Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Posho ya TPDC Ni 250,000/night
 
Huku ukiingia na uhakika wa ajira permanent kutoka ni ngumu sana.
Kuna jamaa yangu wa karibu, aliingia kule MWAUWASA early 2000.

Kufikia 2002 alikuwa Don na mwaka huo akaoa, harusi ilikuwa ya kidon kabisa ingawa alipata support huko kazini kwake.

Bado yupo huko hadi sasa, kashapiga hatua ndefu sana.

Kumbuka huyo aliingia kwa sifa ya Diploma...
 

Mkuu huko ukibahatika kupata kitengo mambo ya kutaka kuhama utakuwa unasikia kwa wengine uhakika wa maisha kidogo upo kulinganisha na sehem nyingi tu.
 
Kuna mashirika ya umma
Salary scale ni 2.6m
Posho ya Nyumba 800,000/-
Extraduty 900,000/-
Transport 450,000/-
Kaka huyo anayelipwa hiyo ana cheo gani aisee 800,000 posho ya nyumba , hamnaga hiyo labda private sector..

Kama ni serikalin basi pesa zetu zinatumika vibaya
 
Tpdc degree 1.5M , diploma 1.1M hiyo kabla ya makato.

Ila kule kinacho wabeba ni perdiem nyingi ni nadra sana kukaa ofisini.

Kwenye maokoto ni kwenye mamlaka kama:-

1.TCRA( Perdiem nyingi na kusafiri sana)
2.EWURA( perdiem zake kubwa pamoja na mshahara mkubwa)
3.LATRA( mshahara mkubwa)
4.UCSAF( hapa usipimie mpunga mrefu sana)
5.MAMLAKA ZA MAJI ZA MAJIJI KAMA DAWASA, AUWSA, MWAUWASA, DUWASA

6.TRA( mishe nyingi za kupata hela ukiwa mtoto wa mjini)
7. TANROADS( makusanyo makubwa so perdiem nyingi)
8. TARURA( haina tofauti sana na tanroads)
9. NHIF( extra duty yao 900k pamoja na mshahara mkubwa ila hawana safari sana kwa nature ya kazi zao).
10. Hazina mshahara wao ni TGS.. Ila usipime maokoto yao extra duty yao tu 1.8M
 
Hiyo extraduty ya 1.8m itakuwa ni Uongo,
 
Mkuu hiyo namba 4. USCAS ndio taasisi gani hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…