Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

1.5m ndio mshahara mzuri brother?uko dunia gani mwenzetu?
Ndio wanalipwa vzr, mm nipo bodi ya korosho nakula 1.3+ ukitoa makato napata 980 na vichenji bado safari kila kukicha. Mwanajeshi ananizidi tu kwasabab wao hawana makato kama kodi ya mshahara na Chama cha wafanya kazi lakin pia wana mikopo ya gharama nafuu lakin pia mm naweza kukopa hazina kwa riba ya 4% tukaenda Sawa tu
 
1.5m ndio mshahara mzuri brother?uko dunia gani mwenzetu?
Kutokana na taasisi nyingi zilizotajwa na watu humu basi inaonekana kwa mtazamo wao huo ni mshahara mzuri, na kama huo siyo mzuri basi hakuna taasisi ya serikali inayolipa mshahara mzuri bongo kwa entry level, maana kumbuka huo ni mshahara wa luteni usu (nyota moja) ambaye ndio anaanza kazi, na hicho cheo ni cha muda mfupi tu baada ya mwaka huwa wanaveshwa nyota mbili na kuwa maluteni, hivyo mshahara nao kuongezeka
 
Ana degree yaan total yotr jumla inakua 1.5m
Hapana ukijumlisha na posho ni zaidi ya hiyo, kila mwezi wana posho ya chakula 300K, kila baada ya miezi mitatu wanapewa ration ya vinywaji 300K, kwa kifupi ukijumlisha mshahara na posho luteni usu anakunja 2.3M, hayo usitegemee utayaona kwenye salary slip mkuu
 
Zipo Kuna taasis entry level mwenue degree anaanza na 3.2M
 
Zipo Kuna taasis entry level mwenue degree anaanza na 3.2M
Mkuu nafahamu zipo taasisi zenye mishahara hiyo ila kwangu mimi 3M siyo mshahara mzuri sijui kwa wengine, mimi naandika kulingana na mitazamo niliyoiona kwa watu wengi humu, watu wakitaka kusikia mishahara mizuri kwa entry level, basi wakaulizie kwenye makampuni ya kuchimba madini au baadhi ya NGOs za wazungu, ila serikalini tunadanganyana tu
 
Sijaona NIMR, OSHA , TCA??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…