Habari waungwana.
Kuna jamaa alinipigia simu kuwa kuna kampuni inatafuta mtu wa nafasi fulani. Basi nikamwambia wape namba ya simu.
Nikapigiwa simu kwamba nitume Cv, nikawatumia cv halafu ikawa kimya karibu mwezi basi mimi ikawa nimeipotezea tu hiyo kazi.
Baadae nikapigiwa simu na kufanyiwa interview kwa njia ya simu na baada ya kumaliza nikaambiwa niwasiliane na hr. Nikatumiwa namba ya simu ya hr.
Nikampigia hr hakupokea simu, basi ikabidi nimtumie ujumbe whatsap na kujitambulisha, akanijibu kuwa niende ofisini.Nikamjibu sawa ila ofisini nitakuja kesho kutwa kwa sababu niko mbali na ofisi kwa maana natokea umbali wa zaidi ya km 900 , akawa kimya.
Nikasafiri na kufika ofisini na kukutana na hr na tukakubaliana malipo. Baada ya makubaliano nilitegemea nitapewa mkataba ila cha kushangaza hr akaniambia atanitafuta. Basi nikaondoka na kwa vile nilitegemea labda nitaitwa ndani ya siku tatu ikabidi nibaki karibu naofisi lakini ikawa kimya.
Ikabidi nimuulize HR kwa njia ya whatsap sababu ukipiga simu hapokei. Nikamuuliza kama mchakato bado bado je naweza kurudi nilikotoka ambako ni zaidi ya km 900? Hakujibu mpaka leo na ni zaidi ya wiki.
Je, wadau hizi si ni dharau maana sipewi ushirikiano na hr na labda hata kuniambia kuna vigezo sijakidhi kwa upande wake maana boss wake ashanikubali. Yaani wamefanya nisafiri km zaidi ya 900 kwenda kunegotiate malipo halafu baada ya makubaliano wanapiga kimya.
Je, hakuna sheria ya kuwa shake ili hizi dharau na kuingizana gharama kwa namna hii isijirudie?