Hizi ndizo zama za kila mtu abebe msalaba wake, njia ya msalaba

Hizi ndizo zama za kila mtu abebe msalaba wake, njia ya msalaba

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Shida zako zilikuwa za familia, ukoo na jamii nzima.

Furaha yako, ilikuwa ya familia, ukoo na jamii nzima.

Mtoto wako alikuwa wa familia, ukoo na jamii nzima.

Maadili yako yalikuwa ya familia, ukoo na jamii nzima.

Huko ndiko tulipotoka, tumefika hapa ndiko tuliko katika njia ya msalaba, kila mmoja aubebe wake, na hakika hatujui ni mabaya yapi yatakayotupata.

Nguvu na uwezo wa Mwanadamu upo katika upendo, yote yawezekana palipo na upendo. Upendo ndio Maisha.
Nguvu binafsi haziwezi kufua dafu, zitagonga mwamba, na anguko kuu ni hakika.

Kila mtu Lakwe, kila mtu afanye atakavyo, kila MTU atatue yake, hakuna kuingiliana hapa. Huo ndio Uhuru wa kizazi kilichoanguka. Uhuru wenye utamu wa muda, lakini baadaye utazua Msiba na kilio kikuu, Kila MTU atalia, lakini ili kila MTU alie ni hakika hakutokuwa na familia, wala koo wala jamii. Kwa maana kwenye ubinafsi na kila MTU kubeba msalaba wake ni kufuta familia na koo na jamii. Naam hiyo ndio namna Bora ya kuiangusha jamii.

Zama za sasa matatizo ni yako mwenyewe, Kwa sababu kila MTU alitaka maadili yabinafsishwe yawe ya mtu binafsi, yaani kila MTU ajiamulie maadili yake mwenyewe, badala ya jamii kuamua maadili ya Watu wake.
Hivyo kila MTU atashughulika na matatizo yake mwenyewe.

Hadhi na kile kilichoitwa utu wa Mwanadamu vitaanguka Rasmi, Watu hawatakuwa binadamu tena, wala hawatakuwa wanyama kwani hata wanyama wana hadhi Yao na Maadili Yao. Watu watakuwa zaidi ya Wanyama. Ushoga ndio itakuwa ni hiyari ya MTU.

Kama hiyo haitoshi, Baba kufira au Kufirwa na kijana wake haitakuwa Jambo la kushangaza, huo ndio Uhuru unaokuja, Mama kulala na kusagwa na Binti yake itakuwa NI Haki yake. Nani atajali, nauliza Nani atajali.

Kwa sababu Uhuru wa wapumbavu haujali maadili ya jamii au hadhi ya binadamu.

Nani atashangaa siku Kijana akitaka kuoa Mama mkwe na Binti yake, huku muda huohuo akiwa analiwa kiboga na Baba Mkwe, Nani atashangaa ikiwa kila mtu atabeba msalaba wake. Haitakuwa jamii tena, haitakuwa Dunia tena, na wala hakutakuwa na watu wenye utu, wala binadamu wenye Maadili. Ni Ile Njia ya MSALABA, ndio ni kuubeba msalaba wako mwenyewe, kisha usihukumu usije ukahukumiwa.

Usihukumu Kwa sababu sheria zimefutwa, ikiwa sheria zimefutwa utahukumu Kwa namna ipi? Kuondoa sheria ni kuondoa Maadili, kuondoa Maadili ni kuondoa upendo, na kuondoa upendo ni kuondoa utu wa binadamu.

Taikon unazungumzia Jambo Gani? Subiri!

Uhuru na Msalaba, Usawa na mateso ya kuangikwa, kusulubishwa, na maangamizo. Kisha Mauti, hayo yote ni matokeo ya Zama Hizi.

Kwenye Uhuru na usawa kila mtu anahaki Sawa Mbele ya sheria, lakini sheria ipi hiyo ikiwa ilishafutwa na walioamua kila MTU ABEBE msalaba wake? Ikiwa kila mtu itampasa kubeba msalaba wake, basi hakuna Uhuru na usawa Mbele ya Haki, Kwa sababu penye Haki sheria itakuwepo, penye sheria upendo ungalipo.

Uzito WA msalaba baina ya wabeba misalaba sio Sawa, iweje Uhuru uwe sawia, familia, koo na jamii Kwa ujumla tangu kale zilifahamu mambo haya, ndio maana mambo yote yalikuwa Chini ya familia, koo na jamii ili kusawazisha uzito WA misalaba ya wanajamii na kuchonga Njia za misalaba. Lakini kizazi hiki Kwa upofu na upumbavu hakikuona hayo.

Ikiwa hautaki kuamuliwa mambo yako, Tabia zako, basi hakuna atakayebeba matokeo ya mambo na tabia zako. Huo ndio mpasuko na anguko Kwa Vijana wa kileo.

Hata hivyo, Taikon anawausia wale wachache wanaopenda mambo Yao na familia na koo zao ziendelee kuwa na Upendo, kuwa wamoja, wenye ushirikiano. Hasa wanaume wenye Familia, Vijana na wakinababa. Jitahidini kuhakikisha msalaba wa wanafamilia unashughulikiwa na Watu wote ndani ya familia.

Uhuru udhibitiwe kadiri itakavyowezekana. MKE na watoto wasiwe huru kupitiliza isipokuwa uhuru wa kulinda maadili na hadhi ya binadamu. Ni Bora mwanafamilia yeyote atakayevuka mipaka ya kuiangusha hadhi na Maadili ya binadamu ndani ya familia aangikwe na kusulubishwa, na kuangamizwa kisha Mauti Kwa sababu ya kulinda hadhi na Maadili ya Mwanadamu. Hivyo ndivyo utakavyoweza kuubeba msalaba na kuuondoa uovu katika familia, ukoo na jamii yako.

Lakini huruma yoyote Ile inapuuza waharibifu wa hadhi na Maadili ya Mwanadamu hiyo sio huruma Bali ni Roho chafu, na kuiangamiza familia yako. Hata hivyo, usiingilie mambo ya koo na jamii zingine isipokuwa Kwa kuombwa msaada.

Acha nipumzike, ni Yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli.

Ijumaa Kareem

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Zamani ilikua mtoto ni wa jamii nzima, unaweza kukutwa na jirani unafanya ujinga atakutia viboko njia nzima mpaka kwenu na ukifika huko maza nae anakuongezea. Lakini siku hizi mambo yamebadilika, mguse mtoto wa mtu uone kitakachokutokea.
 
Zamani ilikua mtoto ni wa jamii nzima, unaweza kukutwa na jirani unafanya ujinga atakutia viboko njia nzima mpaka kwenu na ukifika huko maza nae anakuongezea. Lakini siku hizi mambo yamebadilika, mguse mtoto wa mtu uone kitakachokutokea.
Halafu Watu haohao wanataka msaada kwenye matatizo
 
Kama vipi tujoin forces na elon musk kwenye mpango wake wa Mars colonisation
 
Back
Top Bottom