Hizi ndizo Sababu kuu 4 za Ufisadi Tanzania

Hizi ndizo Sababu kuu 4 za Ufisadi Tanzania

Habari Wana JF,

Ufisadi Tanzania sio kitu kigeni nimekaa kwa kipindi kirefu, nimefanya Utafiti usio rasmi nimegundua kuna vitu vinne ambavyo vinafanya uendelee kuwepo kama Ifuatavyo:

1. KATIBA, kwanza haina makali pili viongozi wengi hawawajibiki kwa Wananchi, wanafanya kazi kwa ajili ya mamlaka ya Uteuzi sio wananchi. Hivyo tunahitaji katiba mpya.

2. CCM, chama hiki kina watu wengi ambao wako kwa ajili ya maslahi yao tu kibaya zaidi wana mizizi mikubwa sana suluhisho ni kukitoa kwa namna yoyote ile .tatizo ni nani wa kumpa

3. UMASKINI, wananchi wengi ni maskini sana hivyo moja wako bize kutafuta kula yao kuliko mambo ya Taifa pili wanapoteza ujasiri na uthubutu wa kuweza kuhoji mambo yanayoendelea, kikubwa wanajawa hofu.

4. UDUMAVU WA AKILI, nimefuatilia nimegundua Watanzania wengi walipata shida ya afya ya akili sababu kubwa nikapata ni lishe duni wakiwa watoto ,Ndio maana watu wanapiga pesa watu wanaangalia na wengine wako bize kwasifia /kuwapongeza na kuwatetea

Hivyo kuna haja ya kutafuta suluhisho la hivi vitu ili Nchi iwe kuendelea.
Kinana fisadi mkubwa. Hawa ndiyo wako CCM kwa ajili ya matumbo yao. Magufuli alikuwa kiongozi mbaya sana, ila walikoofishana na Kinana kwa sababu alimkatia mirija yake. Sasa hivi amerudi kwa kasi sana na anapiga mbele, nyuma, kila upande kama mchwa!
 
😂😂😂 daa
 
Kuna ushahidi lakini?
 
Tatizo watanzania hatuelewi tunataka nn mlimtukana sana mwendazake leo hii mnalia na mafisadi.
 
Back
Top Bottom