim katika ujenzi wa Al-Kaaba

Hamchoki kuhangaika na dini yenu Mnachosha jamani huku hakuna maji kama mnayo maji njooni moshono ya chini mniletee maji
 
Bila shaka hapo ulipo sidhani kama una uwezo wa kutaja mababu zako 20 kwa mfuatano. Kama historia yako imekushinda kuitunza basi historia ya MUNGU huhifadhiwa na MUNGU mwenyewe, basi tambua ya kwamba sisi tunamkumbuka na kumtambua Ibrahim kwakua Yeye ni Baba wa imani ya Mungu mmoja (kuamini katika Mungu mmoja) na imani zote tatu zinazojulikana kama imani za Ibrahimu, ametajwa katika vitabu vyote vitatu Vitakatifu vyenye hadithi zinazoonyesha imani yake kwa Mungu mmoja.
Madhaifu yako ktk utunzaji wa kumbukumb yamekupa ujasiri wa kuamin ktk hadithi za kusadikika.
 
Ujinga mtupu! Abraham hajawahi kufika Saud Arabia. Umbali wa alikukuwa anakaa ( Israel) mpaka saudia ni zaidi ya km 760, ambayo ni sawa na Namanga - Dar.. kwa usafiri wa ngamia jangwani anafata nini huko? Acheni kudanganya watu kuonyesha hiyo sehemu ni takatifu, wakati tunajua kuwa ilikuwa ni sehemu ya kufanyia matambiko ya miungu Allat, Al- Uzza na manat. Hata Muhammad wakati amezaliwa alikuta utaratibu huo upo, na ukoo wake ulikuwa ni wanufaika wa sadaka/makusanyo na biashara ya kuwahudumia wale mahujaji wa kipagan. Makka Abraham hajawahi kwenda na hiyo sehemu waarabu walikuwa wanatambika na kuhiji kabla hata Ibrahim hajazaliwa
 
Hapo tunasoma historia ya mababu wa wenzetu na kuona ufahari na wengine kusafiri masafa kushangaa miguu ya Mababu wa Kiarabu huku sisi mababu zetu tunawaita Mizimu tena inayotisha kama hiyo haitoshi hata historia za Mababu zetu hatuzijui,

Inasikitisha
Unakuta mleta mada hata historia ya babu yake mzaa baba haijui. Takataka sana
 
Unakuta mleta mada hata historia ya babu yake mzaa baba haijui. Takataka sana

Mind colonization ilifanyika kwa ustaadi mkubwa sana , na kuhakikisha vitabu vyote vinajengewa udikteta mkubwa iwe biblia au quran, ushawahi kuona muumini anauliza swali lolote kutokana na yale aliyofundishwa? Jibu hakuna ni kwa nini? Ili kuendesha watu kwa amri moja,
 
WE MUONGO SANA.

IBRAHIM ALIISHI MESAPOTANIA. IRAQ.
AKAAMBIWA AENDE ISLAEL.

HUKO MECCA NI UONGO MTAKATIFU.
WAISLAMU MUOGOPENI MUNGU.
[emoji3] hawa ndugu zetu hata vijiweni story zao n kujimwambafai na dini yao. Huwa wanaonaga watu wa imani nyingine kama vile n mashemetani. Wanaamini dini yao ina nguvu kuliko zingine,

Kuna vitu vinachekesha na kutia hasira sana [emoji3]
 
Waafrika bado sana yani mnaabudu dini za mababu wa watu mnaacha babu zenu rudi kwenye asili yako siwalazimishi lakini
 
hizo nyayo hakuwa na vidole? nyayo za namna gani zipo hivyo jamani, tuwe angalau basi tunaheshimiana hata kidogo.
 
Back
Top Bottom