Mimi ninachoona hapa kwenye hoja zako ni ukosaji wa mtiririko au mpangilio.
Maandiko yanasema vitu vyote viwili wewe unataka kuvimerge ili kukubwisha hoja yako kitu ambacho ni kosa la kimakusudi.
Tukizingatia biblia inasema kwa neno la mashahidi wawili shauri ninathibitika. Kuhusu watu wote kwenda mbinguni limesisitizwa kwa waandishi wa vitabu vya biblia zaidi ya kimoja akiwemo na Yesu mwenyewe atakayesimamia mchakato huo.
Pili Maandiko yamezungumzia jambo la pili katika mchakato wa kwenda mbinguni utafuatiwa na tukio la kuubwa upya maskani ya mwanadamu baada ya uteketezwaji wa huu uchafu dunia.
Mungu mmiliki wa dunia na sayari zaidi ya decillion katika ulimwengu kwa hiyari yake mwenyewe ataamua kuuunganisha maskani yake mbinguni na yale atakayowatengenezea wanadamu. Hii ni baada ya kuwachukua wote na makaburi kupasuliwa na watu wasiohesabika kwenda mbinguni aliko sasa Mungu.
Tena hawendi tu mbinguni wanaenda kukaa mahali pa hadhi ya juu sana ambapo hata malaika wa mbinguni hawajawahi kupaona hata kupafikia labda wale makerubi.
Kwenye kiti cha enzi na Baba yao.
Ufunuo wa Yohana 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Hoja yako imejengwa katika kuyafarakanisha maandiko na sio kuyaunganisha. Tukio ulilosimamishia hoja lako ni sehemu ya tukio la shamlashamla ya baada ya kuchukuliwa hapa duniani sio jumla kuu.
Yaani ni sawa na kipofu aliyeletewa tembo akashika sikio akaanza kubishia watu kuwa tembo anafanana na jani la gimbi au sinia. Kumbe anazungumzia sehemu ya tembo sio stori yote kuhusu mofolojia ya tembo. Mimi ninaposema mbinguni najumuisha package yote.
Kwa sasa huyu Mungu ikulu yake iko mbinguni na anaikulu ndogo katika subconscious mind yangu akitawala kutokea huko.
Yohana 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Kama mtu mwenye majini anavyoitwa kiti na Mkristo ni kiti cha Serikali ya Mungu. Hivyo hizo raha za kuingia mbinguni na makao mapya tutakayoishi naye zimeshaanza sasa kwa jinsi ya rohoni kwa kutembea ukiwa na convoy ya serikali ya mbinguni duniani. Kama ni mkristo na hauamini haya ni afadhali uwe atheist au mason maana utakuwa ni ukristo wa shida na taabu sana. Dini itakuwa ni mzigo mkubwa