Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ndugu yangu Nyerere katuachia utajiri mkubwa sana,madini yapo,mito na maziwa,mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, amani na utulivu vipo sasa unamlaumu kwa lipi familia yake yenyewe masikini kila kitu ametuachia sasa sijui unamaanisha nini?
Miaka 25 alikuwa anafanya Nini hasa?
 
Maendeleo yapi yanayolingana na Miaka 25?

Unajua Maendeleo wewe? Bora Wazungu
 
Na hakuwahi kujiita Dokta kama hawa wa sasa.
 
Nadhani Vita vya Uganda vya 1978/79 ndio chanzo kikuu.
Hapo alichemka hiyo vita ya kumbeba mshikaji Obote kwa gharama zetu. Na hakuna awezae kusema ukweli wa hii vita, ni kama Azimio la Arusha tu.
 
Uko sahihi. Kila kiongozi anakuwa na vipaumbele vyake. Mwalimu alijali ELIMU NA UKOMBOZI. Kilimo alikihubiri sana. Nchi hii imewahi kufuta ujinga kwa kuwa na wenye elimu walao kusoma na kuandika zaidi ya 80%. Moaka mwaka 1988, elimu mpaka chuo kikuu ilikuwa BUREEEEEEE. Alipambama na ukombozi. Barabara ilikuwa shida. Kutokana na ukombozi. Mikoa ya Mtwara na Lindi ilipata shida sana. Mfanyakazi aliyehamishiwa huko aliacha kazi siku hiyo hiyo. Ilichikua wiki kwenda Mtwara hasa wakati wa masika.
Anywa ALIHESHIMIKA SANA kwa sababu alisimamia misingi yake.

Sent from my TECNO KG5k using JamiiForums mobile app
 
Kabisa kabisa !! Hata hao wamagharibi walimuheshimu sana kwa hilo !!
 
Kama wasovieti wangekuwa wanampa pesa nyingi asingelazimika kwenda kuomba mkopo wa IMF na World Bank na ndicho kilichopelekea yeye kuachia madaraka kuliko kukubali masharti aliyopewa ya kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania. !!
Uchumi wa soviet ulikufa ikawalazimu kila nchi ya kijamaa kustruggle kivyake hapo ndio tatizo lilipoanza (cuba ilipata shida sana hadi ikabadili sera zake za uchumi, china wakajiongeza chap wakaadopt mixed economy, tanzania tukabaki hatujui tunataka nini hadi leo bora liende..
 
Ukisikiliza hadithi zinazosimuliwa na hawa wapuuzi utadhani Mwalimu hakuwa na akili, tena wanapindisha taarifa waonekane wajuaji, kumbe ni limbukeni tu.

Hapana dollar ilikuwa kwenye Tsh 7 hivi siyo tano.

Sasa angalia wanayohimiza hao hao World Bank na IMF katika kukopesha ili hatimae kunufaisha hayo hayo mataifa yaliyoendelea. Mkazo wao ni sekta binafsi, ambayo ni mashirika hayo hayo ya huko wanakotunyongea.

Ukiwasikiliza vizuri akina Samia, utadhani maendeleo yetu yatatokana na hao hao wanaokuja hapa kuzoa mali zetu huku sisi tukikenua meno tu kama vichaa!
 
Hoja yangu iko kwenye Ujamaa wa Nyerere. Yeye aliamini katika Ujamaa pekee na kuupinga kabisa ubepari; jambo ambalo halikuwa sahihi kwa mtazamo wangu.
Mkuu, hili ulilitoa wapi, kwamba Mwalimu Nyerere "alipinga kabisa ubepari". Umewahi kusoma Azimio la Arusha?

Lakini pamoja na hayo, nyakati hubadilika, na kwa mtu mwenye uelewa kama Mwalimu asingeng'ang'ania kitu ambacho haoni manufaa yake na hasa wakati husika umebadilika; kama ulivyobadilika duniani kote.

Wengi wanapotosha kabisa lengo la Ujamaa hasa lilikuwa nini. Nadhani lawama zinaanzia hapo kwa kutojua madhumini yake yalikuwa ni nini.
 
Exactly !! Ujamaa pamoja na mambo mengine mengi mazuri lakini pia ujamaa ulikuwa ukiwatengenezea uzalendo wananchi wa kuipenda nchi yao na kulinda rasilmali za nchi zisiweze kuibiwa au kufisidiwa na kikundi chochote kile ambacho kingejaribu kufanya hivyo! Iwe ni cha kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…