Winifrida Meshack
New Member
- Sep 18, 2023
- 2
- 3
Tunaomba mamlaka husika zifanye uchunguzi kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi na watumishi katika Ofisi za Wizara ya Ardhi Mwanza, ili zipatiwe ufumbuzi wa kudumu.
- Changamoto ya vyoo vya matumizi ya pamoja
Jengo hilo lina mlango mmoja wa kuingia kwenye eneo la vyoo, ambavyo vinahusisha vyoo vitatu pekee. Kati ya hivyo, viwili vinatumika na jinsia zote pamoja na wananchi na watumishi. Hali hii imekuwa ikileta usumbufu, hasa kwa wanawake wanaohitaji faragha kwa huduma maalum kama kubadili pedi, kutokana na hofu ya kukutana na wanaume wanaotumia eneo hilo. - Ufinyu wa jengo na usumbufu wa upatikanaji wa huduma
Jengo la Wizara ni dogo kiasi kwamba baadhi ya watumishi wamelazimika kufanya kazi katika ofisi za nje ya jengo kuu. Hali hii inaleta changamoto kwa wananchi, hususan wazee na watu wenye ulemavu, ambao hulazimika kutafuta ofisi mbalimbali zilizotawanyika ili kupata huduma wanazohitaji. - Wananchi kukosa eneo la kusubiri huduma kwa staha
Kutokana na ufinyu wa nafasi, wananchi hulazimika kusubiri huduma wakiwa nje ya jengo, na wakati mwingine kuhudumiwa kupitia madirisha. Hali hii huwaweka katika mazingira yasiyoridhisha kutokana na vumbi linalosababishwa na magari yanayoingia na kutoka kwenye eneo la maegesho ya watumishi, ambalo pia linatumika karibu na eneo la huduma kwa wananchi.