Hizi ndio wizara ngumu ambazo zinahitaji mtu aina ya Magufuli kuziongoza

Hizi ndio wizara ngumu ambazo zinahitaji mtu aina ya Magufuli kuziongoza

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
3,952
Reaction score
8,807
Niaje waungwana

Siku ya leo ningependa kuangazia wizara 2 ambazo ni ngumu kiutendaji, na zinahitaji mtu aina ya Magufuli kuziongoza ili zilete ufanisi, au matokeo chanya kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Wizara hizo ni Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Mheshimiwa Abdallah Ulega. Na Wizara ya Ardhi inayoongozwa na Mheshimiwa Deogratius J Ndejembi.

Ki ukweli wizara hizi ni ngumu mno. Zinahitaji watu wenye misimamo thabiti, wachapakazi, wafuatiliaji wa kazi na maamuzi ya wizara, wapenda haki na maendeleo, wazalendo, na mwisho kabisa wafuataji wa sheria.

Sio mtu anapewa wizara ya ardhi au ujenzi kumbe mtu mwenyewe muoga, mvivu, hana uzalendo, hana muda na maendeleo. Matokeo yake hali inakuwa kama ilivyo sasa. Watu wanadhulumiwa nyumba zao, viwanja vyao nk huku waziri wa ardhi yupo lkn anaogopa kuingilia kati mpaka mkuu wa mkoa anaamua kuingilia swala ambalo waziri husika yupo na anapokea mshahara kupitia kodi zetu kila mwezi.

Ukija kwa upande wa ujenzi ndio kabisa mkoa wa Dar umekuwa mavumbi matupu. Barabara nyingi toka zianze kujengwa mpaka sasa ni miaka zaidi ya mitatu, lkn hakuna cha maana kinachofanyika, watu wanaumwa mafua kutokana na mavumbi, mji umechafuka, side walks (njia za watembea kwa miguu) pembezoni mwa barabara haziwekwi, ni mamichanga na udongo mtupu. Miradi haikamiliki, wajenzi wanaripua ripua tu ilimradi liende bila kuzingatia ubora wa barabara. Waziri yupo na hana muda wa kuchukua hatua stahiki za kuwafunga na kuwafukuza kazi watendaji wababaishaji kama alivyokuwa anafanya Jerry Silaa, au Magufuli wakati alipokuwa waziri.

Watu wa aina hii wanatuchelewesha sana kufikia malengo ya kweli, hivyo wanahitajika watu aina ya Paul C. Makonda kuongoza wizara ya Ujenzi, huku Jerry W. Silaa akirudishwa Ardhi akaendelee kuwashughulikia vizuri kina Alex Msama na magenge mengine ya uhalifu wa ardhi.

Hawa mawaziri wa sasa wabaki kwenye ubunge wao tu inatosha.
 
ofisi ngumu ni ofisi kuu ya rais. Hiyo ndio inahitaji mtu makini sio huyo mwanamama, huko kwingine ni matokeo ya ofisi kuu
 
Upo sahihi.

Ila kwa Makonda na Silaa umezingua, hao watu hawafanani na JPM hata kidogo.
Silaa alipokuwa waziri wa ardhi watu wengi waliodhulumiwa viwanja vyao na nyumba zao walipata haki zao hadi kupelekea wadhulumati kuishi matumbo joto.

Kwa upande wa Makonda huyu anaweza kuwa mpya wizarani, lakini katika utendaji ana uthubutu ukilinganisha na wengine.
 
Tatizo lipo juu!

Kama kichwa ni kibovu, mwili wote utakuwa mbovu,

Mawaziri watapambanaje na walaji wakati ni wakubwa wao?!

Kauli mbiu yetu ni KAZI NA UTU ndio UTU wenyewe huo! wakipambana nao wataambiwa hawana UTU ni makatili kama mwendazake! au wanafukuza na kubughudhi wawekezaji wakigeni.

kazi tunayo, mpaka mitano tena iishe tutakuwa tumebagazwa sana na kuchoka hoi bin taabani.
 
Wizara ya bata ni wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga taifa.Umeshawahi sikia bajeti yake ikibishaniwa bungeni kuwa tumenunua ndege vita kadhaa na vifaru kadhaa?.Umeshawahi sikia mbunge anasema natoa shillingi.

Ndio maa raisi mwinyi wa Zanzibar kipara chake kilikuwa kinameremeta kila siku ila sasa kaukwaa uraisi ulivyo mgumu mvi zimeanza kumtoka.
Salim Ahmed Salim na Prof Sarungi rip naye pia wote vipara vilikuwa vinameremeta sababu walishakuwa mawaziri wa wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga taifa.
Natamani mate wangu wa Azania Mwinyi asome hii message acheke kidogo nimeamua kumfurahisha mate wangu.
 
Umenichekesha san mkuu 🤣🤣🤣
 
Tatizo lipo juu!

Kama kichwa ni kibovu, mwili wote utakuwa mbovu,

Mawaziri watapambanaje na walaji wakati ni wakubwa wao?!

Kauli mbiu yetu ni KAZI NA UTU ndio UTU wenyewe huo! wakipambana nao wataambiwa hawana UTU ni makatili kama mwendazake! au wanafukuza na kubughudhi wawekezaji wakigeni.

kazi tunayo, mpaka mitano tena iishe tutakuwa tumebagazwa sana na kuchoka hoi bin taabani.
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom