Hizi ndio sababu huwa sitaki kuwaweka ndugu kwenye biashara zangu, Ni heri niwape mitaji wafungue biashara zao wapambane kivyao !!

Hizi ndio sababu huwa sitaki kuwaweka ndugu kwenye biashara zangu, Ni heri niwape mitaji wafungue biashara zao wapambane kivyao !!

Biashara ntashirikisha familia yangu niliyoijenga (hasa watoto) ama familia niliyotokea (kaka, dada, wadogo zangu, wazazi), nje ya hapo hawa watoto wa mjomba, ma mkubwa, ba mkubwa, ba mdogo, ndugu flani, n.k. sidhani kwakweli, undugu uwepo na ninaweza kuwasaidia mitaji ama kuwasimesha pamoja na kuwa mteja wa biashara zao lakini tusiingiliane kwenye usimamizi wa Biashara zangu

Unakuta wafanyakazi wengine wanafika saa moja asubuhi ndugu anafika saa mbili ama tatu, Ndugu akiumwa hata mafua anaweza asije kazini, hii inanijengea chuki kwa wafanyakazi wengine kwa kuona nina upendeleo wa wazi wazi.

Kuna ndugu wanajikuta wao mabosi kuwa sawa na mimi kisa tu tuna undugu, wanapitiliza kuanza kuwavimbia wafanya kazi wengine, huanza kujiona miungu watu kwa wafanyakazi wengine, hawa ndugu wa kiume baadhi yao huanza kutumia nafasi hii kuwanyanyasa kingono wafanyakazi wa kike

Ndugu hasa wasio na majukumu wanaanza kunichora kwamba naingiza pesa nyingi, maneno yanaanza kupelekwa vijijini kwamba naingiza pesa nyingi lakini siwasaidii kwa uwiano wa kiasi nachoingiza, hapo hawajui kwamba nalipa marejesho ya mkopo, nalipa kodi, nalipa mishahara, nalipia ulinzi, n.k.
Hao Ndugu umewaajiri au ni shareholders?
 
Jambo kuwa hata kama ni ndugu au mwanao Yuko kwenye production chain ya biashara yako au mradi lazima muwe na vikao vya mara Kwa mara alafu kila mmoja ajue responsibility zake na wewe ukiwa kama top leadership kikialibika kitu no excuse ila kama ujafanya job deligation Kwa kila mmoja itakuwa shida tupu .
 
Hao kitu cha kwanza lazima muwe wamoja na mtaishi wote nyumba moja, hii naona inasaidia sana na inafanya wanafki watambulike haraka na kufungishwa virago kurudi huko Asia
Utarudi vipi Asia ikiwa umezaliwa hapahapa Tz na ni Mtz pia ila tu una asili ya Asia?
 
Back
Top Bottom