Uchaguzi 2020 Hizi ndizo hoja zitakazomuangusha Dkt. Magufuli na kumpaisha Tundu Lissu kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Hizi ndizo hoja zitakazomuangusha Dkt. Magufuli na kumpaisha Tundu Lissu kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Mkuu jaribu kuukubali uchambuzi wa kina uliofanywa na hawa waTanzania wenzetu bila kuwa na uhafidhina kwa kutengua hoja walizoziweka mezani

Mkuu unafikiri kwa sababu wako USA wao ndio wachangia bora au upeo wao ni mkubwa kuliko mimi ambaye nipo Narungombe? Nakuhakikishia JPM hana mpinzani, hizi propaganda za mitandaoni hazitasaidia kitu. CCM wana wanachama ambao wamejiandikisha na wanauhakika wa kushinda kutokana na sera na mambo ambayo JPM amefanya.

Only a fool will believe that hakuna haki Tanzania. Je, USA kuna haki kuliko Tanzania? Lisu will never win any election fact. Mwanzo mlisema Membe ndio tishio. Wewe na akili zako unafikiri Lissu anaweza kuwa Rais? Stop dreaming, JPM will never lose this election come what may.
 
Ndugu yangu hizi flyovers zimetumia fedha nyingi za walipa kodi wa nchi hii lakini zimeshindwa kuleta ahueni ya foleni. Ni bora zipigwe nyundo na kujenga feeder roads. Duniani kote flyovers hazijawhi kutatua tatizo la foleni ndugu yangu. Fanya utafiti utaona ninachokuambia.
Zilikuwa za kupigiwa 10% alale mbele.
 
Mkuu unafikiri kwa sababu wako USA wao ndio wachangia bora au upeo wao ni mkubwa kuliko mimi ambaye nipo Narungombe? Nakuhakikishia JPM hana mpinzani, hizi propaganda za mitandaoni hazitasaidia kitu. CCM wana wanachama ambao wamejiandikisha na wanauhakika wa kushinda kutokana na sera na mambo ambayo JPM amefanya. Only a fool will believe that hakuna haki Tanzania. Je, USA kuna haki kuliko Tanzania? Lisu will never win any election fact. Mwanzo mlisema membe ndio tishio. Wewe na akili zako unafikiri Lisu anaweza kuwa rais? Stop dreaming, JPM will never lose this election come what may.
Ni wivu tu. Utakuua.
 
Mkuu unafikiri kwa sababu wako USA wao ndio wachangia bora au upeo wao ni mkubwa kuliko mimi ambaye nipo Narungombe? Nakuhakikishia JPM hana mpinzani, hizi propaganda za mitandaoni hazitasaidia kitu. CCM wana wanachama ambao wamejiandikisha na wanauhakika wa kushinda kutokana na sera na mambo ambayo JPM amefanya. Only a fool will believe that hakuna haki Tanzania. Je, USA kuna haki kuliko Tanzania? Lisu will never win any election fact. Mwanzo mlisema Membe ndio tishio. Wewe na akili zako unafikiri Lisu anaweza kuwa rais? Stop dreaming, JPM will never lose this election come what may.

Tupia hoja au hata nadharia za kina hapa Jukwaani tuone ushawishi wa CCM Mpya kwa wapiga kura

medium.com › one-of-my-political-...
One of my political mentors used to say that politics is a game of addition, not ...

3 Jan 2019 — One of my political mentors used to say that politics is a game of addition, not subtraction. It still amszes me how some activists treat their politics
 
Tupia data hapa tuone ushawishi wa CCM Mpya kwa wapiga kura
Unataka data zipi? Umeme tu kila kona ya Dar ilikuwa na magenerator madukani kelele mtindo moja mgawo wa umeme kila kona. Je, siku hizi vipi? Makusanyo ya Bandari sasa hivi yako kwenye Billion 5 na ushee kila siku achilia mbali Serikali ambayo ipo makini kwenye kila Jambo. JPM amewaacha wazungu wanatetemeka kwa sababu wanafahanu kinachofuatia. Afrika nzima itajikomboa kutokana na udhalimu wao. JPM hana mpinzani.



 
Unataka data zipi? Umeme tu kila kona ya Dar ilikuwa na magenerator madukani kelele mtindo moja mgawo wa umeme kila kona. Je, siku hizi vipi? Makusanyo ya Bandari sasa hivi yako kwenye Billion 5 na ushee kila siku achilia mbali Serikali ambayo ipo makini kwenye kila Jambo. JPM amewaacha wazungu wanatetemeka kwa sababu wanafahanu kinachofuatia. Afrika nzima itajikomboa kutokana na udhalimu wao. JPM hana mpinzani.




Faida ya Makusanyo hayo hayaonekani na hayana mgusu ktk maisha ya watu ndiyo maana wananchi wapiga kura hawaielewi sera hii ya mgombea wa CCM Mpya John Magufuli .

Watu hawali mabarabara ya mbali, ndege za ATCL, madaraja ya baharini wala kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Chato n.k kwa kifupi Maendeleo ya Vitu.
 
Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, naingia kwenye mada moja kwa moja. Katika andiko hili nimebainisha kinagaubaga mambo ambayo yatamuangusha Magufuli na kumuinua Hon Dr Tundu Antipas Lissu kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 kama ifuatavyo...
Naamini mbele ya niliyoyaona Mungu wangu anashuhudia akipenda Mimi ni mkatoliki tundu lisu atashinda kwa namna ambayo jeshi itabidi liingilie Kati.
 
12 October 2020
Kahama

Tundu Lissu, anaukaribia Urais 2020 Wana-Kahama wanamkubali , SwahiliVilla Online wafuatilia kampeni zake!


source : swahili villa
 
Faida ya Makusanyo haya hayaonekani na hayana mgusu ktk maisha ya watu ndiyo maana wananchi wapiga kura hawaielewi sera hii ya mgombea wa CCM Mpya John Magufuli .

Watu hawali mabarabara ya mbali, ndege za ATCL, madaraja ya baharini wala kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Chato n.k kwa kifupi Maendeleo ya Vitu.
Ndio uhuru huo wa kuamua, una siku chache sana hadi tarehe 28 whether you like it or not JPM ndiye rais na hao makuwadi wenu ambao mliwaandaa janja yao tunaifahamu hamchomoki. You are too late.
 
Mimi nimeapa siongei uongo CCM ikishinda huu uchaguzi hata nchi jirani hawataamini. Shida ni kwamba Magufuli ameitesa sana Tanzania hatujawahi kuishi kiree hivi eti kisa tunajenga madaraja.
 
Ndio uhuru huo wa kuamua, una siku chache sana hadi tarehe 28 whether you like it or not JPM ndiye rais na hao makuwadi wenu ambao mliwaandaa janja yao tunaifahamu hamchomoki. You are too late.
basi sawa maana chuki mliianza wenyewe kwa kuuwa watu mtaona watanzania watakavyowajibu mkiiba kura.
 
basi sawa maana chuki mliianza wenyewe kwa kuwa watu mtaona watanzania watakavyowajibu mkiiba kura.
Tuna wanachama waliojiandikisha hai ambao watapiga kura. nyie nani atawapigia kura? khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee Mlevi wa konyagi peke yake khe hkhe khe heeeeeeeeeeeeeeeeeee kwanza mpo nje ya Tanzania yanayotokea Tanzania mnasimuliwa tu Aibu! Mlijifanya kukimbia sasa tanzania kumenoga mmebaki na makapi tu ngoja mfe na corona.
 
basi sawa maana chuki mliianza wenyewe kwa kuuwa watu mtaona watanzania watakavyowajibu mkiiba kura.
Tulimuua nani? Wewe kwanza rudisheni pesa mlizokuwa mnachota NSSF? Pamoja na miradi yenu hewa ya Kigamboni?
 
Tuna wanachama waliojiandikisha hai ambao watapiga kura. nyie nani atawapigia kura? khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee Mlevi wa konyagi peke yake khe hkhe khe heeeeeeeeeeeeeeeeeee kwanza mpo nje ya Tanzania yanayotokea Tanzania mnasimuliwa tu Aibu! Mlijifanya kukimbia sasa tanzania kumenoga mmebaki na makapi tu ngoja mfe na corona.
We ongea kama mpumbavu ila CCM haipiti kabisa na shida sio CCM shida ni Magufuli siasa zake za kuuwa watu hebu tukuulize Ben Saanane Yuko wapi? Tujibu
 
We ongea kama mpumbavu ila CCM haipiti kabisa na shida sio CCM shida ni Magufuli siasa zake za kuuwa watu hebu tukuulize Ben Saanane Yuko wapi? Tujibu
Muulize mlevi wa Konyagi?
 
Tulimuua nani? Wewe kwanza rudisheni pesa mlizokuwa mnachota NSSF? Pamoja na miradi yenu hewa ya Kigamboni?
Miradi hewa ya kigamboni unamuuliza Nani? Kwani hatukuwa na mamlaka ya nchi? Iulize mamlaka ya nchi chini ya rais John momose cheyo UDP ndio walioitawala Tanzania mwaka Jana.
 
07 October 2020
Nachingwe, Lindi
Tanzania

Kampeni za CHADEMA kuwania Urais 2020
Wananchi waamua basi, na kusema kwaheri CCM Mpya, kwaheri John Pombe Magufuli, karibu CHADEMA 2020 karibu Tundu Lissu


MAELEZO NA HISTORIA KUHUSU MKOA WA LINDI

Historia ya Mkoa wa Lindi


Mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza Mkoa wa Lindi haukuwapo kabisa katika ramani. Kilichokuwapo wakati huo ni Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya sasa ya Lindi Mtwara na Ruvuma. Makao Makuu ya Jimbo hilo la Kusini yalikuwa katika Mji wa Lindi.

Hadhi ya Mji wa Lindi kuwa Makao Makuu iliishia mara baada ya Uhuru ambapo Jimbo la Kusini likawa linajulikana kama Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu yakawa ni Mji wa Mtwara. Yamkini Mkoa wa Mtwara ulikuwa mkubwa sana kwa eneo hata Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mtwara Bwana John Nzunda alikuwa anasema:

“Natawala kipande cha nchi toka Pwani ya Bahari ya Hindi hadi Ziwa Nyasa na kutoka Mto Ruvuma hadi karibu na mto Rufiji.”

Serikali wa awamu ya kwanza Iliyoongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliugawa Mkoa wa Mtwara miaka ya mwanzo ya Uhuru ambapo kukawa na Mikoa ya Mtwara na Ruvuma. Mgawanyiko huu uliifanya Lindi kuwa ndani ya Mtwara.

Julai 1, 1971 ndipo Mkoa wa Lindi ulianzishwa rasmi baada ya tena kuugawa Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu ya Mkoa yakawa Mji wa Lindi. Wakati Tanzania inaadhimisha Miaka 10 ya Uhuru wa Bara kwa kuwaita Waingereza kuja kuiona hatua iliyopiga Mkoa ulikuwa na umri wa miezi 6 tu.

Eneo

Mkoa wa Lindi unapakana na Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, Mkoa wa Pwani upande wa Kaskazini, Morogoro na Ruvuma upande wa Magharibi na upande wa Kusini ni Mkoa wa Mtwara.

Mkoa una eneo la kilometa za mraba 67,000 ambalo ni sawa na asilimia 7.1 ya eneo la Tanzania Bara. Hata hivyo karibu asilimia 27 ya eneo la Mkoa lipo chini ya mbuga ya Selous (Selous Game Reserve) ambayo iko Magharibi mwa Wilaya ya Liwale.

Utawala

Mwaka 1971 Mkoa wa Lindi ulianza ukiwa na Wilaya 3 – Lindi, Kilwa na Nachingwea. Wilaya ya Liwae ilianzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Nachingwea mwaka 1975 na Ruangwa ilianzishwa mwaka 1995 kwa kuigawa Wilaya ya Lindi. Zipo Halmashauri 6 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Halmashauri za Wilaya za Lindi, Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa.

Pia Mkoa una jumla ya Tarafa 28, Kata 152, Mitaa 117, Vijiji 526 vilivyoandikishwa, Miji Midogo 3, (Kilwa Masoko, Kilwa Kivinje na Nachingwea), vitongoji 2,429 na Majimbo 8 ya Uchaguzi na Wabunge wa Viti Maalum 2.

Hali ya Hewa

Kwa wastani hali ya hewa katika Mkoa huu ni ya joto la kati ya nyuzi joto 24C hadi 27C na joto hili hutegemea sana pepo za bahari zinazovuma katika kipindi husika kwa mfano pepo za Kusi ni za baridi na Kaskazi huleta joto. Sehemu za miinuko zilizoko kati na Kaskazini kama Rondo, Kilimarondo, Kipatimu na Mpigamiti hali ya joto hupungua na kuonyesha tofauti za nyakati za joto na baridi.



Mvua


Mvua hunyesha mwezi Novemba mpaka Aprili na hali ya ukame kati ya Januari na Februari, Agosti hadi Oktoba. Wastani wa mvua kwa mwaka ni Milimita 750 – 1,200.



Idadi ya Watu


Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Lindi una jumla ya wakazi 864,652 wanaume wakiwa 414,507 na wanawake 450,145.



Makabila


Mkoa una makabila mbalimbali ambayo ni Mwera, Makonde, Ngindo, Matumbi, Machinga, na watu wachache wenye asili ya Asia na Kiarabu.

Dini

Mkoa wa Lindi una Dini zifuatazo: Wakristo 30%, 45% Muslem, Hindu 0.01% wengine 24.09%

Uchumi

Uchumi wa Mkoa wa Lindi unategemea sana sekta ya kilimo ambayo asilimia kubwa ni kilimo cha kujikimu na biashara kiasi. Hata hivyo vipo vyanzo vingine vya kiuchumi ambavyo ni Uvuvi, Ufugaji nyuki na Mifugo, Madini, Viwanda vidogo na vya Kati.

Huduma za Jamii

Mkoa unatoa huduma za jamii (ambazo ni Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na Michezo) katika Mkoa utoaji wa huduma hizi umeendelea kupanuka kulingana na malengo ya serikali ya kuwasogezea wananchi huduma mahali walipo. Changamoto iliyopo ni ufinyu wa bajeti lakini Mkoa unaendelea kutoa huduma bora na kwa viwango vinavyostahili.

Mawasiliano Na Uchukuzi

Mawasiliano, Huduma za posta, Telefax, Internet na Telex zinapatikana katika miji yote iliyotajwa hapo juu. Kwa upande wa usafiri Mkoa umeunganishwa na Wilaya zake zote kwa barabara zenye jumla ya kilomita 7,118 kati ya hizo kilomita 1200 ni za lami.

Mkoa una Bandari maji mbili za Lindi na Kilwa, bandari ya Lindi kwa sasa ipo katika matengenezo lakini ya Kilwa inaendelea kufanya kazi. Kwa upande wa viwanja vya ndege kipo kiwanja chenye barabara 6 ambacho sio cha lami. Kilwa na Nachingwea vipo viwanja vyenye barabara moja. Liwale kipo kiwanja cha kutua ndege ndogo.

Pato la Mkoa

kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2009 Pato la mkazi kwa mwaka lilikuwa shilingi 767,948 na mwaka 2015 liliongezeka na kufikia shilingi 1,901,044 hili ni ongezeko la asilimia 148 kwa wastani wa ongezeko la asilimia 21 kwa mwaka. Pia pato la Mkoa limeendelea kuongezeka kutoka shilingi 695,361,000 mwaka 2009 hadi kufikia shilingi 1,690,403,000 mwaka 2015, hili ni ongezeko la silimia 143 kwa wastani wa silimia 20 kwa mwaka. Pamoja na kuwepo kwa ongezeko hilo la kipato bado kumekuwepo na changamoto kubwa ya umaskini miongoni mwa wananchi, hivo basi Serikali ya Mkoa inaendelea na jitihada za kuwahamasisha wananchi wote wenye uwezo wa kufanya kazi wafanye kazi ili kuendana na kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU”.

JEDWALI NA. 3: PATO LA MKAZI NA PATO LA MKOA KWA KIPINDI CHA 2009 – 2015


Mwaka
Pato la Mkazi kwa mwaka (per capita)
Pato la Mkoa kwa mwaka(GDP) (000)
2009​
767,948​
695,361​
2010​
913,678​
843,880​
2011​
1,061,282​
999,604​
2012​
1,341,117​
1,159,599​
2013​
1,503,942​
1,312,577​
2014​
1,677,336​
1,482,763​
2015​
1,901,044​
1,690,403​

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS, 2016).
Historia | Lindi Region
NB: Takwimu hizi zinaonyesha kwamba, kwa wastani wananchi wa Mkoa wa Lindi, wamevuka kiwango cha umaskini uliokithiri cha watu kuishi chini ya dola moja kwa siku.
 
Back
Top Bottom