Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 24,606
- 39,289
Kiongozi wa nini tena mkuu?Apana master mimi ndio nitakua kiongozi wenu huko mbinguni wewe tulia tu utaona
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi wa nini tena mkuu?Apana master mimi ndio nitakua kiongozi wenu huko mbinguni wewe tulia tu utaona
Nitakua waden kaka mkubwa.Kiongozi wa nini tena mkuu?
Sasa Hapo Wewe Uliambiwa Ni mbinguni???Unaweza kuthibisha hoja yako mkuu?
Ufunuo wa Yohana 7:9
Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
Baada ya hayo uliyoandika.
Ufunuo Yohana anaonyeshwa mambo makubwa kuliko upeo wake au wa mwanadamu maana ni mambo ambayo macho ya binadamu hayajawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia.Sasa Hapo Wewe Uliambiwa Ni mbinguni???
Ufunuo wa Yohana 21:1-3
"Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao."
Na kuhusu Hao 144,000
Ufunuo wa Yohana 7:4
"Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu."
Ufunuo wa Yohana 14:1,4
"Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo."
Sasa Kama Mbingu inashuka na Dunia Inashuka Na wanaoenda Mbinguni ni Hao 144..
Na ndo watakaohukumu wewe unataka kwenda Mbinguni kufanyaje
Humanism hii.Mbinguni ni hapa hapa Duniani,..... "TUNZA MITI TUNZA MAZINGIRA"
Fanya juhudi kumjua Mungu zaidi na kushika amri zake,usitegemee faraja za kibinadamu,Mungu ni Mwema ,mwenye huruma na Mwenye kusamehe kwa anaye mwabudu na kuzitenda amri zake.1: Mungu ananguvu kuliko shetani.
2: Mungu ametoa kila kitu cha lazima mtu yeyote atakaye kwenda aende. Hakuna alichobakiza.
3: Neema ya Mungu ina nguvu kuliko nguvu ya dhambi
4: Kwa Mungu unaweza kuwa muovu miaka yako yote ilq sekunde moja tu kama mwizi msalabani ukasema Unikumbuke katika ufalme wako tayari tiketi ikiwa umemaanisha.
5: Biblia inaonyesha watakeondea mbinguni ni wengi kama mchanga wa bahari. Yaani hawahesabiki. Hata wewe ukitaka unaenda.
Ni hayo tu.
Ingekuwa wewe ndiye mtoa hukumu ya ama kwenda peponi au motoni wewe ungeamuru wanadamu wote waende motoni isipokuwa wewe tu🤪Watu wote wataenda pepon isipokua waliokufuru na wakasema Mungu wapo watatu
Baada ya haya yote, watu wote hawa walitazamia mambo makubwa kuliko haya tunayoyaona. Ukifanya haya yote bila kutazamia mji mpya na nchi mpya ambao unatanguliwa na kukaa mbinguni ikulu hightable na Mungu huyo hakuna sababu ya kuamini uwepo wa Mungu.Fanya juhudi kumjua Mungu zaidi na kushika amri zake,usitegemee faraja za kibinadamu,Mungu ni Mwema ,mwenye huruma na Mwenye kusamehe kwa anaye mwabudu na kuzitenda amri zake.
Hata kama iwapo ni chawa mwambie tu ukweli na ukweli utampa kheri na barakaMatunduizi wewe ni mtu wa maana kabisa ujue😁😁😁
Yeah na Wakristo Wote wamo kwenye Hiyo idadi sio?Ufunuo Yohana anaonyeshwa mambo makubwa kuliko upeo wake au wa mwanadamu maana ni mambo ambayo macho ya binadamu hayajawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia.
Ili kusaidia angalau ujumbe utufikie kwa urahisi vingi angalau ameviandika kwa mtazamo na ufahamu wa agano la kale.
Karibu kila msamiati ikiwemo hiyo 144,000 anautoa kwenye agano la kale.
Hiyo ni hesabu ya kijeshi, formation ya jeshi la Israel. Ni namba ya uwakilisho maana yenye tafsiri ambayo inabeba wote hata wasio waisrael. Maana kwenye agano jipya Muislae au mzao wa Ibrahim sio myahudi bali ni Mkristo. Wagalatia 3:29. Ndio maana amewaandikia hizo barua wazungu wa mashariki ya ulaya wakati kitabu kimeqndikwa kwa mtizamo wa kiyahudi. Makanisa saba ya asia. East and central europe. Ujumbe ambao ulikusudiwa hadi kwetu.
Pia kuhusu sisi watu wengi kwenda mbingini biblia haijaandika kakifungu kamoja. Ni marundo ya mafungu mkuu. Najua wewe ni mwanataalimungu na msomi wa maandiko labda kama yamekukinai na umetumia kujenga msimamo mipya farijishi.
1 Wathesalonike 4:16
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
1 Wathesalonike 4:17
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Mwache abaki chawa huyo ni sikio la kufa hasikii dawaHata kama iwapo ni chawa mwambie tu ukweli na ukweli utampa kheri na baraka
Unaiita Takataka sehemu ambayo inakuhifadhi, unaposema Dunia ni takataka naomba unijibu swali hili kati ya Dunia na watu nani amepewa hukumu ya kufa ?Humanism hii.
Dunia sio sehemu salama ya kuishi. Ikiachwa miaka mingi ijayo itajisuicide. Kwa kuokoa haya inabidi Yesu aje atupe hii takataka na kuchomoa wanaopenda vitu vizuri, kisha kut3ngeneza nyingin4 kabisa.
Hii unayoipromote ni worst version ya vile ilivyopaswa kuwa. Utunze mazingira kwa sababu za kibaiolojia na kijiografia ila sio ili dunia iwe sehemu bora maana hilo limeshafeli miaka 6000 iliyopita
Mimi ninachoona hapa kwenye hoja zako ni ukosaji wa mtiririko au mpangilio.Yeah na Wakristo Wote wamo kwenye Hiyo idadi sio?
Maana na wenyewe Ni waisraeli wa Kiroho au naongopa? 😅
Nakupa Scenario Moja Ndogo unaporudi Nyumbani ukitoka kazini wanao wanapokulaki, baada ya Kukulaki Huwa Unawachukua unawapandisha Kwenye gari Unarudi nao kazini au Unawachukua Mnaenda nao Ndanu nyumbani???
Namaanisha Baada ya sisi Kumlaki au Kumpokea Yesu Tutampokea galafu tutaenda juu au tutampkea naye atakuwa Imanuel (Kwa maana Makazi ya Mungu ni pamoja na wanadamu) kama Ufunuo inavyosema..
Ufunuo wa Yohana 3:12
Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
mkuu Soma Ufunuo yako Na Biblia yako Vizuri Utaelewa tu..
Hakuna Mtu anaenda Mbinguni Mzee
Mimi ninachoona hapa kwenye hoja zako ni ukosaji wa mtiririko au mpangilio.Yeah na Wakristo Wote wamo kwenye Hiyo idadi sio?
Maana na wenyewe Ni waisraeli wa Kiroho au naongopa? 😅
Nakupa Scenario Moja Ndogo unaporudi Nyumbani ukitoka kazini wanao wanapokulaki, baada ya Kukulaki Huwa Unawachukua unawapandisha Kwenye gari Unarudi nao kazini au Unawachukua Mnaenda nao Ndanu nyumbani???
Namaanisha Baada ya sisi Kumlaki au Kumpokea Yesu Tutampokea galafu tutaenda juu au tutampkea naye atakuwa Imanuel (Kwa maana Makazi ya Mungu ni pamoja na wanadamu) kama Ufunuo inavyosema..
Ufunuo wa Yohana 3:12
Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
mkuu Soma Ufunuo yako Na Biblia yako Vizuri Utaelewa tu..
Hakuna Mtu anaenda Mbinguni Mzee
Umeongea Vizuri Ila hujaonyesha Ushahidi wa Kwe da Mbinguni ulioandikwa kwenye biblia zaidi ya maneno yako mwenyewe..Mimi ninachoona hapa kwenye hoja zako ni ukosaji wa mtiririko au mpangilio.
Maandiko yanasema vitu vyote viwili wewe unataka kuvimerge ili kukubwisha hoja yako kitu ambacho ni kosa la kimakusudi.
Tukizingatia biblia inasema kwa neno la mashahidi wawili shauri ninathibitika. Kuhusu watu wote kwenda mbinguni limesisitizwa kwa waandishi wa vitabu vya biblia zaidi ya kimoja akiwemo na Yesu mwenyewe atakayesimamia mchakato huo.
Pili Maandiko yamezungumzia jambo la pili katika mchakato wa kwenda mbinguni utafuatiwa na tukio la kuubwa upya maskani ya mwanadamu baada ya uteketezwaji wa huu uchafu dunia.
Mungu mmiliki wa dunia na sayari zaidi ya decillion katika ulimwengu kwa hiyari yake mwenyewe ataamua kuuunganisha maskani yake mbinguni na yale atakayowatengenezea wanadamu. Hii ni baada ya kuwachukua wote na makaburi kupasuliwa na watu wasiohesabika kwenda mbinguni aliko sasa Mungu.
Tena hawendi tu mbinguni wanaenda kukaa mahali pa hadhi ya juu sana ambapo hata malaika wa mbinguni hawajawahi kupaona hata kupafikia labda wale makerubi.
Kwenye kiti cha enzi na Baba yao.
Ufunuo wa Yohana 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Hoja yako imejengwa katika kuyafarakanisha maandiko na sio kuyaunganisha. Tukio ulilosimamishia hoja lako ni sehemu ya tukio la shamlashamla ya baada ya kuchukuliwa hapa duniani sio jumla kuu.
Yaani ni sawa na kipofu aliyeletewa tembo akashika sikio akaanza kubishia watu kuwa tembo anafanana na jani la gimbi au sinia. Kumbe anazungumzia sehemu ya tembo sio stori yote kuhusu mofolojia ya tembo. Mimi ninaposema mbinguni najumuisha package yote.
Kwa sasa huyu Mungu ikulu yake iko mbinguni na anaikulu ndogo katika subconscious mind yangu akitawala kutokea huko.
Yohana 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Kama mtu mwenye majini anavyoitwa kiti na Mkristo ni kiti cha Serikali ya Mungu. Hivyo hizo raha za kuingia mbinguni na makao mapya tutakayoishi naye zimeshaanza sasa kwa jinsi ya rohoni kwa kutembea ukiwa na convoy ya serikali ya mbinguni duniani. Kama ni mkristo na hauamini haya ni afadhali uwe atheist au mason maana utakuwa ni ukristo wa shida na taabu sana. Dini itakuwa ni mzigo mkubwa