1,hela siku zote zinahesabika kwa mkono,ila pesa haiwezekani lazima mashine ihusike.
2,chenji elfu 10 upewe 500 tupu kama zitakaa ktk wallet,vipi una pesa tayari?
3,wasifu hauhusiani na pesa kama maprof wengi wana status ila pesa hawana.
4,ndege[emoji28][emoji28],acha ushamba bana.
5,23mln kwa mwaka ni sawa na ave 1.8 per month,huyu mtu hata kipato cha kati cha juu hayupo,bado ni masikini.
6,kama unatumia 70mln kununua gari kati ya masikini wanaoweza kufikiri unatapanya pesa,bado u kati yao,ili uwe ni fogo kakae masaki ambapo ukinunua gari la 70mln unapongezwa.
7,haya mambo wanafanya masikini waliopata pesa za ghafla,wanaotafuta hela toka chini huwa hawaachi kuuliza bei.
8,kufanikiwa hakutegemei ndumba au njia haramu ila utajiri lazima mbinu haramu zitumike,ukitaka kunielewa nenda kaanze kulima matikiti ukisikilizia mtaji kufika tsh 1bln,utagundua ni kwa namna gani ni ngumu kuwa tajiri.
9,kuomba hela mpaka tusikie tusio husika ni ufukara,lakini kutoa pesa mpaka tusiohusika tusikie ni umasikini.
10,usichanganye msaada na biashara,ukitaka kufanya msaada unawezanunua mboga ya 250 kwa elfu 5,ila ukisimama kama mteja tu,utagundua 50 utakayopunguziwa inawezanunua kitunguu.