Hizi ndio sababu huwa sitaki kuwaweka ndugu kwenye biashara zangu, Ni heri niwape mitaji wafungue biashara zao wapambane kivyao !!

Hizi ndio sababu huwa sitaki kuwaweka ndugu kwenye biashara zangu, Ni heri niwape mitaji wafungue biashara zao wapambane kivyao !!

Umasikini ni swala la familia na utajiri pia.
Kuna Cha kujifunza Kwa watanzania wenyewe Asili ya Asia.
Naami wanao ndugu visirani lakini je,huwa wanadeal nao vipi?
Hao kitu cha kwanza lazima muwe wamoja na mtaishi wote nyumba moja, hii naona inasaidia sana na inafanya wanafki watambulike haraka na kufungishwa virago kurudi huko Asia
 
Mara ya mwisho kuonana na Ndugu Ni mwaka 2011 Nikiwa form one baada ya wao kunizuia nisiendelee na shule. Nikapambana huku namtanguliza Mungu, nikamaliza University, nikapata kazi sasaiv Nina maisha yangu na Sina habari nao. Huku Nimenunua kiwanja ambacho nimeandika waraka in case nikifa ghafla mwili wangu utazikwa hapa bila kuitwa Ndugu
Sio lazima udeal na ndugu directly kama Wana watoto basi chukua hao na uwekeze ktk ndugu zako kama wazazi ni visirani,hakika hutojuta.
 
Sisi
Umasikini ni swala la familia na utajiri pia.
Kuna Cha kujifunza Kwa watanzania wenyewe Asili ya Asia.
Naami wanao ndugu visirani lakini je,huwa wanadeal nao vipi?
Sisi kuna sehemu tunakwama mnoo, ndugu hapendi maendeleo yako, bado tunaishi maisha ya kila mmoja apambanie chake.
Mzee hata awe don vipi haingizi watoto kwenye utaratibu wake wa kuingiza fedha.
Ndugu wakiona una uafadhali woote watakuja hapo hapo.
Bado kuwangiana, ndugu anakuwangia usifanikiwe.
 
Hao kitu cha kwanza lazima muwe wamoja na mtaishi wote nyumba moja, hii naona inasaidia sana na inafanya wanafki watambulike haraka na kufungishwa virago kurudi huko Asia
Kuwa wamoja hicho kitu hakipo ila likija swala la Maslahi ni mwendo wa kuwajibisha na kupongezana .Kuwe hakuna undugu ktk biashara.
Undugu ni baada ya faida.
 
Sisi

Sisi kuna sehemu tunakwama mnoo, ndugu hapendi maendeleo yako, bado tunaishi maisha ya kila mmoja apambanie chake.
Mzee hata awe don vipi haingizi watoto kwenye utaratibu wake wa kuingiza fedha.
Ndugu wakiona una uafadhali woote watakuja hapo hapo.
Bado kuwangiana, ndugu anakuwangia usifanikiwe.
Sio hawapendi maendeleo ila hakuna kiongozi ndilo kubwa ila kila mtu anapenda maendeleo ila kila mmoja anataka awe juu ya mwingine kieshima .
Kuna mwandishi aliandika kitabu 48 laws of power.,kikubwa wengi wetu hatujui kucheza na hizi mbinu.
Kuwafanya baadhi ya wajuaji wajione ndio in charge lakini kumbe sio.
 
Biashara ntashirikisha familia yangu niliyoijenga (hasa watoto) ama familia niliyotokea (kaka, dada, wadogo zangu, wazazi), nje ya hapo hawa watoto wa mjomba, ma mkubwa, ba mkubwa, ba mdogo, ndugu flani, n.k. sidhani kwakweli, undugu uwepo na ninaweza kuwasaidia mitaji ama kuwasimesha pamoja na kuwa mteja wa biashara zao lakini tusiingiliane kwenye usimamizi wa Biashara zangu

Unakuta wafanyakazi wengine wanafika saa moja asubuhi ndugu anafika saa mbili ama tatu, Ndugu akiumwa hata mafua anaweza asije kazini, hii inanijengea chuki kwa wafanyakazi wengine kwa kuona nina upendeleo wa wazi wazi.

Kuna ndugu wanajikuta wao mabosi kuwa sawa na mimi kisa tu tuna undugu, wanapitiliza kuanza kuwavimbia wafanya kazi wengine, huanza kujiona miungu watu kwa wafanyakazi wengine, hawa ndugu wa kiume baadhi yao huanza kutumia nafasi hii kuwanyanyasa kingono wafanyakazi wa kike

Ndugu hasa wasio na majukumu wanaanza kunichora kwamba naingiza pesa nyingi, maneno yanaanza kupelekwa vijijini kwamba naingiza pesa nyingi lakini siwasaidii kwa uwiano wa kiasi nachoingiza, hapo hawajui kwamba nalipa marejesho ya mkopo, nalipa kodi, nalipa mishahara, nalipia ulinzi, n.k.
Hasa watoto wa mjomba ndio hawafai kabisa yaani

[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji120][emoji419][emoji419]
 
Unakuta mtu amemuweka Shemeji mdogo wa mke ndio Meneja😁.
Hio haijakaa sawa, lazima kutakua na gap hapo manager hapaswi kua ndugu hii nimeona sehemu jamaa aliharibu biashara wakamtimua ingawa dada yake hakupenda Ila kwa kua mdogo ake kaharibu ikabidi akubari shingo upande tu
 
Mara ya mwisho kuonana na Ndugu Ni mwaka 2011 Nikiwa form one baada ya wao kunizuia nisiendelee na shule. Nikapambana huku namtanguliza Mungu, nikamaliza University, nikapata kazi sasaiv Nina maisha yangu na Sina habari nao. Huku Nimenunua kiwanja ambacho nimeandika waraka in case nikifa ghafla mwili wangu utazikwa hapa bila kuitwa Ndugu
Tusamehe ndugu yangu,usitujumlishe wote,wakati huo mimi nilikuwa na mwaka mmoja!
 
Ngozi nyeusi tuna shida. Ukishalijua hilo utakuwa umetatua matatizo mengi sana.
 
Back
Top Bottom